Ishara 7 Mwanamke Mwenye Aibu Huonyesha Kama Anakupenda


Mwanamke ambaye ana aibu na anakupenda ni rahisi kumtambua. Hawezi kukuambia moja kwa moja kuwa anakupenda lakini kuna ishara ambazo atajaribu kuzifanya aidha kimaksudi ama bila kujua.Ishara kama hizi unapaswa kuwa makini nazo na wala hupaswi kupuuza hata moja. Pia hakikisha ya kuwa unatambua ya kwamba mwanamke kama huyu unampeleka polepole na wala hauhitaji kuharakisha mambo. Ishara zenyewe za kutambua mwanamke mwenye aibu anakupenda ni kama zifuatazo.

1. Kukuangalia
Mwanamke kukuangalia kwa muda mrefu bila kuangalia kando ni dalili moja kuonyesha kuwa anakupenda. Hii pia hufanyika kwa mwanamke ambaye ana aibu. Ukihakikisha kuwa mwanamke aina kama hii anakuangalia wewe na wala si mwingine kwa muda ujue hio ni moja wapo ya dalili ya kukupenda. Ukimwangalia halafu kwa ghafla aangalie kando itakuwa ni ishara ya zaidi kuwa anakupenda. Hakikisha kuwa akikuangalia wewe mrudishie kwa kumwonyesha tabasamu. Hakikisha kuwa kama unamwangalia, usiangalie kando mpaka yeye aanze kuangalia kando. Ukiangalia kando wa kwanza utadhihrisha kwake kuwa hujapendezwa naye hivyo kumfanya yeye kuingiwa na aibu zaidi ya kujaribu kueleza hisia zake kwako. [Soma: Mbinu 3 kuu za kumfanya mwanamke akupende chini ya dakika 2]

2. Anapenda kukuonyesha tabasamu/smile zaidi kwako kuliko kwa wengine
Kuelewa hisia za tabasamu kwa mtu ni jambo gumu sana katika binadamu. Kutabasamu kunaweza kumaanisha kitu na pia kunaweza kusimaanishe chochote. Kama mimi ni wewe nikiona mwanamke akinipa tabasamu sitarukia kuanza kuingiwa na mawazo ya kuwa ananipenda. Kile ambacho nitafanya ni kumakinika na vile ambavyo anatabasamu. Je tabasamu hilo analipeana kwa kila mtu ana ni specially kwangu. Na je aina ya tabasamu hilo likoje.
Kwa mwanamke ambaye ana aibu, kutabasamu kunaweza kuwa ni tabia yake ya kila siku lakini kile ambacho utamakinika nacho nikuangalia tabasamu hilo analiweka vipi. Wakati akikupa tabasamu, hakikisha kuangalia miondogo yake ya midomo na pia yaangalie macho yake kwa undani. bila shaka kama anakupenda utangundua mara moja.

3. Anapenda kucheka wakati unapofanya ama kutoa mizaha/jokes zako
Ok labda wewe ni mtu mcheshi ambaye hakupiti neno moja bila kuchekesha watu. Kila mtu anakujua wewe ni mcheshi lakini kuna huyu mwanamke mwenye aibu ambaye kila neno utakalotoa lazima yeye acheke. Hata kama umetumia maneno ambayo hayachekeshi kabisa bado utamwona akicheka. Hapa kuna vitu viwili ambavyo vinaweza kuashiriwa. Anaweza kuwa ni naturally kuwa yeye anapenda kucheka ama amekuzimia na amependezwa nawe.[Soma: Mbinu wanawake hutumia kutongoza wanaume bila kujulikana]

4. Anapenda kukugusa ama kukushika kwa bahati mbaya mara kwa mara
Kama anapenda kukugusagusa mara kwa mara wakati anapoongea itakuwa ni habari njema kwako. Wanawake kwa kawaida wanajitambua kwa miili yao na kawaida wanapenda kuwagusa wale ambao wanawapenda. Kama anapenda kukugusa kwa mabega kwa bahati mbaya hii ichukulie kama ishara ya kuwa mwanamke kama huyu anakupenda kwa kiasi fulani.
Onyo: Kuwa makini, hata kama mwanamke kama huyu ni mwenye aibu na mara kwa mara anapenda kukukumbatia, inaweza labda kumaanisha tofauti kabisa. Labda mwanamke kama huyu amejenga ukuta wa kukufanya wewe rafiki yake pekee. Yaani kwa kimombo tunaita 'friend zone'. Anaweza kukueleza mambo yake yote huku akilini mwake akijua kuwa wewe ni rafiki yake thabiti na hauwezi kuwa mpenzi wake.[Soma: Jinsi ya kuuhepa mtego wa mwanamke kukutia katika 'friend-zone']

5. Anapenda kuongea na kila mtu isipokuwa wewe
Hii ni tabia halisi ya mwanamke mwenye kuona aibu. Wakati mwingine mwanamke aina hii huona aibu kwa mtu mmoja tu na kwa wengine anakuwa mtu wa kawaida. Ushawahi kumgundua kuwa kwa watu wengine anakuwa huru kuongea nao lakini akifika kwako anaingiwa na aibu nzito.
Hili ni jambo la kawaida ambalo hutokea kwa wanawake, labda hataki kuongea na wewe kwa kuwa na uoga wa kuongea kitu ambacho kitamuaibisha ama kuongea mambo ambayo utayaona hayafai. Pia labda atakataa kuongea na wewe ili kukuona una wivu kiasi gani akiwa anaongea na wanaume wengine.

6. Anakuwa na tabia isioeleweka
Ushawahi kumwona akiangusha vitu vyake kwa sakafu kwa bahati mbaya ama kuonyesha tabia nyingine za kutatanisha? Ashawahi kukuuliza maswali ya kijumla huku akijua wazi huwezi kuyajibu? Wakati anapoongea na wewe wakati mwingine ushawahi kuongea mambo kumhusu ambayo anayafanya kama ni lazima kwa maisha yake? Ama kwa kawaida anapenda kuongea na sauti kubwa lakini pindi unapotokezea anabadilisha sauti nk?
Dalili hizi zote zinamwonyesha kuwa ameingiwa na wasiwasi akiwa karibu yako.

7. Anapenda kujichunguzachunguza
hivi anajaribu kujipendekeza kwako kuonekana kama hana tatizo lolote vile alivyovyaa. Utamwona mara kwa mara akijishika nywele zake ama kuivuta nguo yake ili ionekane imekaa vizuri ama kushika miwani yake mara kwa mara. Kila kitu ambacho anafanya ni kuhakikisha kuwa kinaoneka vizuri machoni mwako.
Kama wataka kujua mwanamke amekuzimia haswa mkiwa date pamoja atakuwa kila ya madakika akienda msalani kujiangalia kwa kioo kuhakikisha ya kuwa anaoneka mrembo akiwa mbele yako.[soma: Aina za wanawake unazofaa kuepuka nao]

8. Kila mahali uendapo atakuwa hapo
Anakula hoteli unayoenda, anapenda kuwa karibu na marafiki zako, na parties zote utakazoenda atakuwa hapo. Tabia ambazo uzianza mpya kwa ghafla utamwona mwanamke kama huyu amekuwa nazo. Wakati ambapo kila mtu atakuwa ameenda, yeye atakuwa wa mwisho ili mradi awe karibu yako.
Dalili hizi zote zinaweza kutokea kwa nyote wawili kwa bahati mbaya lakini kama zitatokezea na baadhi ya dalili nyingine za kushuku, basi itakuwa mwanamke huyu anafanya hivyo ili kukuona umeridhika na amekupendeza.

Ok kumalizia ni kuwa mwanamke kama huyu inaweza kuwa vigumu kumwelewa sababu mara leo atakuwa hivi ama keshoa jeuke hivyo ukipata nafasi kama hii ukiona anakuzimia ama kuonyesha dalili zozote, hakikisha ya kwamba haupotezi nafasi yoyote ile kwani hatabiriki kwa urahisi.[soma: tabia ovyo za wanawake ambazo wanaume hupenda]


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.