Jinsi Ya Kuingia Katika DM Ya Mwanamke, Umsisimue Na Ajibu Meseji Yako


Mitandao ya kijamii imerahisisha mawasiliano baina ya watu. Pia mitandao imewezesha wengi kuweza kupata wachumba. Kiufupi mitandao ya kijamii imeleta urahisi na raha katika mawasiliano.

Mtandao ya kijamii ukiijua kuitumia vizuri itakusaidia sana. Unaweza kuutumia kuwasiliana na wenzako, kujenga jamii, kufanya mawasiliano na kadhalika. Je kwa upande wako mitandao ya kijamii imeweza kukurahisishia upande upi?


Hapa Nesi Mapenzi, mitandao ya kijamii tunaiangalia na taswira tofauti, nayo ni kuitumia kutafuta wachumba. Mitandao yenyewe ni kama vile Instagram na Facebook. Unaweza kumtumia jumbe mwanamke na mwisho ukafaulu.

Kabla tuingie kwa mada, neno DM linamaanisha Direct Message. Huku ni kule kumtumia mtu meseji kwa kuingia kwa inbox yake na hakuna mwingine anaweza kusoma jumbe zenu.

Sasa unajua ni mbinu zipi ambazo unaweza kutumia hadi ukaunasa moyo wa mwanamke na kuanza kukutumia jumbe mara kwa mara?

Zama nasi.

#1 Kuwa original. 
Wakati ambapo umeamua kuingia katika DM ya mwanamke, hakikisha ya kuwa meseji yako inakuwa original. Usiige meseji za watu ama meseji ambazo unajua kila mtu hutumia. Kwa mfano wanaume wengi hupenda kuingia kwa inbox za wanawake na kutuma ‘hi’, ‘vp’, ‘hali yako’, ‘mishe vipi’ na kadhalika. Meseji hizi zimetumika sana na mwanamke akiona meseji kama hii basi anaweza kuipuuza meseji yako ama kukuona fala.

Pia wakati unaandika meseji usianze kutumia meseji za kutongoza nk. Kwa mfano hupaswi kumtumia mwanamke meseji kama, ‘nimeona picha yako kwa profile na nimependezwa na mapaja yako nk’. Jaribu kadri uwezavyo kuepuka meseji kama hizi.

Badala yake unaweza kuwa mbunifu na ukaja na meseji nzuri. Mfano unaweza kuingia kwa status yake, soma meseji anazoandika kisha unamuuliza swali kama, ‘Nimeona umeweka picha ukiwa katika ‘......’ nimetamani kuenda hio sehemu. Je ulilipia shilingi ngapi kuwa huko?

Ubunifu wako ndio utaweza kuteka atenshen ya mwanamke haraka sana. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa mtandao wa Facebook]

#2 Jiepushe kutumia emoji ama meme.
Utumizi wa emoji na meme una umuhimu wake, lakini lazima uwe mjanja wakati unapomtumia mwanamke. Pia usisahau kuna emoji ambazo unaweza kuzitumia na nyingine ambazo hupaswi kutumia. Kiufupi ukitaka kuwa salama unapaswa kuepuka na matumizi ya emoji zozote zile.

#3 Fanya utafiti.
Kabla kuwasiliana na mwanamke kupitia DM yake unapaswa kufanya utafiti. Kumjua mtu kupitia mitandao ya kijamii ni rahisi kwa kuwa mambo mengi kumhusu ameyaweka wazi. Ni wewe tu kujituma ili uyasome. [Soma: Sms ambazo zitamnyegeza mwanamke]

So ukiwa unafanya utafiti na ukigundua kuna mambo ambayo mwanamke huyu anapenda kama filamu za vita ama za vitisho unaweza kuingia inbox yake na kumuuliza swali kama, ‘halo nimeona kwa profile umesema unapenda filamu za kutisha, je ushaona filamu ya SAW?’ Maswali kama haya yatasisimua mazungumzo baina yenu.

#4 Tafuta muda mwafaka wa kumtumia meseji.
Time yako ya kumtumia jumbe mwanamke kuna umuhimu mkubwa. Ukituma wakati usiofaa basi anaweza kuipuuza na kuitupilia mbali kama vile afanyavyo kwa wanaume wengine.

Wakati mzuri wa kumtumia mwanamke meseji ni nyakati za asubuhi na jioni. Huu ni ule wakati ambao muda mwingi hayuko busy na anaweza kuiona meseji yako na kuijibu kwa urahisi.

#5 Kuwa mpole kama hakujibu jumbe yako.
Kama umetuma meseji na hujaona reply kutoka kwake baada ya saa moja ama masaa ya kuhesabu, kwa upande wako haupaswi kutuma meseji nyingine. Pengine atakuwa ameona meseji yako na ameipuuza na hataki maongezi yako. Ama labda ameiona meseji yako na yuko busy wakati huo na labda ataamua kukutumia jumbe baadae. Kivyovyote vile unapaswa kuwa na subira. Acha mapepe. Na ukiona hakuna matumaini basi achana naye na ubaatishe kwingine. [Soma: Mbinu za ushawishi kumpata mwanamke]

3 comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.