Jinsi Ya Kufanya Mwanamke Asikudanganye


Kuna wanawake wengine ambao ni waongo na hawaaminiki kwa mambo wanayosema. Na tabia kama hii huchukiza kwa yeyote.

Mnapanga kukutana sehemu flani, unafika hapo mapema, unamgojea awasili lakini hafiki. Unampigia simu hashiki halafu anakutumia SMS akikueleza ya kuwa amepata shughli ya dharura, ameenda airport kumpokea rafiki yake aliyetoka Dubai.


Wakati huo amekuacha na maswali ya kujiuliza "Nani atasafiri kutoka Dubai ghafla bila kujulisha na mapema?"

Well, usijisumbue. Mwanamke kama huyo amekudanganya kweupe.

So swali muhimu hapa ni kutaka kujua jinsi ya kufahamu na kujua jinsi ya kumzuia mwanamke asipoteze muda wako kwa sababu zisizokuwa na maana.

Zama nami...

1. Kutabiri kuzuia asikudanganye
Jambo la msingi la kuzuia mwanamke asikudanganye ni kujua mambo ambayo yanajionyesha dhahiri. Hebu tuongee ukweli, wakati mwingine tunajua wazi kama wanawake wanatudanganya. Lakini tatizo ni kuwa wanaume wengi hupuuza swala hili na kujipa moyo. Mwisho wa siku unaanza kujilaumu na kujutia kwa nini ulikubali kudanganywa kwa kusema: "Nilikuwa na hisia za kuwa ananidanganya....ningejua ningemwambia kitu na mapema" [Soma: Hatua za kufanya ili umfanye mwanamke aingiwe na wivu kwa manufaa yako]

Ok. Jambo hili halipaswi kutokea tena.

Badala yake, wakati ambapo unataka kukata simu baada ya kumwalika mtoke out muulize hili swali:

"Ok. Kabla hatujakutana hio siku, kuna kitu nataka nikuulize: kuna uwezekano kiasi kipi cha wewe kutotokezea katika______?"

Kawaida inakuwa hivi, wanawake waongo mara nyingi si eti kuwa hawawezi kuweka msimamo wao wa maneno, bali mara nyingi wanashindwa kukataa jambo flani ama kushindwa kusema 'hapana'. Hivyo mara nyingi wanakubaliana na kila utakachosema lakini watakataa kwa aidha kutopokea simu zako ama kutojibu sms zako. [Soma: Sababu za kwanini unafaa kufanya mapenzi na rafiki yako]

Hivyo ukimuuliza swali ambalo liko wazi kama hatokutana na wewe ni rahisi zaidi kujua msimamo wake badala ya kumuuliza kwa njia tofauti.

Kama akikataa unaweza kupanga wakati mwingine ambapo mnaweza kumeet.

2. Soma mvuto wake
Njia nyingine ya kutambua iwapo mwanamke anakudanganya ama hasemi ukweli ni kwa kusoma mvuto wake ama interest kwako. Kutaka kujua mvuto wake unaweza kumuuliza maswali ya kumpima kv "Unapenda kujifurahisha kwa kufanya nini?" ama "Unafanya nini kwa_____?" ama "Ushawahi kufanya____?"

Kumuuliza mwanamke maswali kama haya unaweza kujua iwapo yuko interested na wewe ama anakuenjoy. Wakati mwingi wanawake hutoa hila za fununu wakati ambapo wanayajibu maswali kama hawajiskii na wewe. Mwanzo mara nyingi huwa na tabia kama hii kama hawataki kukujibu moja kwa moja.

Kama umemakinika kuangalia mambo haya, itakuwa rahisi kwako kujiepusha kumuuliza mwanamke ambaye hajavutiwa kwako. [Soma: Dalili za kuonyesha kama mwanamke anakupenda]

3. Sheria ya kudanganya kwa mara moja
Ok hii ndio hatua ya mwisho na muhimu ya kufuata ili kuepusha asikudanganye. Hatua hii ni kuhakikisha ya kuwa mwanamke aina hii hana nafasi tena ya kukudanganya kamwe. Aidha ni achague 'ndio' au 'la'.

Kuongea kweli ni kuwa hata ujaribu kiasi kipi, kama mwanamke  ana tabia ya kukudanganya ni vigumu kwako kumrekebisha awe sawa. Hivyo sheria unayofaa kufuata ni hii:

Kudanganya mara ya kwanza kuwe mara ya mwisho.

Usipoteze muda wako kwa mwanamke muongo. Mwanamke aina kama hii aidha hajapendezwa na wewe ama ni mwanamke asiyekuwa na misimamo. Zaidi ni kuwa mwanamke aina kama hii atashusha hadhi yako katika jamii na pia kupunguza kujiamini kwako.

Kuna wanawake wengine wengi ambao wako single na wanatafuta wanaume wa dhati. Hivyo achana na wanawake wadanganyifu na uanze kumakinika na wanawake ambao wana uhakika. [Soma: Mwongozo wa kuchagua mwanamke mrembo]

So wakati mwingine ambapo utakutana na mwanamke mpya jaribu kutumia fomula hii ya kujua udanganyifu wake.
  1. Mpime mvuto wake kwa kumuuliza maswali ya kumsoma
  2. Hakikisha mara ya pili kwa kumuuliza uwezekano wake wa kutokezea kwa out yenu
  3. Akikudanganya mara moja....achana na yeye kabisa, muelezee sababu za wewe kuachana na yeye.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.