Maswali 10 Ya Kumuuliza Mwanaume Umekutana Naye Mara Ya Kwanza


Katika mazungumzo, si mwanaume pekee anapaswa kuuliza maswali. Mwanamke pia ana nafasi ya kumuuliza maswali mwanaume.

Na kumuuliza maswali kunasaidia sana kwa sababu mwanamke atapata kujua iwapo mwanaume huyu anafaa ama ni fala tu.


Wakati ambapo unamuuliza maswali, kuna maswali ambayo unafaa kuyaepuka kuyauliza kwanza ili usionekane mgumu ama mwenye dharau. Maswali haya ni yale yanahusiana na ex wake ama kumuuliza ushauri wa mahusiano. Badala yake, maswali ambayo unaweza kuuliza kwanza ni kama vile kuuliza kama yuko single na ulitoa namba yangu wapi. Lakini pia usiingie ndani kuuliza maswali haya kwa kuwa utamfanya mwanaume atunge uongo ama aishiwe na maneno.

So, ni maswali gani ya kumuuliza mwanaume unapokutana naye mara ya kwanza?

Zama nasi!

#1 Huwa unafanya nini maishani?
Hili swali ni lazima kumuuliza mwanaume. Pia swali hili limezoeka kiasi cha kuwa limepoteza ladha. Lakini usijali, huu ni mwanzo wa mazungumzo. Kazi ni kazi. Na kama anapenda kazi yake basi atakuwa na hamu ya kueleza kila kitu kuanzia mambo anayopenda na kumchukiza akiwa kazini. Hapa utapata nafasi ya kuchagua iwapo utataka kuendelea na yeye ama ulikuwa unamngojea yule mwanaume anayefanya kazi ya uhandisi.

#2 Ulilelewa wapi?
Hili swali ni la kawaida lakini pia lina umuhimu wake. Je, alilewa mjini ama kijijini. Na kama alilelewa mji mmoja na wewe na wewe ulikuwa unataka mwanaume kutoka sehemu nyingine basi huu ni wakati mzuri wa kuwa na uamuzi mzuri.

#3 Je, wewe na wazazi wako una ukaribu kiasi gani?
Mwanaume ambaye hupenda wazazi wake pia ni rahisi yeye kukutunza na kukupenda. Hivyo mwanaume akisema kuwa haishi na wazazi wake lakini kila wikendi anaenda kuwatembelea basi huyo yuko karibu na wazazi wake. Hili ni swali unapaswa kumuuliza ili uujue msimamo wake. [Soma: Njia wanawake hutumia kutongoza wanaume]

#4 Ni jambo gani zaidi ambalo ushawahi kulifanya ghafla
Well, swali kama hili linaweza kuwa na majibu mengi ya ghafla. Hivyo tarajia mazungumzo kunoga zaidi. Mfano anaweza kusema alienda skuba diving, anaweza kusema kuenda kuwatch gemu England bila kupanga ama anaweza kusema kukutana na wewe leo. Hapa kutakupa nafasi ya kutambua iwapo mnafaana au la.

#5 Kama ungekuwa hauko na mimi sahizi ungekuwa unafanya nini.
Hili ni swali ambalo hupaswi kuliacha. Uliza swali hili kila wakati utakabiliana na mwanaume yeyote. Swali hili lina raha yake sababu hayo majibu utakayoyapokea ni mengi.

#6 Je huwa unafuga mnyama gani wa nyumbani (pet)
Hapa utatambua iwapo huyu mwanaume anajali au la. Kulingana na utafiti unasema ya kuwa mwanaume anayefuga mnyama nyumbani aidha paka ama mbwa ana chemchembe za kujali mtu haswa anapokuwa na uhusiano na mwanamke. [Soma: Sababu mpenzi wako hajibu meseji zako]

Hivyo akisema hafugi chochote si mbaya, lakini mtakuwa mumekosa hadithi nyingine ndefu ya kuzungumzia.

#7 Ni kipindi gani cha utotoni ambacho ungependa kukiangalia hadi leo.
Hii ni mbinu nzuri ya kusisimua hisia za utotoni mwake. Na pindi utakapomuuliza swali kama hili utafungua ukurasa mpya kwa kuwa atajihisi yuko karibu na wewe zaidi hivyo atafunguka zaidi kwa maswali yako. Hapa usijali kama atasema angetamani kuangalia ‘Tom and Jerry’, Tausi, ama WWF. Muhimu ni kuwa anafunguka.

#8 Ni kitu gani unachukia zaidi
Swali hili si baya kuliuliza kwa kuwa kila mtu lazima kuna jambo ambalo huchukizwa nalo. Labda nyote mnachukizwa na mlevi anayelewa chakari halafu anajaribu kuzungumza na wewe na kadhalika. So si vibaya akieleza jambo lolote lile ambalo linamchukiza. Pia utapata nafasi ya kumjua mtu tabia zake. [Soma: Kutambua kama mpenzi wako amekamilika]

#9 Je unaamini kuwa kuna majini na binadamu kutoka nje ya dunia (aliens)
Hii ni mada nzuri ya kuzungumzia na wanaume kawaida hupenda mijadala kama hii.  Ni vitu ambavyo hakuna uhakika vipo ama havipo na mara nyingi watu huwa na dhana tofauti tofauti na wengine hukiri kuwa wamekabiliana navyo. Hadithi kama hizi za kutisha ni nzuri pia utapata kufahamu iwapo mwanaume unayeongea naye ni mwoga au la.

#10 Ni kitu gani ambacho kitanishangaza kuhusu wewe.
Ukikutana na mwanaume mara ya kwanza, kuna yale mambo ya kawaida ambayo unatarajia mfano jina lake, sehemu anayofanya kazi na maswali yote ambayo tumeyaorodhesha hapo ju. Lakini kuna mambo mengine ambayo unaweza kushangaa kuskia ama kujua baadae. So ni muhiimu afunguke na mapema ajieleze kabla kuingia na hisia za kumpenda.


So kufikia sasa naamini maswali uko nayo. Kama awali ulikuwa una maswali ambayo umekuwa ukimuuliza mwanaume kila mnapokutana basi yaongezee ladha kwa kutumia haya tuliyokuandikia. Sisi hapa Nesi Mapenzi tunakutakia kila la heri kufanikisha azma yako.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.