Jinsi Ya Kuwa Na Deti Ya Kwanza Na Mwanamke Ambayo Itampendeza


Kusema ule ukweli, hakuna kitu kama formula ama mbinu ambayo inaweza kukufanya upate deti ambayo imeshamiri na bora zaidi. Mwanzo ukiplan kutumia ujanja na gemu katika deti yako ya kwanza, unaweza usifike popote katika deti hio. Lakini hii haimaanishi ya kuwa hakuna mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuhakikisha ya kuwa unakuwa na deti muruwa kabisa. Hivyo basi tumekuja na baadhi ya mambo ya kufanya wakati ambapo utatoka deti kwa mara ya kwanza na mwanamke.#1 Kuwa wewe mwenyewe
Inaweza kuwa na ukweli kiasi flani ya kwamba ni lazima uonyeshe mvuto kwa mara ya kwanza unapotoka deti na mwanamke, lakini hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kuingiwa na wasiwasi kutimiza jambo hilo. Mwanzo, kuwa wewe mwenyewe ni njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kumteka mwanamke. Pia hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kujifanya kuwa mtu ambaye hafanani na hulka yake. Kando na hayo yote, kama utaendelea kuiga tabia ambayo haifanani na wewe usiku mzima, utamfanya afall in love na mtu mwingine. Hivyo basi ni bora zaidi uwe wewe mwenyewe, na uendelee kuanzia hapo.

#2 Pumua
Haina haja ya wewe kujistress na deti yako ya kwanza ama kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa. Deti za kwanza kwa kawaida huwa si za kueleza kwa kina, bali ni kupata kujuana wewe na huyo mwanamke. So hata kama kuna jambo ambalo linaweza kufanyika usiku huo, wewe pumua na kuchulia kosa lolote ambalo linaweza kutendeka kama mwanzo wa gumzo lako ama unaweza kufanya mzaha jambo hilo wakati mwingine ambapo utakutana katika deti ya pili. Pia, usisahau kuonyesha confidence na uonyeshe kuwa wewe ni mwanaume alpha.

#3 Chagua sehemu bora
Kama tulivyotangulia kusema awali, deti za kwanza huwa lengo lake kuu huwa ni kujuana zaidi kati yako na huyo mpenzi wako. So, weka simu yako kando usiku huo, msikilize kwa makini mwanamke uliyetoka naye deti na uhakikishe ya kuwa umechagua sehemu ambayo nyote wawili mtaiona bora ili muweze kutangamana vizuri pamoja. Hii inamaanisha kuwa hupaswi kwenda deti ya kwanza na mwanamke katika sinema, concerts ama sehemu za michezo.

#4 Uliza maswali
Amini usiamini, kitu rahisi kama kuonyesha interest ya uhakika kwa mwanamke katika deti kunaweza kumfanya apendezwe na wewe kwa muda mfupi sana. Haijali kama utamuuliza swali tata au lisiloeleweka. Ilimradi tu uendeleze mazungumzo yenu wawili huku ukimsikiliza kwa umakini, utaonyesha idhibati kuwa wewe ni mwanaume anayejali. Njia hii unaweza kumjua zaidi mwanamke aina hii na pia kupata ujuzi wa kuongea na wanawake kwa ujumla, na kuwa na uunganisho wa haraka katika deti zako.

#5 Jienjoy
Hii inaenda sambamba na pointi tulioieleza awali. Wakati mwingi, wanaume wengi huingiwa na wasiwasi na kibaridi wanapotoka deti kwa mara ya kwanza kiasi cha kuwa wanasahau kujiachilia na kuenjoy deti hio ambayo inaendelea. Unapaswa kujua kuwa mwanamke anayetoka deti na wewe hatavutiwa kwako kama hutatabasamu wala kucheka na yeye hata kwa mara moja.Tofauti na kama utamwonyesha mwanamke kuwa unajienjoy na kuburudika na uwepo wake, basi naye pia ataenjoy company yako wakati wote. So, jaribu kufanya mizaha, mchekeshe na mwonyeshe ishara za mapenzi kadri uwezavyo. Usisahau kumwambia kupitia jumbe au simu kuwa ulienjoy kuwa naye katika deti hio.
Upo!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.