Jinsi Ya Kutambua Kama Mpenzi Wako Anachat Na Mwanaume Mwingine


Hali hii hutokea pande zote mbili, kwa mwanaume na kwa mwanamke. Wakati unapospend time na mpenzi wako inatokea ya kuwa mpenzi wako anakuwa busy akiangalia simu yake mara kwa mara.

 Jambo hili ni la kawaida kwa kuwa siku hizi tunaishi katika maisha ya utandawazi. Kuna mitandao kadha wa kadha ambayo imechipuka ili kuwafanya watu wawe busy. Kuna Tictok, Likee na kadhalika. Pia kuna Instagram na Facebook ambazo tunazifahamu.

Ijapokuwa ni vizuri kupitisha wakati kwa mitandao ya kijamii, mitandao ii hii inaweza kuwa na madhara yake. Na mara nyingi usipomakinika unaweza ukapata mpenzi wako amechukuliwa na mwengine ukiwa unashuhudia. 

So leo tunataka kuleta mada ya jinsi ya kutambua kama mpenzi wako anachat na mwanaume/mwanamke mwingine. Hii itakusaidia kufahamu kile kinachoendelea kati ya mpenzi wako na simu yake ili uweze kuja na maamuzi ya kibusara.

Waswahili husema ukijaribu kuchukua simu ya mpenzi wako uichunguze, unaweza kushikwa na ugonjwa wa moyo. Well, hapa Nesi Mapenzi tutakuongoza tu lakini lile litakalokupata utaamua hatua ambao utakayoichukua wewe. 

So, ni ishara zipi za kuonyesha kama mpenzi wako anachat na mwingine@

 #1 Nishati yake inabadilika ghafla wakati jumbe inapoingia kwa simu yake.

Wakati unapokuwa umekaa na mpenzi wako halafu simu yake iingie meseji, inaona nishati yake inabadilika. Mara nyingi utamwona ameingiwa na wasiwasi ama hata hatojaribu kuangalia simu yake ajibu ujumbe. Anaweza kuichungulia halafu akuangalie iwapo unamuangalia au la.

 #2 Anaficha simu yake usiipate.

Wakati unapokuwa na yeye simu yake ataiweka silent mode ama ataificha kwa mfuko wake ili usiweze kuifikia. Na akipokea jumbe bai anahakikisha ya kuwa anajibu jumbe hio akiwa mbali na wewe.

 #3 Anakuwa na wasiwasi kama hana simu yake.

Hapa labda simu yake ameisahau jikoni na yeye yuko sebuleni. Wakati kama huu utamwona ameingiwa na wasiwasi wa kutaka angalau simu yake iwe mikononi mwake ili aweze kuficha jumbe ambazo zinaweza kuingia kwa simu yake wakati wowote ule. [Soma: Woga unaomkumba mwanaume anapoaproach mwanamke]

 #4 Anaishikilia simu yake.

Hali hii ni pale simu yake inakuwa mikononi mwake wakati wote. Hatotaka yeyote aiguse. Na kama unataka kuangalia picha kwa simu yake atakuwa na wewe muda wote ili usiingie sehemu ambazo ni siri yake. 

#5 Ameweka password mpya.

Labda awali ulikuwa unaijua password ya simu yake. Lakini ghafla umeona ya kuwa amebadilisha password ya simu yake na anatumia nyingine. Ukimwambia akuonyeshe password yake mpya anakupa visababu ambavyo havina mwisho.

 #6 Anacheka tofauti.

Unajua jinsi ambavyo mpenzi wako anacheka. Lakini siku ambayo utaona akipokea jumbe halafu anacheka tofauti na vile ambavyo unajua basi hapo bila shaka kuna kitu ambacho si cha kawaida kinaendelea. Labda amefurahishwa na matamshi matamu kutoka kwa huyo anachat naye. [Soma: Ishara za kuonyesha kuwa imefika wakati wa kumkiss mwanamke]

 #7 Anakuacha chumbani na kwenda kujibu meseji kwengine.

Hii pia ni ishara ambayo inaweza kuashiria ya kuwa mpenzi wako anaona mwingine. Uwepo wako na yeye sehemu mlipo haimpatii uhuru wa kujibu meseji vizuri hivyo anaamua kwenda kwingine kujinafasi.

 #8 Anaanza kukushuku.

Kile ambacho atakuwa anakifanya atadhania pia wewe unafanya vivyo hivyo. Hivyo akiwa yeye anachat na mchepuko pia atashuku pia wewe unafanya hivyo. 

Hali kama hii utanza kuona mpenzi wako anaanza kukushuku, kutokuamini na kuona ya kuwa unamcheat.

#9 Anabadilika.

Hii ni hatua nyingine ambayo hutokea. Utamwona kando na kuonyesha ishara ambazo tumeziorodhesha, mpenzi wako atabadilika kitabia, anabadilisha muonekano wa mavazi n ahata atakuwa anachukia uwepo wako. [Soma: Hatua za kuchukua iwapo mpenzi wako anachat na wanaume wengine

Upo!

Hizi ni baadhi tu za ishara kuonyesha iwapo mpenzi wako anachat na mwingine. Pia usichukulie hatua hizi kwa uharaka ukasema kuwa mpenzi wako anakucheat. Labda inaweza kuwa anachat na marafiki zake tu!No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.