Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Atabasamu Na Apende Kuwa Na Wewe Wakati WoteKama tunataka kutongoza mwanamke, kuwafurahisha ama wajiskie huru mbele zetu huwa tunatumia mbinu ya kuwafanya watabasamu. Kutabasamu ni njia moja wapo ya kuondoa misongo ya mawazo, uchovu, na hata kuondoa uzee. Ndio maana wazungu walikuja na ule msemo wa laughter is the best medicine.


Kabla hatujaingia katika swala la jinsi ya kumfanya mwanamke atabasamu, lazima tufahamu ya kuwa kuna tofauti kati ya kutabasamu na kucheka. Kucheka ni pale ambapo utakuja na mizaha ya zee comedy ili mwanamke acheke ilhali kumfanya mwanamke atabasabu utakuja na mbinu ambazo tutakueleza muda mfupi.

Tukija katika swala la kumfanya mwanamke atabasamu lazma ufahamu kuwa hauhitaji kufikiria sana. Lazima uwe natural. Sababu pindi utakapoanza kufikiria mbinu za kutumia kumfanya mwanamke atabasamu basi atakugundua. Hivyo la kufanya ni kuhakikisha unapumua vizuri na unatumia mbinu za kujiamini. [Soma: Jinsi ya kujiamini]

#1 Mpogeze.

Hii ni mbinu inayotumika sana na bado inafanya kazi. Lakini kabla hujatamka neno unapaswa kuanza na tabasamu. Weka tabasamu na umwambie maneno kama, “Wow! Leo unaonekana mrembo sana.” Ama unaweza kumwambia, “Hii nguo uliovaa leo imekupendeza sana”

Maneno kama haya hujayapangia, yanakuja yenyewe kulingana na mandhari ambayo mko. Mbinu hii ambayo imekuwa ikitumika tangu zamani hufanya kazi vizuri.

#2 Mnunulie kitu.

Hapa unafahamu ya kuwa lengo letu ni kumfanya mwanamke atabasamu na wala si kumtongoza. Kama unataka kumtongoza awe mpenzi wako ingia hapa. Ok, tukirudia kwa hoja yetu ni kuwa mwanamke huyu haimaanishi kuwa unapaswa kumnunulia zawadi, la. Hapa namaanisha unamnunulia kitu kama vile mumeenda klabu ukamnunulia kinywaji ama umeenda kwa mkahawa ukamnunulia vibanzi, chokoleti na kadhalika. Hii ni njia murua ya kumfanya atabasamu.

#3 Msaidie.

Huku ni kumsaidia pale ambapo anashindwa kufanya ama anahitaji msaada. Hii ni kuanzia kama anataka usaidizi wa kubebewa mizigo kwa gari, kumtengenezea aeaeri yake ya tv, kumsaidia kupiga picha akiwa na marafiki zake. Kiufupi ni yale mambo madogo madogo tu. Si lazima ufanye jambo la kuchekesha ndipo umwone mwanamke atabasamu.

#4 Shika macho yake.

Kumsuka mwanamke kwa kutumia macho kunatambulika kama mbinu fioa ya kutongoza mwanamke. Mbinu hii pia inakuwa na uwezo mkubwa wa kumfanya mwanamke atabasamu. Ukijifundisha mbinu za kutongoza kwa kutumia mwanamke itakuwa silaha kubwa katika nyaja ya utongozaji. [Soma: Jinsi ya kutongoza kwa kutumia macho]

Mbinu hii unaweza kuitumia katika klabu, hotelini ama kwa chumba tu. Kile unachohitajika nikuangalia macho yake kwa sekunde tatu halafu uangalie kando. Fanya hivi kwa muda wa kama dakika kumi na tano hivi na mwishowe unaona amekuwa interested na wewe na zaidi utamfanya atabasamu.

#5 Tafuta mwanya mowote ili ujitolee kwake.

Unaweza usipate nafasi ya kumsaidia na kitu, lakini kuna watu wengine wengi katika hii dunia. So mahali popote pale ulipo, makinika kutafuta mwanamke ambaye atakuwa anatatizika kufanya jambo. Hii pia itakusaidia pakuu kuondoa uoga wakati ambapo itafika ule wakati wa kuapproach mwanamke kumtongoza. [Soma: Hatua za kuondoa uoga wa kuapproach wanawake]

#6 Mwambie kuwa anafaa.

Well, hapa utamweleza anafaa kwa njia gani. Hii itategemea na vile ambavyo unamchukulia mwanamke huyu. Unaweza kuwa mumetoka matembezi na mumefurahia hadi jioni. Halafu wakati mnaagana unamwambia, “Wewe unafaa” Maneno haya bila shaka yatamfanya atabasamu.

#7 Kuwa gentleman. 

Kuwa gentleman ni kama vile ambavyo tumeeleza katika hoja ya #3. Gentle ni tabia za utu ambazo wanawake wengi hupenda. Ukimfungulia mlango, kumsaidia kuvuta kiti akae ni baadhi ya tabia za gentleman. Wanawake bila shaka watatabasamu ukiwa na tabia kama hizi.

#8 Kuwa romantic.  

Kando na kuwa gentleman, unafaa kuwa romantic muda wote ambao mtakuwa pamoja. Kuonyesha kuwa romantic ni pale ambapo unamwita katika mazingira ambayo kuna mishumaa, maua, chokoleti na kadhalika. Vitu hivi kwa mwanamke hufanya kazi sana.

Pia unaweza kudance na  yeye. Weka nyimbo ya kimahaba katika simu yako na uanze kudance na yeye polepole bila kukurupuka.

#9 Mshike mkono.

Wakati mnakutana na wazazi wake ama wazazi wetu ama kuwa katika hali ya wasiwasi, unaweza kuukaza mkono wake pole pole. Kufanya hivi kunakuwa na maana nzito ajabu. Hii ni ishara ya kumuonyesha kuwa ‘ijapokuwa hatuwezi kuongea sahizi, niko na wewe na wala siwezi kukuacha’

Finally ni kuwa kumfanya mwanamke atabasamu lazima ile hatua ya kwanza ni kumfanya ajihisi vizuri. Baada ya hapo, chochote kinaweza kufanyika. Hii ni mbinu mora zaidi ya kuanza mahusiano mazuri na mwanamke. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke acheke]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.