Kwa Nini Hupaswi Kutongoza Kwa Mtandao Wa Facebook


Kulingana na takwimu  ni kuwa mtandao wa Facebook una watumiaji zaidi ya bilioni moja. Hii ni kama asilimia 14 ya watu ulimwengu mzima. Takwimu hizi zinamaanisha ya kuwa katika mtandao wa Facebook kuna wanawake wengi sana ambao unaweza kuamka asubuhi na kuanza kutongoza mchana na usiku mzima.

Mwanzo Facebook inarahisishia kazi yako kwa kuwa inakuletea majina ya wanawake warembo ukiulizwa kama unataka kuunganishwa na wao.

Lakini swali ni je, mtandao wa Facebook kweli unafaa kutumiwa kutongoza wanawake?


Kama uliingiwa na tamaa ya kutongoza mwanamke katika mtandao wa Facebook tunakuambia uachane na mpango huo haraka iwezekanavyo. Kuna mitandao mengine ambayo imewekwa hususan ya kutongozana. [Download: App ya Kiswahili ya Kutongozana]

Hizi hapa ni sababu za wewe kuacha na kutongoza wanawake katika mtandao wa Facebook.

1. Ni bora zaidi kutongoza kwa kuonana
Kutongoza kwa Facebook si njia murua ya kutongoza. Huwezi kutumia mbinu za kupapasa, miondoko ya mwili, uso na hata toni ya sauti yako - mambo ambayo ni muhimu sana ikija na maswala ya kuvutia wanawake. Bila kutumia mbinu hizi mwanamke anaweza kutoelewa ujumbe wako vile unapaswa kuupitisha. Mbinu za mapenzi fioa ama vichocheo vyako vya mapenzi ulivyotumia vinaweza visitambulike. Ama kuonekana kuwa na nia mbaya ama kuonekana na ajenda mbaya.

So badala ya kutegemea Facebook, tongoza wanawake moja kwa moja. Kama hujui ni vipi vya kuanza wewe anza kumshika mwanamke kwa kumpapasa wakati mnapokuwa mkiongea. Anza kwa miguso mepesi kwa kiko chake. Ukiona anaingiliana unaweza kuongeza miguso yako kwa sehemu zake binafsi zaidi. [Soma: Jinsi ya kutongoza kama bingwa]

2. Kupungukiwa na uwezo wa kutongoza kiuso
Sababu moja ambayo hupaswi kutongoza wanawake katika mtandao wa Facebook ni kuwa utapungukiwa na uwezo wa kutongoza mwanamke uso kwa uso. Kama unajijua ya kuwa wakati wote unachat na mwanamke kupitia mtandao wa Facebook basi unaweza kujihisi hutohitaji kumtongoza wakati ambapo mtakuwa pamoja. Haya yatakuwa makosa makubwa, kwa sababu kama tulivyoelezea awali ni kuwa kutongoza uso kwa uso ni muhimu zaidi kuliko kutongoza online.

Kuhakikisha ya kuwa haukosi nafasi yeyote ya kutongoza wanawake ambao wamekuvutia, anza kwa kufuata sheria ya kuapproach wanawake. Wakati ambapo umekutana na mwanamke ambaye unataka kuongea naye ama kumtongoza, mfuate na uanze kuongea naye dakika mbili za kumuona. Usifikirie, wewe mfuate. Jifunze tabia ya kuchukua hatua za haraka kwa mwanamke na utaona ukifanikiwa kwa haraka kuliko kutegemea mtandao wa Facebook. [Soma: Toa uoga wa kuapproach mwanamke]

3. Ujumbe wako unasahaulika mapema
Facebook inaweza kuwa sehemu ngumu ya kujieleza. Kuna jumbe nyingi na mpya ambazo zinahitajika kusomwa, habari za kubofya, na mambo mengine yasiyokuwa na maana ambayo yanaweza kufanya ujumbe wako kupotea katika mazingira haya. Mambo haya yote lengo lake kuu ni kuchukua attention ya mwanamke, kumaanisha ya kuwa itakuwa vigumu zaidi kwa wewe kuweza kujieleza ama kuiteka attention ya mwanamke.

Kama unataka kutongoza mwanamke kwa mtandao, sehemu nzuri zaidi ni kwa mitandao ya kudeti. Huko utapata wanawake ambao wako active wakitafuta kufurahishwa, kupendwa na kutongozwa. Washindani wako hapa watakuwa wanaume pekee - ambao asilimia 90 ya hao wanatuma jumbe za kuboesha aina moja. Kama utasimama na kutuma ujumbe mfupi,  wakuvutia na wenye msisimko wa kimapenzi (sana meseji ambazo zinaonyesha ya kuwa unasoma profile yake) - utakuwa na upeo mpana wa kuweza kuwa na mafanikio ya kutongoza wanawake kwa mitandao ya kijamii.[Soma: Orodha ya mitandao spesheli ya kutongoza]

4. Inaendelea kuzeeka
Ni sawa kusuka wanawake mara moja au nyingine katika Facebook, kama tu lengo lako ni kujinoa makali, lakini itafikia wakati flani utaingiwa na hamu ya kuvuka katika level nyingine. Utahitaji kuchukua namba yake ya simu, ama zaidi kukutana naye. La sivyo  maongezi yako yataanza kuoneka kuzeeka na kukwama kuendelea zaidi.

Wakati mzuri wa kuomba namba yake ni wakati ambao maongezi yenu yanaendelea vizuri - wakati ambapo anajibu meseji zako kwa uharaka. Na jinsi ya kumuomba namba kutalingana na jinsi utakavyomuomba, hapa lazima uonyeshe nia na ulenge moja kwa moja. Mpatie wakati mahususi na sehemu ambayo mtaamua kukutana.

5. Inakupa chapa mbaya
Kutuma meseji nyingi kwa Facebook kunaweza kuwapatia wanawake taswira ya kuwa hauna kitu cha kufanya ila unapoteza muda wako mwingi kwa Facebook. Ok, hio si dhana ambayo unataka kuipitisha kwa mwanamke yeyote. Unataka kumuonyesha ya kuwa wewe una mambo muhimu zaidi ya kufanya katika maisha yako. Unataka kumuonyesha ya kuwa una maisha ambayo unatamani yeye awe nayo.

Njia rahisi ya kuonyesha wanawake katika mtandao wa Facebook ya kuwa una maisha yako ni kuonyesha kuwa maisha yako ni ya furaha. Jipe shughli kwa kufanya shughli zako, tangamana na wengine na kujumuika katika matukio tofauti tofauti. Kufanya hivi kutapandisha hadhi yako na itakuwa rahisi kwa yeye kuweza kupendezwa nawe. [Soma: Jinsi ya kumuonyesha mwanamke una maisha yako]


6. Ni sehemu mbaya ya kutafuta wachumba
Kuna baadhi ya wanaume ambao wanadhani ya kuwa mtandao wa Facebook ni sehemu nzuri ya kupata wanawake wapya. Watajaribu kuwafikia wanawake wapya ama marafiki wa marafiki zao ambao wanafikiria ni warembo na kuanza kuwatongoza. Tatizo ni kuwa wanaume aina hii huharibiwa ama kupewa picha mbaya kuwahusu na marafiki zao, na wanapoteza muda wao mwingi ambao hautawapeleka mahali popote kwa hao wanawake.

Njia bora zaidi ya kukutana na wanawake kupitia kwa marafiki zako ni kuwaalika marafiki zako katika party ama kesha mjini. Unaweza kuambia kila rafiki yako aalike rafiki yake ili ajiunge kwa kikundi, kama njia ya kupanua jamii yako ya kutangamana. Njia hii unaweza kujuana wanawake wapya na warembo zaidi ukilinganishwa na kutuma meseji za kubahatisha kwa wanawake usiowajua katika mtandao wa Facebook.[Soma: Zijua sehemu za kukutana na wanawake]


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.