Jinsi Ya Kuwashawishi Wanawake Watoke Out Na Wewe


Kabla hujaendelea kusoma chapisho hili, nataka ufahamu ya kwamba kuna njia moja pekee ya uhakika ambayo unaweza kuitumia kuepuka kukataliwa na wanawake katika dunia na miaka ya kisasa, nayo ni kukaa nyumbani na kuepuka kutangamana na wanawake kabisa. Naturally hakuna shangwe kwa hilo, so unapaswa kukubali kuwa kukataliwa kunakuja wakati ambapo utaamua kuapproach mwanamke. Njia nzuri ya kueleza tatizo hili ni kwa kukabiliana nalo mzima mzima. Mwishowe, kadri unavyozidi kufanya mazoezi ndipo utakapozidi kuwa na mafanikio katika kuapproach wanawake na kuwashawishi watoke out na wewe.


Hizi hapa ni mbinu tofauti tofauti ambazo unaweza kuzitumia kuwashawishi wanawake watoke out na wewe na kuepuka kukataliwa na mwanamke kwa namna yeyote ile.

#1 Makinika na timing yako
Hata kama wewe unavutia ama kupendeza mbele ya wanawake kiasi gani, hutoweza kuwa na wakati rahisi wa kumfanya mwanamke avutiwe ama umfanye akubali kutoka out na wewe kama hujua vile timing inavyofanya kazi. So, utawezaje kufanya timing yako iwe bora? Utajuaje kama ni wakati muruwa wa kumuapproach mwanamke kwa mara ya kwanza na kumtongoza? Unaanzishaje gumzo na mwanamke? Well, kwa wale ambao ndio wanaanza kujua maswala ya kudeti, unahitajika kwanza kujua jinsi ya kusoma vile miondoko ya mwanamke hufanya kazi. Baada ya hapo, unaanza kutafuta ishara hakika ambazo zitakwambia kuwa mwanamke fulani yuko tayari kuapproachiwa na kutongozwa. Kama mwanamke hataonyesha dalili ama ishara zozote, basi unaachana naye na kutafuta windo jingine.

#2 Mhusishe katika gumzo la kisawasawa
Kama unataka mwanamke atoke out na wewe, basi unapaswa kumfanya afall in love na wewe kila dakika ambayo utakuwa unaspend na yeye. Kufanya hivi, unapaswa kuanza na lengo katika akili yako kila wakati ambapo utaamua kumuapproach mwanamke. Jiambie mwenyewe kuwa siku hii utamfagia mwanamke kutoka miguuni mwake. Jiambie mwenyewe kuwa unaweza kumfanya huyu mwanamke ajihisi kama wewe ni nusu wa moyo wake. Hii inaweza kuonekana kazi ngumu kwa sasa, lakini si lazima iwe hivi. Unaweza tu kujiweka ama kujifananisha wewe kama  mwanaume asiyejulikana na ambaye amebobea katika maswala ya kutongoza, na hakika kwa wale wanawake ambao watakutana na wewe siku hio watakuchukulia kama wewe ni mwanaume bora ambaye wameweza kukutana naye.

#3 Ipaze tenshen ya mapenzi
Kitu kingine ambacho unapaswa kufanya ni kumfanya mwanamke apandwe na tenshen ya mapenzi kila wakati anapokuona – tenshen ya hali ya juu ambayo itamfanya aitikie kila kitu ambacho utamuamuru kufanya. Kemia ya kimapenzi ambayo inafanya kazi kama mzizi, ambayo unaweza kumfanya mwanamke arushe mbali wasiwasi wake wote ambao anaweza kuwa anauhisi na kumfanya afanye kila kitu ambacho unataka wewe. Pindi utakapofanikiwa kuongeza level yake ya tenshen za kimapenzi, hutapata shida kwa kueneleza ajenda zako vile unavyokusudia wewe.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.