Mambo 13 Ambayo Humfanya Mwanaume Kuwa Boyfriend Material


Wanaume ni wengi ambao watakuapproach. Wengine ni wazuri umependezwa nao na wengine hujapendezwa wao. Lakini je, utajuaje ni mwanaume yupi anayefaa katika maisha yako? Kuna wanawake wengi ambao wamekabiliwa na mateso ya kuachwa na mwanaume mmoja hadi mwingine kisa ni kuwa hawajui kuchagua. Si kila mwanaume anayekuappoach na kukutongoza unapaswa kumkubali. Kile kinachohitajika kwanza ni kuhakikisha kuwa unamsoma na kuzijua tabia zake kabla hujaamua kumkubali.


Hapa Dakari Mapenzi tumekuja na vigezo vya kuangalia na kuchunguza kabla ya kumchagua mwanaume.
 Zama nasi...

#1 Huwa anapanga mambo na wewe.  Ukimwona mwanaume ambaye anakuhusisha katika maamuzi yake basi fahamu hapo ndipo. Mwanaume ambaye atakuambia na mapema kuhusu mambo anayoyapanga wikendi ya kutoka pamoja basi jua huyu ni mwanaume ambaye anaonyesha dalili za mwanaume bora.

#2 Anakumbuka mambo masuala ambayo uliyazungumza kitambo na kuyaleta katika mazungumzo yenu. Hapa sio siri. Kila mwanamke anapenda mwanaume ambaye anakumbuka mambo ambayo alimwambia ama alimfanyia kitambo. Mfano mwanamke husisimka haswa wakati ambapo mwanaume anamwambia jinsi mara ya kwanza walipokutana na jinsi alivyovalia. Hii ni ishara dhabiti ya kuonyesha mwanaume kama huyu anakudhamini. Ukimwona mwanaume ambaye hakumbuki hata jina lako basi huyo mueke mbali sana.

#3 Haangalii picha zako fb/instagram pekee bali pia ana comment. Kama unazungumza na yeye kwa comments zako bila tatizo basi huyu hata mnaweza kuoana naye hapo hapo :)

#4 Kukutumia na kujibu text zako si tatizo. Ukiona mwanaume anachukua karne nzima kabla kukujibu text yako basi hapo atakuwa labda anawengine anaowaweka umuhimu zaidi kukuliko. Lakini ukimwona anamakinika na wewe katika kila jumbe basi hapo ndipo, usichelewe.

#5 Yuko serious na maisha yake ya mbeleni. Mwanaume ambaye anayapanga maisha yake ya mbeleni ni mwanaume bora kati ya wote. Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa mbeleni hataki kupitia mateso yeyote wakati ambapo atakuwa na kipenzi chake ubavuni mwake. Hivyo wewe unapaswa kuchukua jukumu la kuhakikisha kuwa unayafanikisha maisha yake ya usoni kwa kuwa naye.

#6 Hajali iwapo anaonekana mshamba akiwa anadensi. Utafiti unaonyesha kuwa wanaume ambao hawajui kudensi karibu mara zote huwa ndio wanakuwa boyfriend bora zaidi.

#7 Anampenda mamake na yule mama mboga. Iwapo mtu anawapenda wanawake ambao waliyafanikisha maisha yake na pia wale ambao waliyafanya maisha yake kuwa rahisi, basi pia kwako atakuwa mzuri. Hili ni jambo ambalo limefanyiwa uchunguzi wa  kina.

#8 Anapenda wanyama. Ok ni kusema tu, kuna kitu flani ambacho kinajitokeza wakati unapomwangalia mwanaume mkubwa akimbabaikia paka mdogo ambaye analia. “NI LAZIMA UMDETI MWANAUME AINA HII HARAKA SANA.”

#9 Anakufanya ucheke. Kila mwanaume atafanya juu chini ucheke. Hivyo iwapo unamwona mwanaume anajikakamua ucheke usijilazimishe. Hakikisha kicheko chako kinatoka naturally kwa mambo ambayo yanakufanya ucheke. Anyway, ukimwona  mwanaume anakupendeza na vicheko vyake basi ni ishara ya kuwa ni mbora.

#10 Nyote wawili mnazimia kipindi kimoja cha runinga. Hii ni ishara ya kuwa nyote wawili mko na interest inayofanana, so mkiungana kuwa kitu kimoja pia si vibaya.

#11 Haongea ubaya kuhusu mpenzi wake wa zamani. Mwanaume ambaye anatabia za ujentleman basi haitawahi kutokea hata siku moja ambapo atamtukana ama kumkejeli mpenzi wake wa zamani. Ukiona mwanaume ana tabia kama hii achana naye mara moja coz pia wewe atakufanyia vivyo hivyo.

#12 Anawaheshimu wanawake. Mwanaume anayewaheshimu wanawake bila shaka naye atakuheshimu. Hivyo basi usitupe mbao wala kumkataa mwanaume aina kama hii, ni wachache sana hapa duniani. [Soma: SMS ambazo mwanamke hapaswi kumtumia mwanaume]


Hivi ni baadhi ya mambo ambayo ni dalili ya kuonyesha kuwa mwanaume flani anafaa kuwa boyfriend wako.  Na si lazima aonyeshe ishara hizi zote ndio umwone anakufaa, la. Iwapo ataonyesha baadhi ya ishara hizi basi usingojee mpaka apoteze tamaa kutoka kwako.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.