Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke Katika Mtandao Wa Facebook


Hakuna kitu cha furaha ambacho kinapoteza muda haraka kama kuchat katika mitandao ya kijamii. Nzuri zaidi ni pale wakati unapochat na mwanamke ambaye umeanza kujuana naye kwa mara ya kwanza. Kuchat huku kunakuwa na misisimiko aina yake. Kiufupi hauwezi kuieleza furaha yake.


Uzuri wa kuchat aina hii pia kuna kuja wakati ambapo una tajriba na ujuzi ambao unaweza kuutumia haswa ukiwa unapomtongoza mwanamke kwa njia ya kistaabu katika mitandao hio ya kijamii haswa Facebook.

Wengi hujaribu kutumia mbinu zao zote kuwatongoza wanawake katika Facebook lakini wengi huambatia patupu. Hivyo basi leo Nesi Mapenzi tumekuja na njia ya haraka ambayo unapaswa kuitumia ili uweze kufanikisha azma yako ya kuifaidi mitandao ya kijamii asilimia 100.

Hatua ya 1

Ukianza kuchat na mwanamke usisahau kutumia ile mistari ya kwanza kabisa ambayo wengi hupenda kuiita banta. Ama wengine hupenda kusema ni maneno ya bahati. Kila mtu huwa na mistari yake, lakini kuna ile ya kawaida ya “vipi mrembo hali yako” ama “mambo vipi” nk. Wakati unapoanza kuchat naye usisahau kuweka ile alama ya hisi (!) unapoanza mazungumzo yako. Hii itampa ishara kumwambia kuwa unafurahia uwepo wake online.

Hatua ya 2

Ikija maswala ya kutongoza mwanamke unafaa uwe unaisoma akili yake. Wakati unapochat naye huwa kuna wakati anaandika maandishi ya ucheshi ili ucheke. Hivyo ukiona amekuandikia kitu cha kukufurahisha unafaa umjibu, “wewe unachekesha sana”, ama “hahah” ama “hehehe” inatosha kuashiria kuwa umefurahia. Mbinu hii pia itamfanya mwanamke ajiskie huru na tofauti mbele yako. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa njia ya kirafiki]

Hatua ya 3

Mtongoze mwanamke kwa kutumia emoticon ama emoji. Hizi ni silaha nzito ambazo kila mwanaume anafaa kujihami nazo wakati wowote ule unapochat na mwanamke yeyote. Kwa wale ambao hawazijui emoticon ni zile kama :), :p ama :D. Siku hizi katika kila smartphone umeekewa vitu hivi. Kwa mitandao kama ya Facebook na whatsapp siku hizi zimeboreshwa na kuwekwa kama vibonzo ama visura vya hisia. Hizi kwa kawaida mbele ya mwanamke huzua hisia tofauti tofauti na kawaida huongea maneno zaidi ya kuandika ‘nimekasirika’, ‘nakupenda’ ama ‘nalia’. Jifunze kuzitumia hizi mara kwa mara uone matokeo yake. [Soma: Makosa unayofanya unapomtext mwanamke]

Hatua ya 4

Mwonyeshe kuwa ni spesho. Hapa unakuja na mbinu za kumuonyesha kuwa yeye ni spesho. Mtaftie jina spesheli ambalo utakuwa ukimuita nalo kila wakati mnapochat. Mfano unaweza kumuita ‘mrembo’, ‘beauty’, ‘kiumbe’ nk. Hii ni mbinu muhimu ambayo unahitaji kuitumia kila wakati unapotongoza mwanamke katika mtandao wowote wa kijamii ama Facebook.

Hatua ya 5

Msifie kwa mambo ambayo ni unique kwake na hakuna kwingine ambapo ushaona. Kila mwanamke huwa tofauti. Kile unachohitaji ni kumakinika na lile jambo ambalo linamtofautisha huyu mwanamke halafu unamsifia kutokana na jambo hilo. Ukiona kuwa ni mcheshi, msifu. Ukiona kama ni mwanamke ambae ana bidii, msifu nk.

Hatua ya 6

Jenga interest na maisha yake. Kosa ambalo wengi hulifanya ikija katika maswala ya kutongoza wanawake katika mitandao kama Facebook ni kuwa wanachukulia kuwa wanawake wote wanafanana. Leo akitongoza huyu anadhania kuwa kesho mwingine atakuwa kama wa jana. Tabia hii ndio hufanya wanaume wengi kubaki wapweke wa mitandao. So kuepuka hili, hakikisha unajenga interest kwa mwanamke mfani. Mfano fatilizia maisha yake. Ukiona ni mwanamke ambaye anajaribu kujijenga kisanaa mfano uchoraji basi wewe hakikisha unafuatilia maisha yake ya uchoraji. Msaidie kufanya utafiti, mpe motisha na unampa sapoti kwa kumsifu na kumuuliza maendeleo yake yamefikia wapi. Ukiwa mtu wa aina hii basi utakuwa umejitenga na lile kundi la wanaume wanaoingia inbox yake kila dakika wakitaka kupewa picha zake za uchi. [Soma: Jinsi ya kupata girlfriend chini ya siku 30]

NB! Ikija katika maswala ya kutongoza wanawake katika mitandao ya kijamii lazima uwe mjanja! Usikubali kutoa siri zako hivi hivi sehemu za mitandao ya kijamii. Matapeli ni wengi. Mafanikio kwako!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.