Jinsi Ya Kuwa 'Classy Man' Utongoze Wanawake


Kwa muda nimekuwa nikiushabikia huu wimbo wa Jidenna wa 'Classic Man' kwa kuwa unavutia kwa sauti na maneno ambayo yanatamkwa katika nyimbo hio. Cha kushangaza ni kuwa wimbo huu umependwa sana na wanaume kuliko wanawake. Ok, kwa kuupitia wimbo hii kijuu juu ni kuwa Jidenna anajaribu kujieleza ya kuwa yeye ni mwanaume 'classy', yani mwanaume ambaye ana taasubi za watu wa zamani kimaisha, wanaume wale ambao waliyatambua na kuyaenzi maisha yao kiusafi, kifasheni, kuwa na taasubi za kiume nk.


So kwa kutumia kigezo cha kuwa 'classy', hapa Nesi Mapenzi tumeamua kuandika chapisho spesheli kuhusiana na kigezo cha mwanaume 'classy' kwa kuwa imeonekana kuwa tabia ya mwanaume aina hii inaenziwa mpaka karne ya sasa.

So unataka kuwavutia wanawake?

Kuna wanaume wengine mpaka sasa hawajasahau wala kutupa tabia hii ya kuwa 'classy'. Mwanzo wanawake huvutiwa automatic na wanaume ambao wana tabia aina hii katika maisha yao. Lakini pia kuwa 'classy' pekee hakutakusaidia kuweza kuvuta na kunasa mwanamke yeyote, lazima uwe na ujiaminifu wa kiwango cha juu. (Machapisho yetu ya awali yanafafanua zaidi).

Hizi hapa ni hatua ambazo zitakusaidia kuwa na tabia za uclassy.

1. Usingojee uthibitisho kutoka kwa wengine
James Bond ni mfano mzuri tunaoweza kuufikiria wa mwanaume ambaye ni classy. Ni jambo gani linalomfanya kuwa hivyo? Hangojei wala kutaka uthibitisho kutoka kwa wengine. Mvuto-ushawishi wake si kuwa anavalia tuxedo za kuzuzua, bali ni kwa sababu ni mwanaume ambaye hahitaji kuambiwa na yeyote yule kuwa yuko SAWA - tayari anajua. Kama kuna watu ambao watakubali na kujiunga naye, ni vizuri. Kama hawataki, hakuna tatizo pia. [Soma: Mbinu ya kufanya ili uweze kujiamini]

2. Valia ipasavyo
Kuna watu wanajidanganya ya kwamba kuwa mwanaume classy lazima uwe umevalia suti ya three piece kila mahali ambapo utaenda. Ok ukweli ni huu...kuwa classy kunaangaliwa zaidi na vile unavalia nguo zinazokufaa zaidi kuliko kuvalia nguo ambazo zitakuanika kama mwana fasheni. Classy ni kuvalia nguo ambazo zina hadhi ya juu kuwaliko wengine lakini pia unavalia kulingana na hulka yako.

Mwisho wa siku ni kuwa wewe mwenyewe ndio utajifahamu iwapo ni wewe halisia ama ni mwigo. Kama unashindwa na kutafuta nguo ambazo zitakuweka classy unaweza kuenda katika duka la nguo karibu na wewe ukajigeze. [Soma: Jinsi ya kubadisha mwonekano wako uvutie]

3. Gonga ndipo
Kwa blog tumekuwa tukiligusia hili swala kwa kina na mfano mzuri tukauweka kwa Leonardo Di Caprio. Jambo ambalo yeye hufanya kwa  kuwasiliana kiujiaminifu na uvuto ni kuwa anaongea moja kwa moja. Hii kwa kawaida ni kuonyesha tabia ya uclassy, kwa sababu unaonyesha uadilifu kwa kitu ambacho unaazimia kutaka ama kufuatilia. Hakuna makosa yeyote kusimama na kumuapproach mwanamke katika klabu ama baa na kumwambia "Nimekuona ukisimama katika ile sehemu na nimetaka kuongea na wewe." Maneno haya najua hayafai kuishia hapa, lakini umemwendea direct na kugonga ndipo kuhusu ajenda yako, jambo ambalo huonekana kuwa classy. [Soma: Jinsi ya kugonga ndipo kama Leonardo]

4. Chukua namba yake kama mwanaume classy
Jambo ambalo linakuwa changamoto kwa wanaume wengi hadi sasa ni kuona wakitatizika kupata namba kutoka kwa mwanamke. Hapa tumekuandikia mbinu ya kuomba namba kiclassy (tofauti na mbinu tulizozipendekeza awali)

i) Mwombe namba yake wakati ambapo maongezi yenu yamefikia kileleni, si ule wakati ambapo uko karibu kumaliza maongezi.

ii) Usiweke lionekane kama swali. Badala yake, unamwambia kuwa unataka namba yake ili uweze kukutana na kuongea naye wakati mwingine.

iii) Weka simu yako tayari kupokea namba yake ya simu.

iv) Mpatie simu yako kwa kuiweka sehemu yake anayoichukulia binafsi.

v) Wakati anapoandika namba yake kwa simu yako, gusia kuhusu maswala ya deti ukilenga gumzo ambalo mumekuwa mkiongea awali.

vi) Mtumie jumbe papo hapo wakati amekurudishia simu yako ili aweze kupata namba yako. Mtumie jumbe nyepesi na ya ucheshi. Mfano "Ni P.p.T, yule mwanaume mwenye tabasamu la kuua. :-D" [Soma: Mbinu ya kumfanya mwanamke alazimike kukupatia namba yake ya simu mwenyewe]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.