Jinsi Ya Kutambua Kama Mwanamke Unayempenda Tayari Ana Boyfriend


Kuna jamaa aliniaproach na kutaka nimsaidie kumtongoza mwanamke ambaye alikuwa anampenda. Kama Nesi Mapenzi, tulimpa silaha na zana zote za kujihami ili kukabiliana na mwanamke huyo. Na baada ya siku nne, huyu jamaa ‘Papito’ alitupigia simu kuwa tayari mchezo kaumaliza. Kitu alichotuambia ni kuwa mwanamke anaonyesha dalili za kumkubali na wanatoka out mara kwa mara. Lakini baada ya wiki mbili, huyu jamaa ‘Papito’ alitupigia simu kwa masikitiko, huyu mwanamke aliyekuwa akituambia wiki mbili zilizopita kuwa amemuwini, sasa ana boyfriend mwingine. Jamaa ‘Papito’ amepoteza wiki mbili nzima akifukuzia mwanamke ambaye hakuwa ni wake.


Hapa Nesi Mapenzi ilikuwa pigo kuu tukizingatia kuwa tulimwongoza jamaa ‘Papito’ na njia na mbinu zote tunazoziamini. Mbaya zaidi ni kwa jamaa ‘Papito’ ambaye alipoteza muda, hisia, fedha, na mistari kwa mwanamke ambaye kumbe si wake.

Ilitokeaje haya yote?

Well. Baada ya kutafakari tuligundua kuwa jamaa ‘Papito’ hakufanya jambo lile muhimu kati ya yote...kujua iwapo anayemfukuzia ana boyfriend au la.

Katika machapisho yetu ya awali tumefundisha jinsi ya kumtongoza mwanamke ambaye ana boyfriend lakini hatukufundisha jinsi ya kujua iwapo mwanamke ana boyfriend au la.

Kabla kuapproach mwanamke lazima ujue iwapo ana boyfriend au la. Na kama hujui itabidi utafute ishara za kujua iwapo ana boyfriend au la. Hii ni muhimu kwa sababu hutapoteza wakati kuaproach mwanamke halafu akukatae baada ya wiki mbili kama vile ambavyo ilimtokea jamaa ‘Papito’.

Kuna wanawake wengine hawawezi kukukataa ukiwaaproach hata kama wako na wapenzi. Watakukubali ili wakudondoe pesa na kukupotezea muda na ile siku utataka tunda watakunyima. Watakwambia kuwa wana boyfriend. Na mbaya zaidi wanakuonyesha machungu kwa kukuita ukutane na wapenzi wao.

Halafu katika kitu kinachotia wasiwasi kuuliza mwanamke ni ‘Una boyfriend/mchumba?’ Wanaume huhepa kuuliza hili swali moja kwa moja kwa sababu wanaingiwa na uoga wa kukataliwa au kufokewa maneno yasiyofaa.

Well. Leo hayo yote yataisha kwa kuwa tumekuandalia mbinu za kumuuliza mwanamke iwapo ana boyfriend bila ya kuonekana fala.

#1 Muulize swali lisilo moja kwa moja. Kumuuliza mwanamke swali fiche kama iwapo ana boyfriend ni muhimu sana. Kama ataona swali limekuja bila lengo flani basi atakwambia ukweli. So unaweza kumuuliza swali kama, “Sasa itakuwaje boyfriend wako akuache mahali kama hapa pekeako?”

Kumuuliza hivi atakujibu kiukweli wala hatohisi unashambulia himaya yake. Bora tu swali kama litokee kama utani na utulivu haitakuwa shida.

#2 Mwambie kuwa “boyfriend” wake bila shaka anampenda. Unaweza kusema neno kama hili ama ukatamka kitu kingine kama hiki. Ukimtajia kuhusu kitu ambacho boyfriend wake anapenda kumhusu, unaweza  kujua iwapo ana mmoja. Anaweza hata kukuambia, “Mimi sina boyfriend”

#3 Mwambie kuwa yeyote anaye kuwa naye amebahatika. Hii kando ya kuwa ni mbinu ya kujua iwapo ana boyfriend, pia ni mstari ambao hufanya kazi vizuri wakati unapotongoza. Hapa una uhakika kuwa utapata majibu mawili, “Sina boyfriend” ama “Ndio, ni kweli amebahatika.”

#4 Muulize kama yuko pekeake. Kama amekaa akiwa pekeake haimaanishi kuwa yuko pekeake. Anaweza kuwa ako na mtu mwingine ambaye ameenda kumchukulia kinywaji ama kujisaidia. Kama utapata nafasi ya kuongea na yeye unaweza kumjulia hali na iwapo yuko hapo na mwenzake. Hii haumuulizi moja kwa moja kama yuko na boyfriend, lakini anaweza kukuambia kama yuko na yeye hapo.

#5 Mwambie kuwa unatumai hujakalia kiti cha boyfriend wake. Wakati umekaa kando yake, tumia huu mstari. Kando na kuwa huu ni mstari mzuri wa kuanza mazungumzo na yeye, pia ni njia moja yakufahamu kama ana boyfriend. Mara nyingi wanawake katika hali hii hujibu, “Sina mmoja” na wala si “Haujakalia”

#6 Mwambie kuwa ungependa kukutana na yeye siku nyingine. Mwambie kuwa ungependa kukutana na yeye siku nyingine iwapo umekuwa na maongezi mazuri na yeye.Mtamkie haya maneno iwapo bado hujajua kama ana boyfriend au la. Hii ni njia nzuri ya kujua kama anakupenda. Kama anatakaa na kusema kuwa ana boyfriend basi ni hivyo.

#7 Muulize kuhusiana na wiki yake.  Kumuuliza mtu kuhusu programu zake za wiki huwa wakati mwingine bila kujua wanaweza kutaja wapenzi wao. Mfano unaweza kumuuliza mwanamke siku ya alhamisi na ijumaa ataispend vipi halafu akujibu, “Alhamisi nitakuwa kazini na ijumaa naspend katika club Savanna na boyfriend wako.” Pia wanaweza kuongea mambo ambayo utajua tu anaashiria yuko na boyfriend.

#8 Mnunulie kinywaji. Ukiwa umeenda klabu halafu ukakutana na huyu mwanamke, mnunulie kinywaji. Mbinu hii inaweza kuwa tricky kidogo. Wanawake wengine wanaweza kukubali uwanunulie kinywaji ilhali wako na boyfriends. So unachotakiwa kufanya ni kumwangalia kwa macho na umwashirie kile unachopania kutaka kutoka kwake. Kama atahisi kuwa unataka kitu kutoka kwake atafunguka na kukuambia. [Soma: Jinsi ya kutongoza kwa macho]

Haya ushajua unachohitaji kufanya. Kazi kwako. Usiwe kama jamaa 'Papito'No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.