Jinsi Ya Kumwambia Mwanamke Awe Girlfriend Wako Na Afurahi


Je umekuwa ukikutana na huyu mwanamke kwa muda sasa? Leo tutakufundisha jinsi ya kumwambia kuwa unataka kumfanya girl wako na afurahi.

Kufukizia mwanamke ni raha haswa pale ambapo mnakuwa mnafichiana hisia zenu.

Baada ya kutoka deti kadhaa pamoja kwa muda mrefu, kuna kile kitu ambacho kinakukujia kutaka kumwambia mwanamke kuwa unataka awe girlfriend wako.


Ok, kwa baadhi ya wanaume wengine kumwambia mwanamke kuwa wanataka wawe girlfriend zao si rahisi. Inawaweza kuwachukua muda mrefu hadi watamke neno hilo.

Leo tutakupa mbinu rahisi za kuchukua hadi umwambie mwanamke ajeuke girlfriend wako, Zama nasi.

Hatua za kumwambia mwanamke awe girlfriend wako

#1 Usiharakishe.

Umekuwa ukikutana na huyu mwanamke kwa muda sasa. Labda wiki ama miezi kadhaa mumetoka deti pamoja. Kitu unapaswa kujua ni kuwa mapenzi si mchezo. Hayafai kuharakishwa. Mwanzo fikiria iwapo uko tayari kuwa na huyu mwanamke ama unabahatisha tu. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke Facebook]

#2 Usimpigie magoti.

Usipitishe kile kiwango cha kumpigia magoti mwanamke. Hapa haumvishi pete bali unamwambia unataka awe girlfriend wako tu. Ule wakati ambao utapanga kumpigia magoti mwanamke labda iwe ule wakati ambao unampa posa.

#3 Hakikisha kuwa inakuwa katika kumbukumbu.

Wakati ambapo utataka kumtamkia hayo maneno kuwa unataka awe girlfriend wako basi hakikisha inakuwa sehemu ama wakati ambao hatosahau. Unaweza kumpeleka sehemu romantic ama unaweza kuja na mbinu ambayo itamfurahisha.

#4 Mpatie zawadi ya kitu hata kama ni kidogo.

Wakati mwingine kumpatia mwanamke zile zawadi ndogo ndogo zinakuwa na umuhimu sana. Pia usijisumbue kumnunulia zawadi ghali huyu mwanamke kwa kuwa bado hajakuwa mpenzi wako. [Soma: Hatua muhimu za kupata girlfriend mpya]

#5 Tumia kadi za salamu/mwandikie barua

Ijapokuwa kadi za salamu na barua wengi wanaamini zimepitwa na wakati, mbinu hizi hufanya kazi vizuri. Tafuta kadi za mapenzi halafu ongeza maneno yako kidogo na umpelekee huyu mwanamke. Unapaswa umpatie kadi hii wakati uko hapo halafu umruhusu aisome ukiwa kando yake ili usome hisia zake vile zitakuwa.

#6 Zungumza na yeye.

Wakati umemwandikia barua ya kimapenzi ama kadi ya salamu, hakikisha ya kuwa unazungumza na yeye. Maneno ambayo umemwambia kupitia kwa barua ama kadi hayatoshi. Lazima umwambie jinsi unavyohisi wakati mko pamoja. [Soma: Sababu zinazokufanya usiwe na girlfriend]


#7 Usimuulize kitu

Mwambie hisia zako halafu ngojea jibu lake. Kama atashindwa kukujibu wakati umemuelezea hisia zako, usimlazimishe akambie kitu. Wakati mwingine anahitaji muda kupata kueleza hisia zake kwako. Jibu lake litakuja wakati ambapo yuko tayari.


#8 Mwambie yale maneno manne.

Kufikia sahizi umemwelezea hisia zako kupitia njia ya kadi na barua. Umezungumza naye na umemwambia hisia zako kwake. Sasa ni kumtamkia yale maneno manne. Ni muhimu kuhakikisha kuwa unamwambia mwanamke hisia zako ili apate kukuelewa. Usimwache mwanamke katikati asielewe fikra zako akilini mwako. Lazma ufunguke na umwambie ukweli. Nenda moja kwa moja na umwambie, “Mamino ‘nataka uwe girlfriend wangu’” [Soma: Kwa nini kila mwanaume anafaa kuwa na tabia za alpha]

Pindi utakapofuata approach ya hatua hizi nane ambazo tumeziorodhesha za kumwambia mwanamke kuwa unataka kuwa girlfriend wake, basi hawezi kukataa mwito wako. Ujanja ni kuhakikisha kuwa unachukua time hadi ufikie hatua ya mwisho ya kufunguka.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.