Ujanja 15 Wa Kufanya Ili Uvutie Wanawake Ghafla


Kama kungekuwa na mbinu ya moja kwa moja kuwavutia wanawake mambo yangekuwa rahisi sana hapa duniani. Hebu fikiria ungekuwa na uwezo wa kumfanya mwanamke akupende kwa kumfungia jicho pekee ungehisi nini sahizi??


Tulipokuwa wadogo, mambo kama haya ndio tulikuwa tukiamini. Tulidhania kuna miti shamba ambayo ukimgusa nayo mwanamke basi atakuwa anakuandama kila wakati. Lakini kadri tulipokuwa tunaendelea kupambana na kubalehe ndipo tulipozidi kuona kuwa jambo hilo si rahisi. Na leo tumejipata hapa angalau tupate maujanja ya kuweza kuwafutia wanawake angalau watuabie tu neno, "nimekumiss".


Kama umekuwa ukifuatilia blog yetu ya Nesi Mapenzi, kufikia sahizi tumejaribu kuhakikisha ya kuwa tunaweka wazi mbinu zote ambazo unaweza kutumia kutongoza mwanamke. Na kusema kweli ni kuwa hadi sahizi tumewasaidia maelfu ya watu ambao mara kwa mara wanaingia kwa inbox yetu na kutushukuru kwa mambo ambayo tumewaanikia kuhusu maswala ya mapenzi(Pia wewe unaweza kuingia kwa inbox yetu kutushukuru). Mambo ambayo tumeyashughulikia kwa blog hii ni yakiwemo.

  • Jinsi ya kutongoza wanawake
  • Hatua zinazohusiana na mahusiano
  • Jumbe na SMS ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako
  • na maswala mengine mengi.
So tukirudi kwa somo la leo, tumeamua kuja na mbinu ambazo unaweza kuzitumia kumfanya mwanamke avutiwe na wewe kwa haraka sana. 

Zama nasi!

Ujanja wa kutumia ili umvutie mwanamke kirahisi

#1 Tembea wima
Kama unataka mwanamke aweze kukutambua kwa uharaka basi lazima uonekane kirahisi ukiwa uko katika umati wa watu. Wanawake hutambua wanaume wale ambao wanasimama wima, wakikaa chini wanaonekana bado ni warefu. Mbinu hii unaweza kuitimiza kurahisi kama utakiinua kifua chako mbele, tumbo nalo uliingize ndani na utembee kama wewe ni mtu muhimu katika sehemu uliyopo. Hii itakufanya uonekana kaa unajiamini na kwa uhakika utaanza kuvutia watu.

#2 Valia kuridhisha
Mbinu nyingine ambayo unapaswa kuitumia ili uweze kumvutia mwanamke ni kuhakikisha unavalia nguo ambazo zitaridhisha. Hapa unapaswa kuvalia nguo ambazo zinaendana na hulka yako. Si lazima uvalie nguo ambazo hazikuridhishi. [Soma: Siri za kufanya mwanamke akupende]

#3 Oga na unyoe nywele
Mbinu nyingine ambayo mwanamke anaweza kuvutiwa na wewe ni uhakikishe ya kuwa uko nadhifu. Hakikisha unaoga vizuri na pia unapunguza nywele zako ili uonekane msafi kijumla.

#4 Valia rangi nyekundu.
Wakati unavaa nguo, hakikisha ya kuwa unavalia rangi nyekundu. Rangi nyekundu inahusishwa na mafanikio, upendo, na mapenzi. Unaweza kuvalia kofia, tai ama vile unavyotaka wewe.

#5 Kuchua hatua ya kwanza.
Usimuache mwanamke akuangalie kwa matamanio, hivyo wakati umejenga confidence, unaweza kuchukua hatua ya kumuapproach na kumuuliza jina lake ili muanze mazungumzo. [Soma: Hatua za kupata mwanamke]

#6 Kuwa na hisia chanya
Kuweza kufanikiwa kumfanya mwanamke avutiwe na wewe unapaswa kuwa na hisia chanya ndani yako. Watu huvutiwa na mambo ambayo ni ya chanya. Unaweza kufanya hivi mahali popote pale bora tu watu wanapenda kuona ama kuskia mambo ambayo wanayapenda katika maisha.

#7 Sauti yako.
Wanawake hupenda wanaume ambao wanakuwa na sauti nzito. Hivyo lazima ujifundishe jinsi ya kuongea na sauti nzito ili uweze kuiteka atenshen ya mwanamke kiurahisi.

#8 Mchekeshe
Mbinu nyingine ambayo unaweza kuitumia ili kumfanya mwanamke avutiwe na wewe kirahisi hakikisha ya kuwa unakuwa mcheshi. Hakikisha ya kuwa una uwezo wa kuchekesha watu. Hatua hii itamfanya mwanamke aweze kuvitiwa na wewe haraka zaidi.

#9 Usijali
Wanawake hupenda wanaume ambao hawajali. Na mara nyingi huvutiwa na aina hii ya wanaume. Wanaume ambao wanakuwa hatari kimaisha hupendwa sana. Ndio maana wanaume masharobaro hupendwa zaidi kuliko wanaume wa kawaida. [Soma: Zijue sababu kwa nini wanawake hupenda masharobaro]

#10 Jifunze kutabasamu polepole
Badala ya kutabasamu haraka haraka, jaribu kujifunza kutabasamu kwa upole. Hii ni kwa sababu wanawake hupenda wanaume ambao wanachukua muda wao kutabasamu.

#11 Penda watoto wadogo
Kama wewe hupenda watoto wadogo basi ni hatua rahisi kwa mwanamke kukutambua. Ukiwa umemwona mtoto karibu yako kisha ukaanza kucheza naye japo kwa dakika mbili, mwanamke ambaye yuko karibu atapendezwa na wewe kiurahisi sana.

#12 Endesha gari la kifahari
Kama umeitwa katika party ya rafiki yako unaweza kuenda na gari la kifahari katika party hio. Kama hauna unaweza kuomba rafiki yako ama hata unaweza kukodisha. Ili mradi ufike pale watu wakuone wakutofautishe na wengine.

#13 Tangamana na wengine.
Njia nyingine rahisi ya kuweza kuwavutia wanawake ni kuhakikisha ya kuwa unatangamana na wengine. Usijiweke pekeako maana hautaweza kuonekana na wanawake kirahisi. Hivyo kama umeenda kwa sherehe flani, hakikisha ya kuwa unatangamana na wengine. Kama hauna huo ujuzi basi unaweza kualika marafiki zako ili muweze kufanikisha mpango mzima.

#14 Ingia gym
Mbinu nyingine ni kuhakikisha unaujenga mwili wako. Wanawake hupenda wanaume wenye misuli. Hivyo kama una shepu ya mduara itakuhitaji uanze mazoezi ili ujenge shepu yako.

#15 Onekana mtu mkubwa
Watu walio na umri mkubwa kawaida huonyesha ishara ya mafanikio, uthabiti na ulinzi. Hivyo kama mwanamke unayemuapproach atakuona wewe ni mdogo kiumri basi unafaa utumie mbinu akuone kuwa umekomaa. Na mbinu rahisi ya kuonekana kuwa umekomaa kimiaka ni kwa kuvalia suti. Ama tafuta nguo zozote ambazo kulingana na tamaduni zenu zitakufanya uonekane mkubwa kiumri. [Soma: Jinsi ya kutongoza wanawake waliokupita kimiaka]

Upo!

Well, haya ni baadhi ya mambo ambayo unaweza ukayatumia ili uweze kuwavutia wanawake ghafla. Tumia mbinu hizi ama baadhi yazo ili uweze kufanikisha mpango mzima.

Mafanikio kwako.1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.