Ishara 13 Kuonyesha Iwapo Boyfriend Wako Anakucheat


Kutambua boyfriend ambaye anakucheat ni haraka sana. Utajua na mabadiliko ambayo atakuwa anaonyesha akiwa na wewe. Mara nyingi kumtambua mwanaume ambaye anacheat ni rahisi hata kuliko kuorodhesha A, B, C..


Kabla tuingie kwa mada, nataka kukueleza ya kuwa hakuna mtu hapa ulimwenguni yuko kamili, aidha kwa mwanaume au kwa mwanamke. Hivyo baada ya kusoma chapisho hili na kugundua kuwa boyfriend wako amekuwa akikucheat muda huu wote, rudi nyuma na uangalie ni jambo gani ambalo limemfanya hadi akaanza kukucheat. Ukishapata jibu, la kufanya ni kufunganya virago na umuage. Haina kaja kuwa na boyfriend ambaye amekucheat kwani hio haitakuwa mara yake ya mwisho kufanya hivyo.

Bila ya kupoteza muda hebu tuzame kwa ishara ambazo utakugundua kuwa boyfriend wako anakucheat.

#1 Muda wote yuko kwa simu.
Wakati anapokuwa na wewe, muda mwingi anautumia kwa simu. Mbeleni hakuwa mtu wa kupenda simu lakini ghafla unamwona tabia yake ameibadilisha na muda mwingi anautumia kwa simu. Hapa bila shaka kuna kitu ambacho kimemvutia sana kwa simu yake.

#2 Anailinda faragha yake sana.
Mara nyingi kila mtu anakuwa na faragha yake ambayo hapendi watu kuiona. Kwa mfano katika simu unaweza kuwa na picha ambazo hutamani kumuonyesha yeyote. Hii inakubalika. Lakini ukimwona boyfriend wako kila wakati simu yake iko mkononi, anaingia nayo chooni hadi bafuni basi jua hapo kuna kitu anakuficha. Na mara nyingi anaogopa labda kuna mwanamke anaweza kupiga simu na ukaishika. ]Soma: Jinsi ya kuwaepuka wanaume unaowachukia]

#3 Anabadilisha mwonekano wake.
Hujamzoea kumwona akijipodoa lakini siku hizi anatumia muda mwingi akiwa bafuni akijiangalia kwa kioo. Ukiona tabia kama hii basi bila shaka boyfriend wako atakuwa anakucheat na mwingine.

#4 Anamakinika sana na mwanamke flani katika mtandao wa kijamii.
Labda mwanamke huyu ndie anakucheat naye. Ukiona mara kwa mara anachat ama kumpigia simu mwanamke huyu, basi uwezekano mkuu ni kuwa anakucheat na huyu mwanamke.

#5 Maisha yenu ya mlalano yamebadilika.
Haya ni yale maisha ya chumbani. Mlikuwa mara kwa mara mnachumbiana chumbani. Maisha yenu yalikuwa ya raha. Hakuna ishara yoyote ambayo ilionyesha kuwa maisha haya yatabadilika. Lakini ghafla unaona mtindo umekuwa tofauti. Na wakati unapojaribu kumhimiza angalau siku moja mcheze mchezo wa chumbani anakataa ama anatoa visababu visivyokuwa na msingi.

#6 Anaspend muda mwingi na marafiki zake.
Ukitaka kujua kama boyfriend wako anakucheat na mwingine angalia wale marafiki ambao anatangamana nao. Mara nyingi mwanaume anayecheat hubadilisha marafiki zake na kutangamana na wengine wapya. Hii ni njia ya kutafuta visababu kuwa anaspend muda mwingi na marafiki zake kumbe ni uongo tu wa kupata muda wa kutembea na mwanamke huyo mpya. [Soma: Ishara za kuonyesha anakuchezea]

#7 Anakuwa na wasiwasi unaposhika simu yake.
Hii ni ishara ya moja kwa moja kuonyesha kuwa anakucheat. Ukiishika simu yake bila ya yeye kutarajia utamwona anaingiwa na wasiwasi akitaka umrudishie simu kwanza. Labda apate nafasi ya kufuta zile meseji za awali alizotumiwa na mwanamke anayecheat naye.

#8 Bado anamiliki account ya mitandao ya kudeti.
Hii ni ishara ya kuwa anakucheat na aina tofauti tofauti ya wanawake so mchunguze vizuri. Ukimwona amejiunga na mitandao kama Tinder ama Badoo basi kuna uwezekano wa kuwa anakucheat kweupe.

#9 Simu yake kuna missed calls kutoka kwa namba zisizoeleweka.
Mara unaona namba imeandikwa ‘fundi wa baiskeli’ ilhali hana, ‘mara mtu wa maji’ nk. Ukiona namba ambazo hazieleweki zinapiga simu mara kwa mara basi kuna uwezekano kuwa anakucheat.

#10 Anakudanganya.
Hii nayo unaweza kuitambua kwa urahisi. Anasema ameenda kumtembelea mjomba wake kijijini mara unapata fununu ameonekana sehemu flani. Hapa atakuwa anakucheat tu.

#11 Anaishiwa na pesa na si mambo yake.
Ukiona mara kwa mara anakwambia kuwa ameishiwa na pesa na hawezi kukusaidia basi kuna uwezekano wa kuwa hizo pesa zinawafaidi wengine. Ok, hapa inaeleweka kama boyfriend wako anastruggle katika maisha ama ameweza kufutwa kazi. Lakini kama umezoea kuwa mara zote anakuwa na pesa na sahizi hana bila kukupa sababu za maana basi unapaswa kuanza kuchunguza pesa zake anazipeleka wapi.

#12 Anakuwa na tabia za ukali.
Ukali huja wakati mapenzi yamepungua. Ukiona kila wakati anakukasirikia kwa visababu vidogo vidogo basi kuna ishara ya kuwa kuna mwingine anamfurahisha na wala si wewe.

#13 Anakusingizia kuwa unamcheat.
Ukimwona boyfriend wako anakusingizia ya kuwa unamcheat basi kuna uwezekano wa yeye kuwa anakucheat. Hii inaitwa saikolojia mjeuko kukufanya wewe kujiona kuwa uko katika makosa ili usiweze kuutambua uovu wake anaoufanya.

Je, hizi ishara tulizoziweka hapa boyfriend wako amekuwa akizifanya? Well, je maoni yako ni yapi? Utafunguka umuulize kama anakucheat ama utamezea tu...maoni ni yako!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.