Tumia Mbinu Hizi 7 Kumuomba Deti Mwanamke Kupitia Meseji Na Akujibu ‘Sawa’


Siku hizi mambo yamebadilika. Kitambo wakati ulikuwa unataka kumwomba mwanamke utoke deti na yeye ulikuwa unaenda hadi kwao nyumbani nyakati za usiku na kuanza kupiga mbinja ama ishara tofauti tofauti ili kumtumia jumbe za siri mwanamke atoke kwa nyumba.

Mambo yalikuwa magumu sana iwapo unataka kukutana na mwanamke. Siku hizi teknolojia imerahisisha mawasiliano kiasi cha kuwa unaweza kumwomba mwanamke deti kupitia kwa simu yako ukiwa katika sehemu yeyote ile.


Tatizo ni kuwa si kila mtu anaweza kuitumia teknolojia hii kikamilifu. Wengi wanaweza kuwa na simu lakini hawajui mbinu za kuwaomba wanawake deti. Mara nyingi hujaribu na wanafaulu kwa asilimia 50. Uzuri ni kuwa kuna mbinu nyingi ambazo unaweza kutumia ili kufanikisha hatua za kumwomba mwanamke deti.

Hapa katika blog ya Nesi Mapenzi, tumekuandalia mbinu ambazo unaweza kuzifuata ili uweze kumwomba mwanamke deti na akubali bila kukataa.

Zama nasi!

#1 Anza na maneno ya nguvu.
Usianze kwa kumtumia meseji zile za kawaida. Meseji zile za kawaida ni kama vile
“Mambo”,
“Vipi”,
“Hali yako”,
“Unafanya nini?”
na kadhalika.

Meseji kama hizi zitamfanya mwanamke achoke na wewe haraka sana na ataamua kukatiza mawasiliano yako ama hatoweza kukubaliana na wewe kukubali mwaliko wako. Hivyo ni vizuri kuhakikisha ya kuwa unakuja na mbinu tofauti za kuanza gumzo na mwanamke. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akupende mara ya pili]

#2 Jaribu kusoma hisia zake.
Wakati unapokuwa unachat na mwanamke, kuna hisia ambazo utaziona kama mwanamke hajiskii na kuongea na wewe. Kuna mambo kadhaa ambayo anaweza kukuonyesha. Nayo ni kama vile;


  • Kujibu meseji zako baada ya muda mrefu.
  • Kukujibu kwa meseji fupi fupi.
  • Kutumia majibu kama vile ‘ndio’ na ‘la’
  • Kukuambia kuwa hajiskii kuongea 


So mambo kama haya lazima uyatambue wakati unachat na mwanamke. Ukiona anaonyesha ishara hizi, basi hupaswi kumwambia kuwa unataka kutoka naye deti. La kufanya unapaswa uchat na yeye polepole kisha baada ya muda unamwambia kuwa una shughli na utawasiliana na yeye baadae.

#3 Endelea na gumzo.
So ukimwona ya kuwa meseji anajibu vizuri, basi hii ni nafasi nzuri ya wewe kuendeleza mawasiliano na yeye bila kusitisha. Kama ni mwanamke anayependa kuongea basi hautakuwa na shida kuendeleza mazungumzo. Ukimwona ni mwanamke ambaye si mchangamfu katika mazungumzo basi unaweza kumuuliza maswali ambayo yuko interested nayo. Pia unaweza kufanya utafiti zaidi kumhusu ili uweze kumuuliza maswali mengi bila tatizo. [Soma: Maswali mazuri ya kumuuliza mwanamke]

#4 Ingia kwa lengo lako.
Tumekuwa tukimtumia jumbe kwa muda sasa, najua kufikia sahizi utakuwa unajiuliza maswali ya ni wakati gani unapaswa kumwambia mwanamke huyu kuwa unataka kutoka deti na yeye. Jibu hapa ni kuwa usiwe na haraka ya kumwambia kuwa unataka kutoka na yeye deti, ngojea hadi wakati ule ambao utakuwa sawa.

#5 Mwambie unataka kumtoa deti.
Hapa usiwe na woga wa kumwambia mwanamke ya kuwa unataka kutoka deti na mwanamke. Unaweza kutumia mbinu zozote zile kumwomba mwanamke kuroka deti pamoja. Kuna baadhi ya maneno unaweza kumwambia kama vile;


  • Kesho uko free kuna sehemu nataka kwenda lakini sikujui vizuri, unaweza kunipeleka?
  • Kuna mkahawa mpya nimeuona town, kesho uko free twende kukakuangalie?
  • Nataka kesho twende tukaangalie filamu mpya katika sinema mimi na wewe.


Haya ni baadhi ya maneno ambayo unaweza kumwambia mwanamke bila kukataa. Kama umekuwa ukiongea na mwanamke bila tatizo basi mwanamke huyu anaweza kukubali bila kukuuliza maswali.

#6 Kuwa na mpango.
Akikubali kutoka deti na wewe basi hakikisha ya kuwa unajipanga. Usiende deti na mwanamke sehemu ambayo huijui. Na kama ni sehemu ambayo huijui vizuri basi unahitajika kutembea sehemu hio mapema kabla ya siku yenyewe.


#7 Mpangie siku yenyewe.
Hakikisha ya kuwa haumuachii mwanamke siku na wakati wa kutoka deti. Wewe ndie unapaswa kumwambia saa na siku. Hii ni mbinu muhimu ya kuonyesha ya kuwa wewe una chembechembe za uongozi na pia tabia za kialpha. [Soma: Maswali ya kumuuliza mwanamke katika deti]

Hizi ndio baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuzingatia wakati unapotaka kumwomba mwanamke kutoka deti na yeye.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.