Ishara 9 Za Kutambua Kama Mpenzi Wako Anakukontroli


Kukontrol mtu ni ile hali ambayo mtu hawezi kuwa na maamuzi yake ya kibinafsi bila ya kumshirikisha mwingine, kila kitu ukitaka mtu akufanyie anafanya bila kuuliza swali lolote.


Katika machapisho yetu ya awali ya Sanaa Ya Kutongoza hapa kwa blog yetu ya Nesi Mapenzi, tulilizungumzia hili swala la kukontrol wanawake kwa kina. Tukaona manufaa yake kwa mwanaume yeyote.

Lakini pia sanaa hii ya kukontrol mtu inatumiwa na wanawake, na mara nyingi mbinu hii wanaitumia kifioa kiasi cha kuwa inakuwa vigumu kwa mwanaume kutambua kama mpenzi wake anamkontrol.

Tatizo baya la mwanaume kuweza kukontroliwa na mwanamke ni kuwa atajeuzwa kuwe bwege na maisha yake yatakuwa ni magumu. Mfano hatakuwa na uwezo wa kumwambia mwanamke chochote hata kama anakosea na mbaya zaidi kutokea ni ile hali ya kuwekwa kwa chupa.

Lakini kabla haya yote hayajatokea, leo tumeamua kuja na mbinu za kutambua ishara ambazo zitatoa ufahamu ujue kuwa mpenzi wako anakukontrol au la.

Zama nasi...

#1 Wakati wowote mnapokosana, ni wewe ndiye unayelaumiwa. 
Ukiwa na huyu mwanamke na kila wakati mkiwa mnagombana, mwisho lazima uchukue lawama hata kama kosa ulilofanya si lako. Na utapata mwanamke huyu ataushikilia msimamo wake na atatumia mbinu zozote zile kuhakikisha kuwa lawama inakuangukia wewe.

Hii ni ishara ya mwanamke anayekukontrol kwa kuwa anatumia mbinu hii kuishusha confidence yako mbele yake. Hivyo hii ni ishara kuu ambayo hujitokeza katika kila mwanamke anayetumbia mbinu ya kukontol mwanaume.

#2 Anakasirika haraka kama hakupata kile ambacho alikuwa anatarajia. 
Hii ni ishara nyingine inayodhihirika kwa wanawake aina hii. Wao kila wakati wanatarajia mambo yao kuenda sawa, lakini ikitokea siku ambapo hapakwenda vile wanatarajia basi wanakasirika haraka. [Soma: Hatua 8 mtu hupitia baada ya kuachwa na mpenzi wake]

Mfano labda umemuahidi kitu flani lakini hukukitimiza kwa wakati unaofaa, utamuona akikasirika bila sababu. Hii ni mbinu wanayoitumia ili kuifanyia ufidhuli akili yako ili uweze kutimiza wanachotaka wakati wowote wanapojiskia.

#3 Wakifanya jambo lolote, lazima wakujulishe.
Mwanamke anayependa kukontrol watu hupenda masifa ya kusifiwa wakifanya jambo zuri. Kwa mfano anaweza kuwa amepika chapati tamu hivyo atataka umpe sifa. Sifa hizi ndizo ishara ya kuonyesha kuwa anatabia za kukontrol watu.

Zaidi anaweza kutaka sifa hizi ziwafikie hata marafiki zako na familia yako ukimsifia jinsi alivyo mpenzi bora zaidi ya wote.

#4 Hakuna kitu unachofanya anakiona kizuri.
Hata umpeleke Dubai ama umtoe akaone shoo ya Fiesta, bado ataona ya kuwa hujafanya jambo ambalo linafikia kiwango cha kusifika. Mwisho wa siku utaendelea kufanya kila mbinu ili angalau uweze kumridhisha.

Lakini siri ni kuwa kile ambacho anachofanya hapa ni kukufanya uhisi ya kuwa haumfurahishi vile ambavyo inafaa. Hivyo utatia bidii kiasi cha kuwa utajiona haumfai ama haumtoshelezi. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akupende]

#5 Anauliza kila kitu unachofanya.
Mwanamke anayekukontrol kwa kawaida hajiamini. Yeye hujiona kuwa na thamani ya chini hivyo kila kitu ambacho utakuwa unafanya atataka kujua ni nini. Hii hutokea kwa kuwa hakuamini na chochote ambacho umefanya ama utafanya. Yaani kiufupi hatakubali kuona unamshinda kwa chochote. Na pia atataka kujua mafanikio yako yote ili aweze kunufaika na kwayo.

#6 Anatumia ngono kama kigezo cha kukukontrol.
Wanawake wanajua umuhimu wa ngono kwa mwanaume. Hivyo mwisho wa siku kila mwanamke atatumia mbinu zake ili kutaka kile anachotaka kupitia mapenzi.

Lakini ukiona mwanamke anakunyima msifanye mapenzi kwa kuwa hujamnunulia kitu fulani ama hujamfanyia jambo fulani, basi uwezekano mkubwa ni kuwa mwanamke huyo anakukontrol.

#7 Anakutishia kukuacha.
Mwanamke anayekukontrol hupenda vitisho vya mara kwa mara vya kukuambia kuwa atakuwacha bila hata kumkosea ama kumfanyia jambo lolote baya. Mwisho wa siku kwa kuwa unampenda utakuwa tayari kumfanyia lolote lile ambalo anataka umfanyie bila hata kufikiria mara mbili.

#8 Mwivu.
Kila mtu anakuwa na chembechembe za wivu ndani yake. Lakini mwanamke anayekukontrol anakuwa na wivu uliopita kiasi, na mara nyingi chochote unachofanya lazima aone wivu.

Mfano unaweza kuwa unapiga simu za kikazi na ni mwanamke unayeongea naye utamkuta anatega maskio kutaka kujua ni nani unayeongea naye na ni kwa nini.

#9 Anakuaibisha.
Mara nyingi mwanamke huyu yuko tayari kukushusha hadhi ujione ya kuwa haufai. Pia anaweza amekubandika jina la kimajazi ama ukifanya jambo anaweza kukuangalia na uso wa kuonyesha kuwa unafanya upumbavu. Lengo lake kuu hapa ni kuhakikisha kuwa anashusha confidence ndani yako. [Soma: Dalili za kuonyesha mpenzi wako amechoshwa na wewe]


Ok. Kama umejikuta katika mahusiano na mwanamke na ameonyesha moja ya ishara hizi usiharakishe kuona kuwa anakukontrol, lakini ukiona ameonyesha isha zaidi ya tano ya hizi basi fahamu mwanamke unayempenda anakukontoli. Upo!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.