Ishara 12 Kuonyesha Mwanamke Ulienaye Anakutumia Halafu Akutende


Wazungu hupenda kusema ‘Love is blind’, yaani mapenzi ni kipofu. Usemi huu ni wa kweli kwa sababu unaweza kuona wapenzi wawili wamependana kiasi cha kuwa hata ukimkanya mmoja wao kuhusiana na jambo flani hawatakuelewa.


Ni vizuri kuwa katika uhusiano wa kimapenzi aina hii. Hukuza upendo. Lakini swali linakuja pale ambapo unajiuliza iwapo huyu unayempenda naye anakupenda?

Wanaume wengi wanashindwa kutambua kati ya kupenda na kutendwa. Wengine wanazama katika mapenzi bila kuyaelewa na mwishowe utaskia katika runinga na maredioni kuwa mwanaume amejinyonga kisa ni mwanamke ama utaskia mwanaume amemuua mpenzi wake kisa kamcheat.

Well, kabla mambo yafikie hapo, lazima ujue iwapo huyu unayempenda anakuchezea ama yuko serious nawe. Ndio maana leo hapa Nesi Mapenzi tumekuja na ishara ambazo unaweza kuzitambua iwapo mwanamke unayemchumbia yuko serious ama yuko tu na wewe kukutumia halafu akishamaliza tu akuteme kama mate.

Ishara #1. Unajihisi hujakamilika.
Ukiwa na yeye unajihisi kuwa kuna kitu ambacho kinakosekana. Hii mara nyingi inatokea kwa sababu hamgawi hisia moja. Hii ndio inakufanya uhisi kuna kitu kinachokosekana. Unajaribu kila uwezavyo kumfanya akupende zaidi lakini kila mara ukijaribu unafeli na unauangukia mtego wako mwenyewe.[Soma: Ishara za kuonyesha kuwa anakupenda]

Ishara #2. Yeye ndie anayemiliki uwanja.
Unahisi kuwa ni wewe pekee unayejitolea kufanya kila kitu. Unajifua kila wakati ili uhakikishe unampendeza lakini kwa upande wake hakuna kitu chochote ambacho anajitahidi kukuridhisha nacho.

Kama yeye ndie anamiliki uhusiano wenu haimaanishi kuwa anakutumia lakini anajaribu kukuonyesha uhusiano wenu si wa afya. Uhusiano mwema ni ule ambao unahusisha watu wawili nyakati zote.

Ishara #3. Wewe ndio nguzo yake.
Kama anahitaji sapoti kihisia, wewe ndie anakukimbilia. Mazungumzo yake mara nyingi huzunguka maisha yake na shida zake ambazo anazipitia. Lakini je unapopatika na shida? Anakusikiliza ama anakupuuza? Well, kama hana time na wewe kuskiza shida zako basi hayo si mahusiano ya kudumu.

Ishara #4. Anakutuza wakati umemfanyia jambo zuri kwake.
Hapa ni kama tu vile ambavyo unamwekea farasi nyasi mbele yake ili awe na motisha wa kuendelea kukimbia. Kiufupi anakutumia vibaya ili ufanye kitu ama jambo ambalo ulikuwa hutaki kufanya lakini mwisho wa kumfanyia jambo hilo anakupa hizo nyasi kama zawadi. Nyasi hapa inaweza kuwa ni kukupa uroda, kujipa majukumu ama mapenzi ya muda. Mambo kama haya hayahisabiki kama upendo ama uhusiano kabisa.[Soma: Jinsi ya kumwomba mwanamke mtoke out]

Ishara #5. Ni mtu asiyeeleweka.
Ule wakati ambao umechoshwa na tabia zake mbaya unamwona anajileta chini kabisa. Ananyenyekea mbele yako huku mikono yake yote anaikumbatia kwako. Imefikia ule wakati ambao yuko karibu kupoteza kila kitu so analeta visababu ambavyo havieleweki kabisa.

Mfano mchunguze kama anafanya jambo kama hili. Je huwa anakuwa mnyeyekevu ama kulia wakati ambao unajaribu kumlazimisha akupatie nafasi uwe pekeako, yaani umechoshwa naye so unataka akuachilie uyafikirie maisha yako? Well, hapa hudeal na mwanamke ambaye haeleweki bali unadeal na mwanamke ambaye anakutumia.

Ishara #6. Anataka nafasi binafsi.
Huyu mwanamke mumekuwa mkispend wikendi mkiwa pamoja kila wakati lakini sikuhizi amebadilika eti anataka nafasi yake binafsi. Anakuchukulia kama mwanaume wa kawaida na hakuoni kama uko special kwa njia yeyote ile?

Halafu ule wakati unahisi kama umechoshwa na tabia zake unamwona ndio huyu hapa amejileta tena.

Ishara #7. Watu wake hawakujui.
Ana marafiki kadhaa lakini hujawahi kukutana na hata mmoja wao. Marafiki wake ndio wanafaa kukukosoa lakini hakuna siku hata moja atakutambulisha kwao. Hii ni kwa sababu hakuoni kama mtu ambaye atakuwa naye maishani. Wewe ni mwongozo tu wa kupata mwanaume mwingine. [Soma: Mwongozo wa kutafuta mchumba bora]

Ishara #8. Anapenda akaunti yako ya pesa.
Unaweza kuwa unaichukia kazi yako na kila wakati unalalamika, lakini kwa upande wake anaipenda. Na ikija maswala ya kuzungumzia pesa zako anakuwa makini zaidi ya yote. Hapa ni lazima amakinike zaidi kwa kuwa sababu yake kuu kuwa na wewe ilikuwa ni hizo pesa zako, hakuna zaidi ya hapo.

Ishara #9. Marafiki na familia yako hawampendi.
Kuna uwezekano mkuu kuwa marafiki zako ama familia yako ishawahi kukutana naye angalau mara moja. Na mara nyingi familia huwa wanatoa maoni yao ya ukweli bila kukuficha. Kiufupi hawampendi.

Na wakati huo huo unapata kuwa mpenzi wako nae hataki kujihusisha na familia yako. Lake kuu anataka umakinike na yeye pekee na wala si watu wengine.

Ishara #10 Anajivutia kwako nyakati flani za siku.
Hii inaweza kuonekana kama wazimu lakini ushawahi kugundua kuwa anatabia ya kuwa na wewe kabla jioni ama baada ya saa mbili usiku. Si tabia ya kawaida lakini pia inaweza kuwa na maana flani. Kama anakutana na wewe baada ya saa mbili usiku pekee basi anakutumia kama mtu wa kujitosheleza na wala hataki kuwekeza zaidi kwako.

Ishara #11. Unaogopa kusema sitaki.
Hili jambo hufanyika mara nyingi haswa wakati mwanamke ameitumia saikolojia kukukoroga akili. Wengine huitwa kufungwa kamba. Unaogopa ukikataa mbeleni kuna adhabu ambayo amekupangia. Labda atakunyima uroda ama anaweza kukatiza favour ambazo umezoea kuwa anakupatia ukimfanyia jambo flani.

Ishara #12 Ukisema kitu ambacho unataka anakuona mbaya.
Unaweza fikia level ambayo unaona kuwa uko katika relationship lakini hupati kile ambacho unatarajia. Halafu unamuapproach unamwelezea kuwa kuna kitu unakosa katika relationship yenu. Halafu badala ya kukubali, yeye anakunyooshea kidole kukuambia kuwa lengo lako pekee ni kula uroda na mapenzi na wala humhudumii kama mwanaume wa kweli.

Upo!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.