Maneno 20 Ya Kumwambia Mwanamke Wakati Unamtongoza


Je unayajua maneno ambayo unapaswa kumwambia mwanamke ukiwa unaongea naye?

Ikija katika maswala ya wanawake, huwa si vigumu kuwaelewa. Wao huwa ni simple na ukitaka atenshen kutoka kwao inakuwa ni jambo la rahisi.


Na wakati kama unataka kuwasiliana nao basi hauhitaji uwe na stadi nzito ya kuzungumza, confidence yako ndio inayohitajika pekee.

Wakati ambao unazungumza na mwanamke, kuna mambo ambayo hupaswi kumwambia mwanamke nayo ni:

#1 Kitu chochote ambacho kinaanza na “si kwa ubaya, lakini...”
#2 Uko kwa siku zako?
#3 Umealia makeup nyingi
#4 Wauko kama wanawake wengine
#5 Unapaswa kula zaidi/kidogo
#6 Ungekuwa bora kama...
#7 Mimi si mfeministi
#8 Wanawake wanapenda kulalamika sana
#9 Ilikuwa mzaha tu, usichukulie serious
#10 Tulia

Kuna maneno mengine mengi ambayo hufai kumwambia mwanamke, hizi tulizoziweka hapa ni mfano tu ambao unaweza kuuangalia. Maneno kama haya mbele ya mwanamke hayavutii na mara nyingi huenda akaudhika na wewe.

Aidha, kuna maneno chanya ambayo unafaa uyatumie wakati ambapo unawasiliana na mwanamke. Matumizi ya maneno haya yatamvutia mwanamke na atataka kuspend time zaidi na wewe.

#1 Uko beautiful. Hapa unamsifia kwa umbo na mwili wake. Wakati unamwambia kuwa ni mrembo usisahau kutaja kitu ambacho kinamfanya kuwa mrembo. [Soma: Jifunze jinsi ya kukutana na wanawake wapya]

#2 Uko smart. Kando na kuwa wanawake wanapenda kuitwa warembo, pia wanapenda kuhusishwa na ujanja. Mwambie kuwa unapenda venye anakuwa na fikra pevu.

#3 Napenda vile unavyokuwa na maoni tofauti. Wanaume wengi huwa hawapendi wanawake ambao wanakuwa na maoni tofauti na yao. Hivyo kumwambia mwanamke maneno kama haya atakutofautisha na wale wanaume wa kawaida na kukupa hadhi ya juu.

#4 Uko sawa. Wanawake pia hukosea wakati wanapofanya maamuzi yao. Lakini kama umeona huyu mwanamke amefanya kitu na umeridhika basi bila shaka hauna budi kumwambia kuwa yuko sawa. [Soma: Vitu vya kufanya ili uweze kujiamini mbele ya wanawake]

#5 Nisamehe. Hii ndio ni vigumu kwa mwanaume kutamka. Lakini neno kama hili litateka atenshen ya mwanamke haraka sana. Kusimama na kukubali kosa ni moja wapo wa kujenga uhusiano mwema, na wanawake wangependa kukuskia ukitamka neno kama hilo.

#6 Sikuwa nimefikiria kimtizamo huu. Hii ni ishara ya kumwonyesha mwanamke kuwa uko huru na wazi kujua zaidi. Wanawake kwa upande wao wanapenda wanaume ambao wako tayari kujifunza zaidi.

#7 Niko hapa kwa ajili yako. Kama hujawahi kutumia maneno haya mbele ya mwanamke basi anza kujifunza cz hujui ni mangapi unayokosa kwa kutamka tu hivi. [Soma: Jinsi ya kumpagawisha mwanamke]

#8 Wakumbuka ule wakati... Mkumbushe kumbukumbu nzuri ambazo zilitokea mlipokuwa wawili. Hii huleta hisia nzuri kwa mwanamke na pia anakuona mtu ambaye hasahau yale mambo madogo madogo mlikuwa mkifanya pamoja.

#9 Nikusaidie vipi? Wanawake hupenda kusaidiwa. Hivyo msaidie kwa njia yeyote ambayo anahitaji.

#10 Napenda venye unavyokuwa mcheshi. Kama vile unapenda mwanamke akuambie kuwa unachekesha vivyo hivyo wanawake wanapenda kuitwa wacheshi.

#11 Ni maamuzi yako. Hapa humaanishi kuwa unafaa umwambie kila wakati achague kile anachotaka kv sehemu ya kutembea ama chakula. Lakini namaanisha kuwa mara moja au nyingine unampa uhuru wa kujifanyia maamuzi. Mfano badala ya kila siku kumchagulia nguo za kuvaa, siku nyingine akikuuliza leo nivae nguo hii ama ile wewe mwambie uko sawa, hata ukiamua kuwa uchi niko fiti. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke acheke]

Orodha ni ndefu ya kumwambia mwanamke. Tukisema tutaorodhesha hapa itachukua mwezi mzima. Baadhi ya maneno mengine ni:

#16 Asante
#17 Nataka ujihisi huru
#18 Unacheka kiutamu
#19 Unanifanya najihisi na furaha
#20 Nakupenda

#21 Si kitu. Wakati mwingine hupaswi kusema chochote. Wewe msikilize kila kitu atakachokuambia huku ukiitikia ama kukataa.

#Upo!

3 comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.