Jumbe Za Kumtumia Mwanamke Ili Apende Kuchat Na Wewe Mara Kwa Mara


Kumfanya mwanamke akutumie jumbe mara kwa mara kwa kawaida si rahisi. Wakati mwengine unaweza kuwa na mwanamke unayempenda, unachat nay eye kupitia jumbe za SMS ama Whatsapp lakini baada ya muda mwanamke kama huyu anapunguza mwendo wa kukutumia jumbe na mwishowe unashiwa na mbinu za kumfanya awe anajibu meseji zako.

 

Kama umepitia ama unapitia hatua kama hii usiwe na wasiwasi. Jambo hili hukumba kila mtu. Lile unalopaswa kujua ni kuwa wanawake wote wanakuwa na matamanio tofauti tofauti. Unaweza kuchat na mwanamke na mbinu moja ilhali ikafeli kwa mwingine.

 

So utatumia mbinu gani kuhakikisha ya kuwa mwanamke anapenda kuchat na wewe mara kwa mara?

 

Zama nasi.

 


#1 Kwanza tambua ulijuana na yeye kivipi

Hii ni hatua muhimu. Kuna aina mbili za kujuana na mwanamke. Anaweza kuwa ni rafiki yako wa jadi ama anaweza kuwa mlikutana naye kupitia klabu, masomoni, njiani, ufuoni mwa bahari nk. Hivyo lazima utazingatia yale ya kuongea. [Soma: Kwa nini ni muhimu kutongoza wanawake ufuoni mwa bahari]

 

Kama ni rafiki yako basi lazima utakuwa unajua tabia kadha wa kadha kumhusu. Hivyo unaweza kuwa na mambo mengi ya kuzungumza naye. Iwapo ni mwanamke umekutana naye hivi karibuni basi utakuwa na mambo machache ya kumwambia ama kuchat naye.

 

#2 Jumbe sahili hufanya kazi vizuri.

Kama umekutana naye katika sehemu ya faragha haihitaji ufikirie mambo mengi ya kumwambia. Kwa kuwa umekutana naye hivi karibuni, kumtumia jumbe kama, “Leo nimefurahi kukutana na wewe” ama “Natumai umefika nyumbani salama, uko mzima?” ni rahisi kuanzisha mawasiliano kwa upana.

 

#3 Muulize maswali.

Si vibaya kumuuliza maswali mwanamke uliyekutana naye. Lakini kumbuka ya kuwa maswali yasiwe mengi maana humfanyii mahojiano. Maswali kama, “Kipindi unachokipenda zaidi cha runinga ni gani” ama “una maoni gani kuhusu fleva ya strawberry ama vanilla” yanaweza kuzua hoja Zaidi. Si lazima umuulize maswali ya kihulka. Nenda naye polepole hadi pale ambapo utaingiliana vizuri. [Soma: Maswali ya kumuuliza mwanamke akikupatia namba]

 

#4 Umeamkaje/usiku mwema.

Jumbe hizi zina nguvu zaidi kwa mwanamke kwa kuwa zinamfanya kujihisi ya kuwa kuna mtu ambaye anamtakia mema.

 

Jumbe hizi pia ni ishara ya kumwonyesha mwanamke kuwa unamuwaza kila unapoamua na kila mara kabla ya kulala.

 

#5 Meme!

Dunia ya sasa ni ya kiteknolojia. Ndani ya mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp na Insta watu hutumiana meme mara kwa mara. Hivyo usiachwe nyuma. Kuna meme aina aina. Kuna za ucheshi, za kusisimua, za motisha nk.

 

Hivyo si kila wakati lazima umtumie jumbe mwanamke. Unaweza pia kutumia nafasi hii kumchekesha unayempenda kwa kumtumia meme!

 

#6 Usitumie meseji ya “vipi”

Kuna aina za jumbe hufai kumtumia mwanamke. Meseji kama “vipi”, “sasa”,”oi” na kadhalika hufai kutumia kamwe. Hii ni kwa kuwa unaonyesha dalili ya kuwa huna mawazo ya kumwambia mwanamke.

 

#7 Muige.

Hii ndio mbinu nzuri ya kuweza kumfanya mwanamke awe interested na wewe na aweze kujibu meseji zako mara kwa mara.

 

Mbinu hii unaweza kuitumia kuiga jinsi anavyotuma jumbe. Kwa mfano akiwa anapenda kutumia emoji basi pia wewe jibu kwa kutumia emoji. Kama anajibu meseji haraka haraka nawe fanya hivy hivyo, usichelewe. Kama anapenda kutumia mizaha kwa jumbe zake pia wewe tumia mizaha. Mbinu hii itamfanya mwanamke apende kuchat na wewe mara kwa mara. [Soma: Hatua za kufanya ili uweze kumpapasa mwanamke kiurahisi]

 

#8 Mtumie picha.

Usiwe mwoga wa kumtumia picha mwanamke. Kama umeenda sehemu flani basi unapaswa umuonyeshe siku yako ilikuwaje. Bora usizidishe wala usimtumie picha za uchi. Kumtumia picha zako mwanamke mara kwa mara kutamfanya kukujua kwa undani. Kawaida wanawake hawapendi wanaume ambao hawawajui siri zao.

 

#9 Msifie.

Hatua hii ni lazima kama ibada. Wanawake lazima wasifiwe. Mfano akikutumia picha msifie jinsi alivyovalia nk. Hakikisha unamsifia mambo ambayo si kila mwanaume anaweza kusifu. Mfano usimwambie kuwa ni mrembo maana tayari anajua yeye ni mrembo ama ashaambiwa mara nyingi na wanaume kuwa yeye ni mrembo.

 

Upo!

 

#10 Usisahau kuongea kujihusu.

Mfano wakati utakuwa unamuuliza maswali mwanamke, hakikisha ya kuwa hausahau kujieleza. Mfano katika hatua ya #3 ukimuuliza kuhusu kipindi anachokipenda, usisahau kueleza pia wewe kile kipindi ambacho unapenda. Mazungumzo ni kawaida yanahitaji pande mbili hivyo lazima uwe unasalihisha mazungumzo yenu.

 

#11 Mpigie simu.

Unapochat na mwanamke hakikisha ya kuwa haujifichi kwa jumbe pekee. Hakikisha ya kuwa mara kwa mara unampigia simu ili aweze kuskia sauti yako. Kama itawezekana pia unaweza kuvideo call.

 

 

Hizi ndizo hatua muhimu za kufuata kama unataka mwanamke awe interest na wewe. Pia kabla sijamaliza, hakikisha ya kuwa unapokuwa unamtext mwanamke, hakikisha ya kuwa unakuwa na lengo maalum. Usimtumie jumbe mwanamke kama hujui lengo lako. Malengo ni kama vile kumchekesha, kumliwaza, kumtongoza, kumzuzua nk. Ukiwa na lengo kila siku wakati unamtext mwanamke basi utakuwa na urahisi katika maswala ya kutumia mwanamke jumbe. [Soma: Jifunze kutongoza hapa]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.