Hatua 9 Za Kuapproach Mwanamke Katika Gym


Kumeet na mwanamke kwa mara ya kwanza si rahisi. Unaweza ukawa umekutana naye kwa mitandao ya kijamii lakini ile siku utakapoamua kukutana na yeye ana kwa ana unaweza kuingiwa na baridi na wasiwasi wa jinsi utakavyochukua hatua ya kuanza kumzoea.

 

Kuaproach mwanamke katika gym nako kuna changamoto zake. Mara nyingi wanawake huingia kwa gym ili kufanya mazoezi na wala si kutafuta wachumba. Hivyo hatua yoyote ambayo utaamua kuichukua inaweza kuwa sawa ama kuweza kukujeukia.

 


Hata hivyo hakuna shida. Wanawake ni wale wale, na kila mwanamke unaweza ukamuaproach bila wasiwasi. Kuna ule msemo ambao unasema mwanaume huwa na asilimia 50 ya kukataliwa na alisilimia 50 ya kukubaliwa iwapo atachukua hatua ya kuaproach mwanamke. Lakini atakuwa na asilimia 100 ya kukataliwa kama hatochukua hatua yeyote ya kuaproach mwanamke.

 

Upo!

 

Leo tumekuja na hatua za kuchukua ili uweze kuaproach mwanamke ambaye atakuwa katika gym.

 

#1 Usimuangalie

Wanawake wakiwa katika gym huwa hawapendi sana kuangaliwa kwa kuwa wako katika hali ambazo hawajazoea. Kwanza wanakuwa wanatokwa na majasho na pili wamevalia nguo chache mwilini. Hivyo kwa mwanamke anajua tayari kila mwanaume lazima atakuwa anamuangalia kwa njia moja au nyingine.

 

Unaweza kumuangalia machoni ili uweke eye contact lakini usianze kumshufu kuangalia mwili wake na kadhalika. [Soma: Jinsi ya kutongoza mwanamke kwa kutumia macho]

 

#2 Mngojee ule wakati yuko huru.

Kama yuko katika hatua ya mazoezi, hupaswi kumtatiza. Hakikisha ya kuwa unangojea hadi ule wakati ambao hana shughuli kama vile anapumzika ama ameenda kunywa maji.

 

Pia usiharakishe kumuaproach. Mfano usizibe njia yake kama anaenda kunywa maji ama kuchukua kitu, badala yake kama unaweza kumletea maji itakuwa bora zaidi kwa kuwa anaweza kuongea na wewe kiurahisi.

 

#3 Soma miondoko yake ya mwili.

Ni vizuri kusoma miondoko ya mwili ya mwanamke kabla ya kuchukua hatua yeyote. Mfano ukiona mwanamke yuko gym halafu anaangalia watu mara kwa mara hii ni ishara ya kuwa mwanamke kama huyu yuko huru kuwasiliana na wengine.

 

#4 Msome.

Well, kama umemuona anaonyesha ishara za kutaka kutangamana na wengine basi unaweza kuchukua hatua ya kumuaproach. Lakini ukimuona hayuko interested na wewe baada ya kumsalimia basi hatua ya kuchukua ni kuachana na yeye. Usilazimishe. Labda siku nyingine atakuwa na nafasi nzuri ya kuongea na wewe.

 

#5 Usitumie mistari/banta.

Kitu ambacho mwanamke hatopenda kuskia kwako ni kutumia mistari. Katika blog yetu hii ya Nesi Mapenzi, tuna kitabu cha MAHATI ambacho kinaorodhesha mistari kadhaa ambayo unaweza kutumia mbele ya mwanamke. Lakini katika hali hii, mistari aina hii haupaswi kutumia kwa kuwa haikai halisia/original. [Download: MAHABATI]

 

Hivyo fanya juu chini kuja na hoja ambazo zitazua mazungumzo. Mfano muonyeshe style mpya ambayo anaweza kuitumia kupunguza nyama za uzembe, kumfanya kuwa na shepu bora na kadhalika.

 

#6 Harakisha.

Lengo kuu kwa mwanamke kuingia katika gym ni kufanya mazoezi. So lengo la kutongoza haliko kwa akili yake. Hivyo hakikisha ya kuwa unafanya haraka ili uweze kuepuka kumkwaza mwanamke huyu. Hivyo ni bora kama utaomba namba yake ya simu na uagize kama atatoka out na wewe siku za mbeleni. [Soma: Mbinu 5 za kuomba namba ya simu kutoka kwa mwanamke]

 

#7 Makinika na mazoezi yako.

Usiwe na pupa au tamaa ya kutimiza azma yako ya kutoka deti na mwanamke huyu. Badala yake ingekuwa bora kama utamakinika na mazoezi yako. Tumia ujuzi wako wote wa mazoezi umridhishe. Labda hata anaweza kuchukua hatua ya kukuaproach wewe.

 

#8 Nukia vizuri.

Kufanya mazoezi kunakuwa na changamoto zake. Ukiwa unatokwa na jasho kwa muda mrefu unaweza kuanza kunuka makwapa na kadhalika. Hivyo ni lazima uwe nadhifu wakati wowote ili uweze kuwa tofauti na wanaume wale wengine.

 

#9 Hujapoteza nafasi kama hukufaulu.

Kumbuka ya kuwa kama amekukataa mara ya kwanza haimaanishi ya kuwa huo ndio mwisho wako. La. Mwanamke huyu lazima atarudi tena kuendelea kufanya mazoezi. Hivyo kuteguka kwa simba haimaanishi ya kuwa ni lazima ale nyasi. Hii itakuwa nafasi nzuri ya kurudi nyuma na kuangalia ni hatua gani ambayo ulichukua na haikufanya kazi kama ulivyokuwa unatarajia. Labda hata unaweza ukapata wingine sehemu tofauti ile. [Soma: Kwa nini ni muhimu kuaproach mwanamke katika ufuo wa bahari]

 No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.