Maneno Ya Kusema Unapozungumza Na Mwanamke Mara Ya Kwanza


Wengi wa wanaume ambao wanashindwa kutongoza wanawake huwa wote wanakuwa na tabia moja. Tabia yenyewe ni uoga wa kuzungumza.

Ukweli ni kuwa anaweza kumuapproach mwanamke hadi pale alipo. Anaweza kuwa na confidence ya kumfikia na kumsalimia. Lakini ikija katika maswala ya kuongea huwa anatatizika.


Utapata mwanaume amevalia vizuri, amekaa na confidence na kila kitu ambacho unamuaminia kuwa hawezi kushindwa na chochote.

Lakini tatizo ni shida ya kuzungumza. Ninapoandika hivi nakumbuka siku moja nilikuwa katika klabu nikiwa kando na mwanamke mrembo. Halafu baada ya madakika palitokezea jamaa ambaye kimtizamo tu utajua kuwa alikuwa na lengo la kumtongoza.

Katika mazungumzo yake nilishangazwa. Unajua alimwambia nini huyu mwanamke? Nakumbuka alisema hivi:

Mwanaume: Vipi mrembo, naona uko pekeako so nataka nikukeep company.
Mwanamke: Poa.
Mwanaume: Hivi unaitwa nani?
Mwanamke: Naitwa Sheila.
Mwanaume: Sawa.

Baada ya hapo mwanaume huyu alikwamia hapo. Akaagiza kinywaji kutoka kwa mhudumu, halafu akaendelea kumwambia huyu mwanamke, “Nimekununulia kinywaji.” Mwanamke akamjibu, “Asante”

Baada ya dakika mbili hivi za kimya huku nyimbo zikiwa zinaendelea kwa klabu, mwanaume alitoa simu yake na kumwomba namba....

Unajua kitu gani kilitokea baada ya hapo? Mwanamke alisema anachelewa kurudi nyumbani. Na alitoka akamwacha huyu mwanaume akiuma kucha. [Soma: Mbinu nzuri za kumwomba mwanamke namba ya simu bila kukataa]

Nilisikitika. Nilitaka kumjulisha mbinu za kutongoza lakini nikasema acha apambane na hali yake. Labda dunia ilikuwa haitaki akutane na huyu mwanamke.

Well, haya ndio mambo ambayo wanaume wengi hupitia. Na ni jambo la kawaida.

Ijapokuwa hapa Nesi Mapenzi tunajaribu kadri tuwezavyo kuhakikisha kuwa tunawasaidia wanaume na maneno ya kuongea wakati wanapokuwa na wanawake, maneno haya hayatokuwa na umuhimu kama hautakuwa na fomula ya kuyatumia.

Ndio maana leo tumekuja na mwongozo wa kufuata wakati unapokuwa na mazungumzo na mwanamke.

#1 Muulize kumhusu.

Unapozungumza na mwanamke, jenga mazungumzo yako kwa kumuuliza anafanya mambo gani, muulize sehemu anapofanya kazi ama anaposoma. Haya ni maneno ya kimsingi ambayo tayari amezoea kuyaskia. Yaweke maswali yako yawe sahili na pia utumie hisia wakati anapokujibu. Mfano akisema anasoma Makerere unamjibu, “Wow, hapo mahali ni tajika sana!” Kufanya hivi kutamfanya mwanamke huyu kuvutiwa na wewe na atakuwa interested kufunguka zaidi katika mazungumzo yenu. [Soma: Maswali 20 ya kumuuliza mwanamke unapomtongoza]

#2 Jenga uwiano.

Tafuta jambo lolote ambalo litawiana na yeye. Kwa mfano amesema kuwa anapenda kusikiliza nyimbo za rnb. Wewe unafaa ujibu kitu kama hiki. “Waah, sikujua kama nazungumza na mtu ambaye anapenda kusikiliza rnb kama mimi” ama “Niko na nyimbo nyingi za rbn huwa nazisikiliza lakini mimi si shabiki sugu. Lakini kwa kuwa unapenda hizo nyimbo itabidi unipe siri ambayo nafaa kufanya ili niwe kama wewe.”

Mbinu hii italeta uwiano na mazungumzo yenu yatakuwa marefu. Hapa usitie shaka kwa kuwa hutaishiwa na jambo la kumwambia mwanamke huyu wakati wowote.


#3 Jitambulishe.

Kabla kujieleza wewe ni nani, kwanza lazima ujenge uwiano na mwanamke. Baada ya madakika kadhaa katika mazungumzo yenu, unaweza kuchukua hatua ya kujieleza baada ya kuteka interest yake. So hapa unafunguka kulingana na vile mazungumzo yanavyoenda. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akutambue bila hata kuongea naye]


#4 Shukuru uwepo wake.

Mwambie jambo ambalo ni la kirafiki lakini pia la kumsuka. Mwambie hivi, “Nimesikia raha kuwa uko hapa na mimi, nilikuwa nimeanza kuboeka kuzungukwa na watu ambao hawaeleweki hadi ulipokuja.” Hapa utakuwa umepiga ndege wawili na jiwe moja. Kwanza unampa ishara ya kuwa unamsuka na pili unamshukuru.

#5 Zungumza kuhusu sehemu mlipo.

Angalia kitu chochote wakati mnaendelea na mazungumzo yenu na uzungumzie kuhusu kitu chochote. Mfano kama mko katika klabu unaweza kuleta gumzo kuhusu mziki unaochezwa. Kama mko katika mkahawa unaweza kumuuluza kuhusu chakula kizuri anachopenda na kadhalika. Zungumza kuhusu chochote.

#6 Msifie.

Kufikia sahizi utakuwa ushajenga taswira nzuri kwake kukuhusu. So unapaswa uvuke level nyingine. Wanaume wengi hushindwa kuvuka level hii kwa kuwa wanashindwa kutofautisha kati ya maneno ya kiurafiki na maneno ya kimapenzi. Ndio maana utapata wanaume wengi wanatufuata inbox na kusema kuwa wamekuwa na mwanamke kwa zaidi ya miezi sita lakini hawajawakubali.

So hii ndio hatua muhimu zaidi ya yote. Ikifikia wakati flani katika mazungumzo yenu, hupaswi kuendeleza na kumchekesha mwanamke. Unapaswa kutumia maneno ambayo yatamfanya mwanamke ajue kuwa lengo lako si kujenga urafiki na yeye bali ni kumtaka kimapenzi. Upo? [Soma: Jinsi ya kuzungumza na mwanamke ili umvutie]

Mafanikio kwako.

1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.