Jinsi Ya Kupata Girlfriend Chini Ya Siku 30


Hello reader wa N.M Blog, waonaje kama ungeweza kupata girlfriend chini ya siku 30?

Waonaje chini ya siku 30 kutoka leo uweze kuanza kuitwa mpenzi na mwanamke unayempenda?

Yaani chini ya siku 30 kuanzia leo uwe una mchumba ambaye atakuwa akikupenda, kama vile ambavyo umekuwa ukiota ndotoni mwako.


Well, haya yote yanaweza kutimwizwa kiurahisi sana.

Na kama unadhania hili jambo haliwezekani, basi itakuwa ni sababu haujagundua jinsi ya kutimiza mpango mzima kama huu. Jambo hili lipo, na wachache ambao wana uwezo wa kujiamini, kuwa na mistari na wanaoelewa gemu ya kudeti ndio wanaofaulu.

Kama wewe ni miongoni mwa wale ambao wanashindwa kuelewa itawezekanaje kupata mwanamke wa kukupenda chini ya siku 30 basi usikate tamaa kwani hauko pekeako. Kuna wanaume wengi na wengi ambao hawana mawazo ya jinsi ya kupata girlfriend. Wanachukua miezi, hata miaka wakiwa single na "wakitafuta"

Na wale ambao hupata wachumba (kutoka hili kundi) miongoni mwao ni wale ambao wanaangukia mwanamke ambaye hawakuridhika naye.

So kama wewe umechoka kuwa single kwa muda mrefu ama unaangukia wachumba ambao hawakuridhishi  endelea kusoma chapisho hili. Kwa wale ambao tayari wana wachumba ingieni hapa.

Kupata girlfriend chini ya siku 30 huwa kunahitajika mambo matatu ya kimsingi;

1. Sehemu ifaayo
2. Wakati ufaao
3. Mbinu dhabiti inayohitajika


Mambo haya ni muhimu zaidi kuliko mambo mengine yeyote ambayo ulikuwa unayajua. Hebu tueleze kwa kina.

1. Sehemu ifaayo
Kuna wakati mwigizaji filamu Woody Allen alisema: "Asilimia 90 ya mafanikio ni kuonekena katika sehemu lengwa", Usemi huu ni wa moja kwa moja, lakini ukweli ni kwamba watu wengi wanashindwa kupata kile ambacho wanatafuta kwa kuwa hawajitokezi ili waonekane.

So hivi ndivyo nataka ufanye: pindi utakapomaliza kusoma chapisho hili, nataka ufanye uchunguzi wa kina ujue sehemu ambazo watu ambao ni 'single' hujumuika katika sehemu unayoishi. Hakikisha umetafuta sehemu nyingi ili kwa muda wa siku 30 zitakazokuja utakuwa umezuru sehemu kadhaa.

Hatua ya pili nataka ufanye ni uingie katika simu yako na uwaalike marafiki zako katika sehemu hizi. Najua si kila mtu ataitikia mwito wako, lakini kuna baadhi ambao watakubaliana nawe. Hii ni muhimu kwa kuwa wakati ambapo utakuwa katika sehemu hizi utakuwa ukionyesha ama kudhihirisha kuwa una hadhi ya juu katika jamii. Mfano ukiwaalika marafiki zako katika klabu flani basi wewe pamoja na marafiki zako mtaonekana kama mko na hadhi ya juu katika sehemu hio kwa kuwa mtakuwa mkitangamana na kupiga stori kana kwamba mnamiliki klabu hio...wanipata?

Kama tulivyochapisha katika post moja ya awali, mwanaume ambaye anaonyesha hadhi ya juu katika jamii huwa ana mkono wa mbele ikija maswala ya kuwavutia wanawake.


2. Kuwa na picha dhabiti ya kile unachotaka

Kama asilimia 90 ya mafanikio ni kuonekana katika sehemu lengwa, asilimia 9 kati ya ile 10 ni kujua kile ambacho unataka. Katika dunia ya sasa watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika maisha yao kwa sababu wanashindwa kujua kile ambacho wanataka au kutafuta kwa hivyo wanabakiwa na kuzunguka wakiomba chochote kile ambacho kinaweza kuwastiri.

Lakini kama unataka kupata girlfriend chini ya siku 30, haupaswi kuwa mzembe. Ok, nataka ufanye hivi, baada ya kusoma hili chapisho, kaa chini, chukua kalamu na karatasi na uanze kuandika sifa ambazo unataka girlfriend wako awe nazo. Hii ni kuanzia tabia, umbo lake, sauti, ukomavu kihisia, madoido, sura, nk. Andika sifa yeyote ile ambayo unataka huyo girlfriend wako awe nayo.

Najua huwezi kupata mwanamke ambaye atakuwa na sifa hizi zote chini ya siku 30, lakini kuwa  na msimamo ulio wazi kutadhihirisha kwa mwanamke ambaye utamzukia kuwa wewe una msimamo dhabiti, unajiamini na kuwa una hadhi ya juu.

Pia ukiandika orodha ya sifa ya mwanamke unayetaka utakuwa umetenga aina flani ya wanawake hivyo utabakiwa na wale wanawake wachache unaowataka. Kufanya hivi utakuwa umejitweka jukumu la kuongea na mwanamke aina hii bila kubadilisha misimamo. Wanielewa?

Na mwisho...


3. Fuata kile ambacho unataka

Ok reader wa N.M Blog, hakuna pindi wala hiziri ikija maswala ya kutafuta girlfriend. Kama uko katika sehemu ifaayo, wakati ufaao na unajua kile ambacho unataka, utakuwa umebakiwa tu na jambo moja la kutimiza ambalo linakutenganisha wewe na unachotaka: makamuzi ya hali ya juu.

Makamuzi hapa tunaongea jinsi ambavyo utamuapproach huyo mwanamke ambaye anaonyesha sifa zote unazozitaka. Hapa itategemea mbinu ambayo utaamua kumuapproach. Kama utaanza kwa kuchukua atenshen yake kwa kutumia macho ni sawa, kama utaamua kuenda moja kwa moja hadi pale alipo ni sawa ama kama utaamua kuapproach mkiwa kikundi pia ni bora. (Mbinu hizi zote za kuapproach utazipata hapa)


Kuna mambo matatu muhimu ambayo unapaswa kufanya wakati ambapo unatafuta girlfriend chini ya siku 30. Nayo ni:


  • Approach wanawake wengi kadri unavyoweza
  • Waambie marafiki zako wakutambulishe kwa wanawake wengi iwezekanavyo
  • Agiza deti nyingi (si namba pekee) kadri uwezavyo


Yeah, najua utapata pingamizi nyingi kama vile kukataliwa, kubezwa nk, lakini ukifanya haya yote ukiwa na utaratibu usiofifia utapata baadhi ya wanawake ambao watakubali mwitikio wako na ambao watavutiwa nawe na kutaka kutumia muda mwingi na wewe.

Upo!? Kazi kwako sasa!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.