Jinsi Ya Kudeal Na Mpenzi Wako Ambaye Anatext Mwanaume Mwingine


Hali hii kutokea mara kwa mara kwa wale ambao wamejikuta katika relationship na mwanamke. Najua ishawahi kutokea pale ambapo mpenzi wako unamwona anatext na mwanaume mwingine.


Wakati mwingine hali kama hii huweza hata kujitokeza akiwa mbele yako. Unapata mpenzi wako bila wasiwasi anacheka huku akiendelea kuchat.

Makosa ambayo hutokea ni pale ambapo mwanaume naye anaanza kuingiwa na wivu kiasi cha kuwa anaanza kumgombeza mpenzi wake na kutaka kujua ni nani anaongea naye na mahusiano ya hao wawili yamekuja vipi.

Well, hapa blog ya NESIMAPENZI.com kama kawaida yetu tumekuja na mbinu thabiti ambayo unapaswa huichukua ili kutatua swala zima. Ni vizuri kuwa wazi na mpenzi wako ili kuweza kuyafanya mahusiano yenu yawe mazuri na marefu.

#1 Uhusiano wako na huyu mpenzi wako ni upi?

Kabla hujaaza kuchukua hatua yeyote lazima kwanza ujue uhusiano wako na huyu mwanamke. Wanaume wengine wanaweza kuchukulia swala hili zito na kumbe hata uhusiano wako na huyu mwanamke si wa kufaana. Labda umekuwa ukimdeti huyu mwanamke kujikeep busy tu na wala huna harakati zozote za maisha ya usoni. So iwapo huna interest na huyu mwanamke na hutaki kuwa na mahusiano marefu, basi haina haja kusumbuana. Mwache aendelee kutext yule ambaye anataka.

#2 Ushakutana na huyu mwanaume awali?

Hebu tuchukulie kuwa uko katika relationship ya nguvu na mpenzi wako. Kufikia hapa najua ushakutana na baadhi ya marafiki zake, na labda huyu ambaye anatext naye.

Swali la kujiuliza hapa ni je huyu mwanaume ushakutana naye ama ametokezea ghafla katika maisha yake bila sababu yeyote. Kama ushakutana naye mara kwa mara basi bila shaka umemsoma. Na kama kuna chembechembe za kuwa wana zaidi ya urafiki pia utakuwa ushajua. [Soma: Jinsi ya kumjeuza rafiki yako awe mpenzi wako]

#3 Usipandwe na hisia.

Unamwona mpenzi wako akimtext huyu mwanaume mara kwa mara na haujapendezwa. Lakini pia wakati ambapo unamwona anachat naye usionyeshe hisia zako. Kama umekasirishwa usimwonyeshe. La kufanya ni kuwa unaweza kumuuliza huyo ni nani anaongea naye na umsikilize kila kitu ambacho atakuambia.

#4 Usirukie majibu.

Akikueleza kila kitu kuhusiana na huyu mwanaume hupaswi kurukia kumwambia kuwa anakucheat ama anakuendea kinyume. Hili ni kosa kuu ambalo mwanaume aliyekamilika hapaswi kufanya kamwe.

#5 Kusanya uhakikisho.

Wakati umeona kuwa mpenzi wako anachat na mwanaume mwingine, lazima ufanye utafiti umsome kila reaction ambayo anakuwa nayo. Je, tabia yake imebadilika? Je, siku hizi hapendi kuspend time na wewe, ama je anaficha simu yake ama amebadilisha password? Haya ndio maswali lazima uthibitishe kabla kurukia hatua yeyote ile.

#6 Tambua kati ya rafiki na zaidi ya rafiki.

Kila mtu anakuwa na rafiki yake wa jinsia ile nyingine. Na huwa tunajua kutofautisha kati ya rafiki na ‘zaidi ya rafiki’. Ni rahisi kugundua kemia ya kimapenzi wakati ambapo watakuwa wanaongea pamoja ama wakirushiana texts. Jambo hili haliwezi kufichika. [Soma: Hatua za kujua kama mpenzi wako anakucheat]

#7 Usimwonyeshe wivu mbele yake.

Ukimwona anaendelea kutext na mwanaume huyu, lile na kuepuka ni kutomuonyesha wivu. Hakikisha huonyeshi kuwa unaona wivu. Wanawake wengi hawapendi tabia za mwanaume mwenye wivu. Unaweza kuachwa haraka ukiwa na tabia kama hii.

#8 Baada ya kuongea naye, soma reaction zake.

Mwelezee kuwa hupendi tabia yake ya kutext na wanaume hivi hivi kwa kuwa mwishowe inaweza kuleta matatizo katika relationship yenu. Ikiwa huyu ni mwanamke msikivu, basi ataitikia mwito wako na anafaa kupunguza kuchat na huyu mwanaume.

Iwapo unaona anakupuuza, basi lazima kuna matatizo kati yenu wawili. Hali kama hii atakuwa anakuonyesha ishara ya kuwa wewe hauna thamani ya zaidi kumliko huyu anayechat naye.

#9 Kutana naye.

Ok, kama umegundua kuwa anakucheat na huyu mwanaume basi haina haja ya kukutana naye. Lakini kama ni rafiki yake tu mbona usimeet na yeye umjue zaidi? Kukutana naye kutakupa fursa ya kujua hadhi ya urafiki wa wawili hawa.

#10 Unahitaji kubadilika.

Kama huyu mwanaume ni rafiki yake wa kweli basi ujue hataenda popote. Na usitarajie mabadiliko yeyote. So la kufanya hapa nikujikubali na kufanya juhudi za kuondoa woga na wasiwasi kuhusiana na huyu mwanaume. Kumbuka ya kuwa si kila mwanaume atakaye kuwa naye inamaanisha kuwa analala naye ama anamtamani kihisia. [Soma: Sababu ambazo hufanya wanawake wakatae wanaume]

#11 Usimwambie akatize mawasiliano.

Iwapo ni marafiki wa kawaida na huyu mwanaume basi haina haja ya kumwambia akatize mawasiliano. Ni marafiki tu na hakuna la ziada. Lakini kama unaona kuwa anakuwa interested zaidi na huyu mwanaume kukuliko basi unapaswa umwambie mambo mawili. Aidha akubali kukatiza mawasiliano na huyu mwanaume ama ukatize mahusiano na yeye. Lazima achague moja.

Mwisho ni kuwa lazima ufahamu kwamba kuwa katika mahusiano si rahisi. Wengi hujipata wamependa sehemu ambayo haiwafai na wengine bado wanasumbuka kupata angalau mwanamke mmoja amuite mpenzi. So ukiwa katika mahusiano na mwanamke hakikisha kuwa unalinda mapenzi yenu.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.