Hatua Za Kumjeuza Rafiki Yako Kuwa Mpenzi Wako


Kuna baadhi ya wanaume ambao wanajiskia kuwa na furaha wakiwa na marafiki zao wa kike ambao wanawapenda kisiri, lakini kama umechoshwa na kuboeka kuwa rafiki pekee na mwanamke unayempenda, basi huu ndio wakati mzuri wa kujeuza gemu yako kabisa. Barabara ya kumbadilisha rafiki yako hadi kuwa girlfriend wako inaweza kuwa ndefu, lakini mwishowe huwa na utamu wake. Halafu kama wewe ni mwoga, mpweke, ama bikra ambaye hajui lolote kuhusu jinsi ya kuwatongoza wanawake, basi usitie shaka. Huwa ni rahisi kutimiza hili. Na utaweza kujenga confidence yako na kujeuka mwanaume ambaye anaweza kujumuika na kutangamana na wengine kirahisi. Hii hapa ni njia nzuri zaidi za kukuwezesha kumvutia mwanamke wa ndoto yako na finally ajeuke zaidi ya rafiki yako. Hivi ndivyo unavyopaswa kufanya.


#1 Acha tabia ya kuwa Mr. Mzuri
Ijapokuwa ni vizuri kuwa mwanaume mzuri mara moja au nyingine, kuwa mzuri sana kiasi cha kuwa unaonekana kama unajipendekeza kwa mwanamke hakufai. Mwanzo ukiendelea kumuonyesha uzuri wako kila wakati utabakia kuwa rafiki yake milele. Kama hujawahi kugundua hili, wanawake wengi huwa wanapendezwa zaidi na wanaume ambao ni masharobaro ama ‘bad boys’. Hii ni kwa sababu masharobaro huwa wanaonyesha hulka ya kutojali ama kuwa na hulka ambazo huonyesha ubaya wao mara moja au nyingine – hii huwavutia wanawake sana. Wanawake hupenda wanaume ambao wanaonyesha confidence  – kitu ambacho mwanaume alpha huwa anamiliki. Well, wanaume ambao wanatawala na ambao wanaonyesha kucontrol katika kila hali huwa kikawaida wanakuwa na confidence wakati wote. So, kama utaanza kuiga na kuonekana kama mwanaume sharobaro, unaweza kujeuka na kuonekana na mvuto na nishati zaidi ambayo itakuweka juu katika mashindano kwa muda mfupi sana.

#2 Usimuandame kama kelbu
Kama unapenda kumfuata fuata mwanamke kama kelbu, basi ataudhika na wewe na mwishowe atakuacha katikati. Mbaya zaidi anaweza kuambia marafiki zake kuwa wewe ni fala usiyekuwa na kazi ya kufanya. Ama anaweza kukatiza urafiki wenu. So, njia nzuri ya kufanya kwa sasa ni kurelax na utulize gemu. Kwa njia nyingine ni kuwa, usimkimbize kufanya jambo lolote. Ukitaka kumfanya mwanamke awe interested na wewe  kiharaka ni kwa kuhakikisha ya kuwa unakuwa mtu asiyeeleweka, yaani leo uko na yeye, kesho uko busy hupatikani. Huku kutamfanya akumisi na kutaka kuspend muda wake mwingi na wewe.

#3 Usikubaliane na kila kitu
Kama utaendelea kufanya kila kitu ambacho mwanamke anakuambia ama kukubaliana na kila kitu anachotaka, basi ataanza kukuchukulia advantage kwa sababu atagundua kuwa amekuweka katika viganja vyake. Jithamini wewe mwenyewe zaidi kuanzia sasa na umuonyeshe kuwa haubabaikii ama kuomba atenshen kutoka kwake. Hii itamfanya kuanza kujishuku na itamfanya kutaka kujua kwa nini umekuwa tofauti. Baadaye, ataanza kukukimbilia ili abadilike.

#4 Isome na uielewe sanaa ya kutongoza
Katika dunia ya kudeti na kutongoza, hakuna kitu kinachofanya kazi vizuri zaidi kama kushawishi. Mwanzo, hakuna kitu ambacho kitatokea kati yako na rafiki yako kama hujui kushawishi. So, nenda ujifunze jinsi ya kutumia macho yako kumtongoza rafiki yako, mpe tabasamu, mfinyie jicho, na mhusishe katika gumzo ambalo litampa hamu ya kukukaribia. Fanya haya yote na utaona utofauti wa rafiki yako akianza kufall na wewe pole pole. Utajipata rafiki yako amejeuka kuwa mpenzi wako.

1 comment:

  1. Ni rafiki yangu pia n rafiki ya girlfriend yangu

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.