Jinsi Ya Kucomment Kwa Facebook Pic Ya Mwanamke Na Aweze Kukujibu Haraka


Ni mara ngapi ushawahi kutaka kupata atenshen kutoka kwa mwanamke kwa mtandao wa Facebook bila mafanikio?

Wanaume wengi huwa wanawafuatilia wanawake kwa post zao wakiwa na matumaini ya labda siku moja mwanamke kama huyu atawaingilia kwa inbox zao na kuweza kuwasalimia, jambo ambalo si rahisi kufanyika.

Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja kwa mtandao wa Facebook alikuwa amependezwa na mwanamke flani Fb na alikuwa anamvizia kwa kila post zake huku akionyesha matamanio yake ya kuwa anampenda. Kwa muda aliendelea na hio tabia hadi siku moja mwanamke huyu aliweza kumuanika hadharani kwa kutumia screenshots za inbox. Cha kushangaza mwanamke huyu wakati wote hakutambua kama rafiki yangu alikuwa anajaribu kuteka atenshen yake.

Jambo kama hili singependa limtokee mtu yeyote, haswakwa readers wetu wa Nesi Mapenzi. Kuna hatua rahisi za kuweza kuteka atenshen ya mwanamke kwa mtandao wa Facebook ama Instagram kwa urahisi sana bila wewe kuamini.

Mimi binafsi nakumbuka nilitumia ujanja wangu na niliweza kupewa namba na mwanamke mmoja mrembo Facebook bila hata ya mimi kuwa na azma ya kumtongoza. Baada ya kunipa namba nilichat na yeye kidogo kwa Whatsapp halafu nikaachana naye ila hadi wa leo huwa napokea picha zake kwa status updates. [Soma: SMS za kumtumia mwanamke baaada ya kuwa amekupatia namba yake]

Je, wewe ushawahi kumtamani mwanamke Facebook lakini hujui utatumia mbinu gani za kuteka atenshen yake?

Zama nami!

 

#1 Usiwe na pupa!

Wakati mwanamke kama huyu amepost picha yake kwa mtandao wa Facebook, usiwe na tamaa ya kuandika kuwa unampenda, unamtamani ama maneno yeyote makali. Unafaa usiwe na pupa. Nenda polepole. Maneno kama “Umetokelezea”, “Uko smart”, “imeweza” na kadhalika ni poa kuanza nayo.

Mwanzo sikuhizi Facebook wamerahisisha kazi kwa kukupa baadhi ya maneno ambayo unaweza kumtumia mwanamke ili aweze kufurahia.

 

#2 Kuwa rafiki yake.

Kama nilivyotangulia kusema ni kuwa usiwe na pupa. Fikira za kulala naye zitoe kwa akili yako kabisa. Kwanza la kufanya ni kuwa unafaa uwe rafiki yake. Na kuwa rafiki yake inamaana ya kuwa unapaswa kuzungumza maswala ya maana. Labda anaweza kuandika hoja kwa timeline yake hivyo unapaswa kuzua hoja ambayo italeta mazungumzo ya kufaa. [Soma: Jinsi ya kuwavutia wanawake bila ya kutamka neno]

 

#3 Like post zake kwa kutumia emoji za hisia.

Wakati anapokuwa anapost picha, kuna mbinu tofauti za kuchagua vile utakavyolike. Mfano kwa Facebook kuna like za kucheka, upendo, hasira, huzuni na kadhalika. Hivyo lazima uwe mjanja  wa kutumia hisia hizi vile ambayo inahitajika.

Tatizo ambalo wanaume wengi hufanya ni kuonyesha like ya kidole pekee. Hivyo wewe ukiwa unatumia hisia tofauti tofauti mara kwa mara itafikia mahali mwanamke huyu itakuwa rahisi kwake kutambua uwepo wako.

 

#4 Hakikisha akaunti yako iko active.

Ukiwa unataka mwanamke akutambua kwa uharaka basi unahitajika kuwa na akaunti ambayo iko active. Kando na kuwa utaendelea kulike na kucomment kwa akaunti ya mwanamke huyu, lazima na wewe pia unaapdate akaunti yako. Unaweza kupost picha, status, link, ama kushare post za wengine. Hii itampatia mwanamke nafasi ya kutambua mambo ambayo unayapenda.

 

#5 Usiwe kitombi.

Hii ni ile tabia ya kifisi. Haupaswi kuonyesha tabia hii kwa mwanamke haswa kwa mitandao ya kijamii. Mfano ukiona mwanamke amepost picha amevalia bikini ama amelala kwa kitanda usimwambie kuwa unatamani ungekuwa na yeye muda huo, hii ni tabia mbaya na unaweza kupigwa block wakati wowote ule. [Soma: Mambo ya kuonyesha kuwa mwanamke amevutiwa na wewe]

 

#5 Kuwa tofauti.

Mara kwa mara unapaswa kuwa tofauti na wengine. Ukiona wanaume wengine kwa post wanasema ‘Umependeza’, wewe unaweza kujeuza ukasema, hicho kiatu ulichovaa kinaendana na nguo yako. Hii ni nafasi rahisi kwa mwanamke kutambua kuwa uko tofauti na wengine hivyo utateka atenshen yake. [Soma: Kwa nini mwanaume anafaa kuwa na tabia za Alpha]

Pia siku moja unaweza hata kumsaprize mwanamke huyu kwa kumwambia ‘pozi lako limekutoa vibaya’. NB: Mbinu hii lakini hupaswi kuitumia kama ndio mwanzo wako wa kujifunza maswala ya kutongoza. Hii ni mbinu advance ambayo utaitumia kama umesoma machapisho yetu ya awali ya Nesi Mapenzi kwa upana. Mimi nakumbuka nilimwambia mwanamke amekaa vibaya baada ya kuona wanaume wengi wakimsifia na hapo hapo alinifuata inbox na haikuchukua muda mrefu akanipa namba yake. 

 

#6 Usijieleze sana.

Si lazima uonyeshe upendo wako kwa mwanamke huyu kwa kutumia maneno mengi yasiyokuwa na mwisho. Mara nyingine zile jumbe fupi fupi zinaweza kupitisha ujumbe mzito. Kwa mfano unaweza kutumia emoji ama meme kwa post zake ili uweze kupitisha ujumbe wako kwa urahisi.

 

#7 Jenga connection.

Njia rahisi ya kuweza kuteka atenshen ya mwanamke ni kufuatilia posts zake na kutumia post hizo kujenga uwiano. Kwa mfano unaona anapost picha za paka wake ama na aina ya nguo anazopenda basi unaweza kuleta hoja na vitu hivyo. Hii itakuwa rahisi kwako kuteka atenshen yake.

 

#8 Usiache kumfuatilia.

Usipunguzo mwendo wako. Hakikisha ya kuwa unafuatilia mambo ya mwanamke huyu kwa timeline yake mara kwa mara. Lakini pia zingatia mipaka ili usiweze kuonekana kama fala.

 

#9 Chukua hatua.

Ukiona ya kuwa umeweza kuiteka atenshen ya mwanamke huyu, sasa unaweza kuchukua hatua ya kumtumia jumbe kwa inbox yake. Mtumie jumbe halafu mpatia masaa kadhaa uangalie kama atakujibu.

Ukiona hajareply, unapaswa uingie kwa post yake mpya halafu mwambie umemtumia jumbe kwa inbox yake. Hii ni muhimu kwa kuwa wanawake hutumiwa mamia ya inbox na huwa hawazisomi. Hivyo unafaa umwambie kuwa umemtumia jumbe ili aweze kuisoma.

 

#10 Chukua namba.

Hii ndio hatua muhimu ya mwisho unayopaswa kuwa makini nayo. Ukiona amejibu jumbe yako, basi kuna nafasi kubwa kwake kuweza kuendelea mazungumzo na wewe. Hivyo hatua muhimu ni kuchukua namba yake ya simu ili uweze kuendeleza mazungumzo yenu faraghani. Labda siku moja atakubali utoke na yeye deti. [Soma: Jinsi ya kupata mwanamke kirahisi]

 

Ok. Hizi ni mbinu ambazo unapaswa kufuata ili uweze kuiteka atenshen ya mwanamke kwa mitandao ya kijamii haswa Facebook. Hatua hii haihitaji pupa, ni hatua ambayo kwa kawaida unafuata polepopole.

Ukitumia mbinu hii utajitofautisha na wanaume wengine ambao wanateseka na kuanikwa kila siku kwa mitandao hii ya kijamii. Upo!No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.