Jinsi Ya Kumfriendzone Mwanamke Bila Kumvunja Moyo


Kujifunza jinsi ya kufriendzone mwanamke ni jambo muhimu kwa kuwa siku moja itatokea ya kuwa unatakiwa kumuweka mwanamke anayekuzimia kando.

Kwa wale ambao wanatatizika maana ya friendzone ni ile hali ambayo unamjeuza mtu ambaye anahisia za kimapenzi kwako na kumweka kuwa rafiki yako tu.


Wanaume wengi kawaida hupatikana katika hali hii ya kuwekwa katika himaya ya urafiki/friend zone. Inatokea pale unampenda mwanamke kupindukia, unashindwa kumueleza kuwa unampenda na badala yake unamfanya kuwa rafiki huku ukiwa na matarajio siku moja ataingiwa na hisia za kukupenda. Well, unajipata umemaliza miaka miwili bila hata kupewa busu badala yake anakuona kama rafiki, na mbaya zaidi anakuchukulia kama mjinga vile. Inaumiza sana!

Hebu tuyaweke hayo kando kwanza tushunghuliki hili swala la leo. Kuna huyu mwanamke umekuwa naye rafiki kwa miaka/miezi mingi. Leo amefunguka na kukupa ishara ya kuwa anakupenda. Lakini kwa bahati mbaya wewe uko na mpenzi ama hujapendezwa na huyu mwanamke. Utafanyaje?

Kama gentleman unafaa uachane na huyu mwanamke, na njia nzuri ya kufanya ni kumuingiza katika hii himaya ya urafiki/friendzone. Wao pia hutufanyia hivyo so leo na wao acha tuwaingize katika ile hali ambayo tunajikuta kwayo.

Hatua za kumfriendzone mwanamke.

#1 Hakikisha kuwa uko tayari kufanya hivyo

Usimfriendzone mwanamke kwa kuwa huna suluhisho lengine la kufanya. Pima hisia zako na huyu mwanamke kwa kuwa pindi utakapomuingiza katika hali ya friendzone basi ujue ni vigumu kumtoa huko.

#2 Pima uzani wa mahusiano yenu.

Wakati unataka kumuingiza mwanamke katika friendzone, jaribu kupima uhusiano wenu na huyu mwanamke. Je mumekuwa marafiki tangu lini? Labda umemjua tangu alipokuwa darasa la sita ama labda ulijuana naye hivi juzi. Hapa utahitajika kutumia mbinu nzuri ya kumtenga bila kuharibu uhusiano wenu ambao umejengwa kwa kipindi kirefu. [Soma: Jinsi ya kupata girlfriend mpya chini ya siku 30]

#3 Tilia maanani ujasiri wao.

Kitu ambacho watu wengi husahau kufikiria wakati wanapofriendzone mtu ni kutotia maanani ujasiri ambao umetumika hadi mtu huyo kueleza hisia zake kwako. Kama mlikuwa marafiki tangu zamani basi haimaanishi kuwa alianza kuhisi mapenzi kwako juzi, itakuwa ilikuwa ni kitambo na amekufungukia tu hivi karibuni.

#4 Usiogope kuongea naye.

Mtu akikwambia kuwa ana hisia na wewe, halafu ghalfa ukatize mawasiliano naye ni vibaya na hatajiskia huru na wewe. So kile ambacho unahitajika kufanya ni kumsikiliza. Mwache aeleze hisia zake kwako. Labda anahisia na wewe tu na wala hataki kuingia katika mahusiano na wewe kamwe. So makinika. [Soma: Kwa nini unapaswa kufanya mapenzi na rafiki yako]

#5 Mpatie faragha yake. 

Wakati amefunguka na kukuambia kuwa anakupenda haina haja ya kuleta hio hoja mbele ya marafiki. Hii italeta aibu. So hakikisha ya kuwa pindi mazungumzo yenu yameisha basi usizungumze kwingine.

#6 Kuwa na subira.

Wakati mwingine tunaweza kuwa tunapenda kitu kwa sababu miili yetu inataka. So inaweza kutokea mwanamke kama huyu amekueleza kuwa anahisia na wewe kutokana na matamanio ya mwili wake na wala si moyo wake. So kuwa na subira, mpe muda wa kufikiria na labda siku moja atajeuza msimamo wake.

#7 Usimwambie kuwa yeye ni kama dadako. 

Kama unataka kumuweka mwanamke katika himaya ya urafiki basi epuka na swala la kumfananisha na dadako. Haifai kabisa. Huwa inaumiza wanawake. [Soma: Njia nzuri za kuongea na mwanamke]

#8 Usimwambie kuwa hutaki kuharibu urafiki wenu.

Ok huyu mwanamke amefunguka kuwa anakupenda. Lakini haupaswi kulinganisha hisia zake kwako na urafiki wenu. Hivyo ni vitu viwili tofauti. Na mwanaume aliye kamili hawezi kutamka maneno kama hayo mbele ya mwanamke.

#9 Usiache mlango wazi.

Hapa lazima uwe jasiri na kuamua iwapo unataka kuanza uhusiano na huyu mwanamke ama hutaki. Usiwe mtu ambaye ni kigeugeu, leo anasema hivi kesho vile. So hapa namaanisha kuwa iwapo unataka kumfriendzone mwanamke basi mwache ajue, na kama unataka uhusiano naye pia mjulishe. Usimwache mwanamke katika njia panda hajui ashike njia ipi.

#10 Mwambie mtoke out tena.

Baada ya kumfriendzone mwanamke, usimwambie kuwa ‘tunaweza kuwa marafiki’ halafu hauwasiliani na yeye tena. La kufanya ni kuwa baada ya kumuingiza katika himaya ya urafiki, basi baada ya siku mbili tatu hivi unapaswa umpigie simu umwambie mtakutana lini mkule bata. Mwonyeshe kuwa bado urafiki wenu uko pale pale na unajihisi huru ukiwa na yeye. [Soma: Jinsi ya kumshawishi mwanamke mtoke mkale bata]

#11 Kuwa mtu anayeelewa hali.

Wengi wetu wanajua ile hali tunakuwa wakati tumeingizwa katika friendzone. Huwa inachosha. So elewa situation ya huyu mwanamke na mchukulie kama vile ambavyo ungependa kuchukuliwa kama ungejikuta katika hali aliyo sasa.

#12 Usimrushie mchanganyiko wa ishara.

Hapa ni mbaya wakati ambapo mwanamke ameeleza hisia zake kwako. Usianze kucheza na hisia zake. Kama unamtaka mwambie na wala si kuanza kumkiss wakati umelewa ama unamkumbatia huku ukijua kuwa hatakataa mwito wako. Hapa lazima uwe kama gentleman. Kuwa mtu ambaye unaeleweka.

Sasa ushajua jinsi ya kumfriendzone mwanamke, so hakikisha unampa heshima ile ambayo anaistahili!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.