Jinsi Ya Kufikiria Kama Mwanamke Ili Ufaulu Kutongoza Mwanamke Yeyote.


 Wanaume na wanawake si sawa. Wanaume hufikiria tofauti sana na wanawake. Kwa mfano wanaume mara nyingi hupenda maswala ya siasa, magari, na michezo ilhali wanawake utapata wao hupenda udaku, viatu, na vipindi vya thamthilia. Haya ndio maumbile ya kawaida ya jinsia hizi, na ni muhali kupata aidha jinsia hizi wakienda kinyume na kupenda vitu hivi. Sababu hii ndio hufanya vigumu kwa wanaume kuwaelewa wanawake kirahisi.

So kuna ukweli wa kuwa ukifikiria kama mwanamke unaweza kumuwini msichana yeyote?


Well, huu ni ukweli asilimia mia. Hata mmoja wa paneli yetu ya Nesi Mapenzi anayejulikana kwa jina John huwa hutumia mbinu hii mara kwa mara. Yeye husema ukifikiria kama mwanamke basi utampata mwanamke. Anaendelea kusema wazungu wao wako na usemi unaoambatana na jambo kama hili kwa kusema ‘If you want to catch a thief, think like one’ yaani ukitaka kumshika mwizi, fikiria kama mmoja wao.

Sasa tukija kwa upande wetu, utafikiriaje kama mwanamke?


Wanaume na wanawake wanakuwa na lengo moja la kutimiza kwa akili zao, lakini kuna njia tofauti tofauti za kutimiza malengo hayo.

Ukitaka kumzuzua mwanamke, lazima uanze kufikiria kama mwanamke, na uje na mbinu ambazo zitamfurahisha.

Lazima uhakikishe ya kuwa unajiweka katika nafsi yake, yaani unakuwa yeye. Na pia uwe unajiuliza mwenyewe tabia ambazo angetaka uwe nazo.

Kuna mambo kadhaa ambayo unapaswa kuzingatia wakati ambapo umeamua kufikiria kama mwanamke. Nayo ni kama yafuatayo

#1 Mzungushe

Wanaume hupenda kuongea moja kwa moja wakiwa na hoja ambazo wanataka kupitisha, ilhali kwa wanawake ni tofauti.

Wanawake wanapenda kuwe na drama ama vioja kwa maisha yao. Wanaweza kukosa kukuambia, lakini huu ndio ukweli. Tumia ujanja huu kwa faida yako ili umfanye akupende zaidi na zaidi.

Mbinu hii ni rahisi. Kwanza hupaswi kumwambia kuwa unampenda haraka, na usijisumbue kumuandama kila siku kwa kumpigia simu. Bado hujakuwa boyfriend wake.

Usimwambie mtoke deti na wala usimwambie kuwa unataka kuwa na mahusiano na yeye. Mambo yako yapeleke polepole. Mzungushe kadri iwezekanavyo. Wewe ongea na yeye lakini usisahau kumpatia fununu ya kuwa uko na hamu na yeye. [Soma: Saikolojia ya kumfanya mwanamke akupende]

#2 Wanawake wanapenda atenshen.

Wanaume hawashughuliki kuhusiana na atenshen ama kuwekwa katika gumzo bora tu wapate kile kitu ambacho wanatafuta. Lakini kwa wanawake, wao hupenda atenshen sana.

Mbinu hii unaweza kuitumia vizuri kwa upande wako. Kwa mfano baada ya kutoka deti ama kupata nafasi ya kwanza kuongea na yeye, unapaswa umnunulie maua. Na maua yenyewe usimpelekee nyumbani kwake, la. Unapaswa utafute mtu ampelekea kazini kwake ama sehemu anayosomea. Akipokea maua haya katika sehemu yake ya kazi, atakuwa gumzo la siku. Wenzake watataka kujua zaidi kuhusiana na zawadi uliyompelekea na pia watataka kukujua zaidi kukuhusu. Hii ni njia rahisi ya kumuwini mwanamke huyu kwa kuwa amepata atenshen ambayo anatamani kupata.

#3 Wanawake hupenda kuwafanya marafiki zao kushikwa na wivu.

Kwa wanaume, wao wanaweza kushikwa na wivu kumuona mwanaume mwingine akifanikiwa kimaisha, lakini hawezi shughulika iwapo wamepata nafasi ya kuwa na mwanamke mzuri maishani.

Kwa upande mwingine, wanawake nao hupenda romance na mahaba ya ki Disney. Wanawake wote hupenda kuzuzuliwa, na wote hupenda kupata mwanaume aliyekamilika maishani. Wanaume hawa huwaita Prince Charming.

So hapa utatumia mbinu hii kwa manufaa yako. Ukiwa na mwanamke, hakikisha ya kuwa unakuwa na hulka ya mwanaume aina hii ya Prince Charming. Mtoe deti, kuwa romantic, mnyeshee zawadi, mfungulie milango na kadhalika.

Marafiki zake wakigundua kuwa yeye amepata mwanaume aina hii ya Prince Charming basi watakuwa na wivu. Watatamani wangekuwa wao katika nafasi ile alipo yeye. Pindi huyu mwananamke wako atakapogundua kuwa anawafanya marafiki zake wa kike kushikwa na wivu kwa sababu yako, basi ataongeza penzi lake kwako zaidi. Mbinu hii si ya kubahatisha kwani hufanya kazi asilimia 100. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke ashikwe na wivu]

#4 Wanawake hupenda mahaba.

Kwa wanaume, mahaba si muhimu kwao. Wao bora tu waone kuwa mwanamke anampenda. Lakini kwa mwanamke, hii ni kitu tofauti. Wao kila wakati unapowaonyesha mahaba basi wao huzidi kukupenda zaidi. So hapa la kufanya unapaswa kumuonyesha upendo kila wakati atakapokuwa na wewe. Muonyeshe sapriz mara kwa mara. Mnunulie maua na mambo yote ambayo yatamfanya afurahi.

#5 Wanawake hupenda uhakikisho.

Ni hivi. Wakati mwanaume anapopenda mwanamke, marafiki zake hawawezi kumzuia ama kumwambia iwapo ni mzuri au mbaya. Kwao haina shida bora amuwini mwanamke yule. Hii ni tofauti kwa wanawake.

Wanawake kwao hupenda uhakikisho. Wakati ambapo umeanza kumzuzua mwanamke, lazima itafikia wakati flani atawauliza marafiki zake kuhusiana na wewe. Sasa vile ambavyo atachukua hatua ya mbele italingana na mawazo ya rafiki zake. So hapa kama unataka kumuwini mwanamke huyu kirahisi lazima ujipendekeze kwa marafiki zake.

Kama marafiki zake wamependezwa na wewe, basi atakupenda zaidi. Iwapo marafiki zake watamwambia kuwa amebahatika kupatana na mwanaume bora (ambaye ni wewe) basi utakuwa umefanikiwa bila pingamizi lolote. So hapa la kufanya ni kuhakikisha ya kuwa kila wakati unapokumbana na marafiki zake unakuwa mtulivu, mcheshi na unawasiliana nao vizuri. Pia usisahau kumtunza mwanamke huyu kama malkia wakati mnapokuwa na marafiki zake. Hii ni njia nyingine ya kuwafanya washikwe na wivu zaidi.Well, hizi ndizo mbinu za kufikiria kama mwanamke ili umuwini msichana yeyote. Mbinu hizi ni rahisi. Ukizijaribu mbinu hizi, bila shaka utashangazwa na jinsi utakavyofaulu kwa muda mfupi. [Soma: Jinsi ya kuuteka nyara moyo wa mwanamke]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.