Jinsi Ya Kujiweka Wakati Unatangamana Na Mwanamke Ili Usishikwe Na Aibu


Kuna huyu mwanamke ambaye unampenda lakini unashindwa la kufanya. Akitokezea mbele yako unashindwa la kumwambia. Na ukijaribu kuongea na yeye unaingiwa na wingu la woga unatamani utoke. Lakini baadaye ukiwa pekeako unaanza kujutia kwa nini hukupiga story nay eye. Unaishiwa ukijilaumu kwa woga ambao umekupata. Unaamua kuwa liwalo na liwe siku utakayo kutana naye lazima uongee naye. Lakini unarudia ule ule woga ambao unakuzunguka na hatua hii inakuzunguka kila mara hadi mwanamke kama huyu anapata mwanaume mwengine huku wewe ukijeuka shemeji.


Well, hili ni jambo ambalo mara nyingi hutokea kwa wanaume wengi. Si wewe pekeako. Ni hatua ambayo baadhi ya wanaume hupitia maishani. Lakini leo nataka mzunguko huo wa woga ambao unakuwa nao mbele ya wanawake uishe. 


Hatua zenyewe za kufuata ni rahisi na chache. Na ukifuata vizuri utaona jinsi ambavyo utafanikiwa kusimama mbele ya mwanamke yeyote yule na kumwambia chochote kile bila woga wowote. Zama nami!


Hatua za kufanya wakati unapokuwa mbele ya mwanamke


#1 Kuwa wewe mwenyewe.

Hili ni jambo muhimu ambalo mwanamke huangalia kwa mwanamke haswa mara za kwanza. Wakati unakutana na mwanamke hupaswi kuiga tabia ambazo si zako. Hii ni sababu mwanamke anaweza kukutambua kwa haraka kuwa unaiga tabia ambazo si zako. Pia wewe mwenyewe ukiwa unaiga tabia ambazo si zako utashindwa kumudu kuendelea na tabia hii na ni rahisi kuingiwa na woga. [Soma: Mbinu ambazo wana wake hutumia kutongoza wanaume]


#2 Usijaribu kuwa mcheshi.

Ok, hapa kama una talanta ya ucheshi ama umejifundisha kuwa mcheshi basi unaweza kuendelea kutumia ucheshi mbele ya mwanamke. Lakini kama huwezi basi usijaribu. Hii ni kwa sababu ukifanya kosa na kutoa mzaha ambao hauchekeshi mwanamke kama huyu anaweza kukuabisha bila ya wewe kutarajia.


#3 Valia nguo ambazo zinakuridhisha.

Kwa kuwa hujazoeana na mwanamke unayeonana naye, ni vizuri kuvalia nguo ambazo umezoea kuvaa tangu awali. Usilazimishe kuvalia nguo ambazo haziambatani na hulka yako. Kama hujazoea kuvaa suti basi usivae maana utajiona uko tofauti na vile ambavyo umejizoea.


#4 Usitumie mistari ile inayojulikana.

Kutumia mistari mara kwa mara hakufai, haswa ile mistari ambayo inajulikana na kila mtu. Wanawake hawapendi wanaume ambao hutumia mistari ambayo inajulikana kuwatongozea. Hizo ni muhimu kuwa unaongea na mwanamke free style. Usiwe na wasiwasi wa kuwa utaishiwa na maneno. Wewe funguka na uongee kile ambacho kitakuja kwa akili yako bila ya kuwa na woga. [Soma: Maneno ya kumwambia mwanamke unapoongea na yeye]


#5 Kuwa huru

Kando na kuwa na hulka ya tabia yako na kuvalia nguo ambazo zinakuridhisha, ni lazima uwe huru unapokuwa na mwanamke. Hakikisha mazingira unayokuwa unaongea na mwanamke umeyazoea. Usikubali kuongea na mwanamke katika mazingira ambayo hujayazoea.


#6 Msifie

Usisahau kumsifia mwanamke. Hili ni jambo ambalo kila mwanamke anapaswa kuambiwa. Kumsifu mwanamke kunakupa nafasi ya wewe kuwa confident ili uweze kuendelea na mazungumzo na yeye bila wasiwasi wowote.


#7 Usiwe na woga

Woga ndio humfanya mwanaume kutoweza kuzungumza na mwanamke. Hivyo ni muhimu kuhakikisha ya kuwa unauondoa woga. Ukifuta hatua ya 1, 3 na ya 4, utapunguza woga wako na itakuwa rahisi kwako kuweza kuwasiliana na mwanamke bila wasiwasi wowote. [Soma: Jinsi ya kutumia mwili kutongoza]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.