Jinsi Ya Kumzuzua Mwanamke Na Kumsuka Mpaka Akupende


Kila mwanaume anapenda kutaka kujua jinsi ya kumzuzua mwanamke mpaka ampende. Lakini wengi hushindwa kutimiza azma hii kwa kuwa hawajui mambo muhimu ya kufanya ili aweze kumzuzua mwanamke.

Je, uko tayari kuzijua mbinu TANO kuu za kumfanya mwanamke azuzulike kwako?


Najua labda ushawahi kuwaona mwanamke fulani wakiweza kuzuzuliwa na mwanaume, na mwanamke kama huyu anacheka mara kwa mara huku akikiri kuwa mwanaume flani anajua kuzuzua. Well, waonaje kama ni wewe sasa hivi unapewa sifa kama hii?

Kupewa sifa ya kuwa mzuzuaji na mwanamke ni sifa kubwa zaidi kwa mwanaume kutoka kwa mwanamke. Na si kwa ajili ya sura, shepu wala ujanja wako. Yote itategemea na kipawa chako na tajriba yako wa kuzuzua.

So, utamzuzua vipi mwanamke?

Kumzuzua mwanamke kutategemea uwezo wako wa kuwasiliana na yeye na kumfanya ajihisi kuwa na furaha wakati wote. Tumia mbinu tano ambazo tumezihakikisha utendaji wake.

#1 Ongea na yeye mambo ambayo anataka
Unaweza kuona kuwa haina umuhimu wowote, sababu wanaume wengi hufanya hivi. Wanaume wengi hubaki wakijiuliza kuna haja gani  kwao kuongea mambo ambayo mwanamke anataka kuongea. Mbona wanawake hawawezi kuongea mambo ambayo mwanaume pia anataka?

Bila shaka, wanawake wanaweza. Wanawake pia wanakuwa active kutaka kujua aina ya mwanaume ambao wanajihusisha nao. Lakini wakati mwingine, haswa unapotaka kumfurahisha na kuteka atenshen yake kwako, ni vizuri kujua mambo ambayo yanagonga ndani ya kichwa cha mwanamke. Na kumakinika kuteka atenshen yake haimaanishi kuwa mwanaume anapaswa kuongea kuhusu mambo ya vipodozi na urembo na mwanamke, La. Daraja kati ya mwanaume na mwanamke imepungua siku hizi. Ni rahisi kuongea na mwanamke mambo ambayo anapenda bila hata kutatizika. Bora tu uhakikishe kuwa utaweka kando maswala ya mipira, elekroniki na hesabu katika mazungumzo yenu.

#2 Msuke
Wakati unapozungumza na mwanamke, ni rahisi kumfanya aweze kuongea na wewe. Lakini hio haitoshi. Kama unataka kumzuzua mwanamke basi unahitajika kumfanya ajihisi huru, na pia umuonyeshe kuwa uko interested na yeye.

Marafiki hawawezi kuzuzuana hadi wavuane chupi. So kama utaongea na yeye kama rafiki yako basi atakuona tu kama mwanaume anayevutia. Lakini hatakuona kama mwanaume anayezuzua. Kutaka kuonekana kama mwanaume mweye uwezo wa kuzuzua machoni mwa mwanamke, basi unahitajika kumfanya akuone wewe kama mwanaume ambaye anaweza kutoka naye deti. Na kufanya hivyo lazima umsuke.

Na unapochukua hatua ya kumsuka hakikisha kuwa hautumii maneno kama ‘unapendeza’, ‘leo umerembeka’, ama kutumia mstari wowote ambao unaendana na hii. Inaboesha na haionekani kuwa na uhalisia wowote. Badala yake tumia maneno ambayo yanamlenga yeye moja kwa moja. Umemuona amepaka wanja kwa macho? Mwambie “Leo nauona utofauti kwa sura yako, kwani umejipaka nini?” akijibu hajui, ama akikwambia ni wanja mtamkie, “Basi unapendeza kupindukia, hata nashindwa kuacha kukuangalia.” Haya ni baadhi ya maneno ambayo unaweza kumsifia yeye binafsi na moja kwa moja.

Kwa kumsuka utakuwa umefanya mambo matatu wakati mmoja. Kwanza ni kuwa umemchangamsha kwa kumfanya atabasamu. Pili umemfanya atambue kuwa wewe umemuona anapendeza. Na tatu ni kuwa umemuonyesha kuwa umevutiwa na yeye. Yote haya ni ya kufanya ili akutizame kama mwanaume ambaye anaweza kutoka deti na yeye.

#3 Kuwa mcheshi
Kufikia sasa kwa kuwa tayari ushamfanya kuwa na tabasamu kwa kumsuka, ni wakati wa kuingia katika himaya yake binafsi. Kila mtu huwa na himaya yake binafsi na kawaida hatujihisi huru iwapo mtu mwingine ataingia katika himaya zetu unless mtu huyu ni mtu ambaye tunajihisi comfortable naye. Ok, kwa kueleza juu juu ni kuwa mfano hauwezi kumuaproach mwanamke usiyemjua halafu uende ukakae na yeye sako kwa bako na uongee na yeye kana kwamba ni mtu unayemjua na kufahamiana naye tangu kitambo bila kufuata taratibu zake.

Kumfanya ajihisi huru na wewe, lazima uwe na muda  mrefu na yeye ili akuzoee. Akikuzoea hapo sasa unaweza kutumia ucheshi ambao unaweza kuutumia kwa manufaa yako. (machapisho ya awali tuliongea kuhusu jinsi ya kuwa mcheshi)

Hapa hakikisha kuwa wakati unapomchekesha mwanamke usitumia wala usijilazimishe kutumia hekaya ama stori za kuchekesha ulizozisikia mahali ama kusoma kitabuni. Kinachohitajika kwako ni kuwa mhalisia tu, mwanamke akipendezwa atacheka tu.

#4 Mtongoze
Wanaume huwatongoza wanawake kila wakati, lakini wakati mwingine wanawake wanahisi kuwa wanaume wanaowatongoza ni mafala. So usivuke mipaka yako wakati unapomtongoza sababu anaweza kukubeza. Mbinu rahisi ya kuanza kutongoza ni kwa kuanza kwa wepesi. Muulize wikendi atakuwa wapi baada ya shughli zake za wiki, muulize kuhusiana na sehemu anayopenda kubarizi na pia mkahawaha anaoupenda, na kitu chochote kile kinaweza kuhusiana na yeye moja kwa moja. Atajua kuwa unajaribu kumtongoza kwa sababu hakuna mtu anaweza kuuliza maswali haya bila lengo madhumuni.

Halafu mrushie hili swali.

“Enhe, hii inaweza kuwa personal, hivi wewe una boyfriend? Kama uko naye, basi moyo wangu naona unaweza kuyayuka wakati wowote kuanzia sasa!”

Hii inaweza kuoneka nzito lakini hufanya kazi wakati wote.

Atacheka, lakini mstari huu utakuwa umepitisha lengo lako kwako, na atajua kuwa uko interested na yeye. Lakini usifanye mambo yaende segemnege kwa kunyamaza kwa muda baada ya kukupa jibu lake. Endelea na stori nyingine ujifanye kana kwamba swali hilo halikuwa na umuhimu wowote kwako. Lengo lako umeliweka wazi lakini hutaki ajihisi kuwa hayuko huru mbele yako.

#5 Mguse
Hii ni sehemu hatari, lakini unahitaji muda kujifundisha. Unataka kujua jinsi ya kumzuza mwanamke, sawa? Basi kumgusa wakati ufaao inakupa point tano muhimu ambazo unahitaji kujua ili umzuzue mwanamke. Kama umepata kila kitu sawa, basi utakuwa umefanikiwa kwa kila kitu.

Lakini tena kumgusa mwanamke ni sawa na kucheza na moto. Ukiwa na haraka ya kuuguza hautahisi lile joto. Na ukikaa muda mrefu ukiugusa, utachomeka. Unaona venye hatari iliopo hapa?

Unaweza kutuma msisimko hadi kwa uti wake wa mgongo kwa kumgusa kiulaini kama tayari umemchangamsha awali. Lakini kumbuka hili, mguse wakati ambao unataka kumgusa pekee, kama vile kugusa sikio lake wakati unapomsifia kuhusu vipuli alivyofaa, kupapasa nywele zake wakati kuna upepo mkali, ama kuuwekeza mkono wako nyuma yake wakati mnavuka barabara. Mguso ni njia ya kuingia katika hulka ya mwanamke, so unahitajika kuwa makini zaidi na umsome vile ambavyo atareact kabla umguse kwa mara ya pili.

Upo?

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.