Hatua 5 Za Kuapproach Mwanamke Wakati Wowote


Ok, hili swala tushawahi kuliongea awali. Tumeshaongea kuhusu mbinu za kuapproach mwanamke. Lakini kwa kuwa wewe ni reader wetu tunaekujali, tumeamua kuja na mbinu mpya bora zaidi na pia kuongezea zile za zamani ili kuweza kurahisisha mchakato mzima wa kuapproach mwanamke kwa haraka.


Ujanja wa kuapproach mwanamke ni mmoja tu, nao ni kuondoa uoga wakati unapochukua hatua ya kwanza. Leo tutakupa mbinu za kuchukua haraka ili uoga usiweze kukuingia na kukukatiza tamaa ya kuwinda windo lako.

#1 Fuata sheria ya sekunde tatu.

Ukimwona mwanamke ambaye unataka kumuapproach, kwa kawaida kuna zile sekunde tatu za kwanza ambazo unafaa uchukue hatua kabla ile sauti ambayo inajaribu kuongea na wewe kukujia.

Kila mwanaume akichelewa kuapproach mwanamke kuna ile sauti ambayo inaanza kukuongelesha. Hii ndio sauti ambayo inawafanya wanaume wengi wabaki kuwa single milele. So la kufanya hapa ukimwona mwanamke unayetaka kumuapproach basi fanya fasta. Una sekunde tatu za kuweza kufanikisha mpango mzima.

#2 Tengeneza miondoko yako ya mwili.

Pindi utakapoanza hatua ya kumuapproach mwanamke unahitajika kuweka kifua chako mbele, mabega nyuma, kidevu juu kiasi cha kuwa unaweza kuangalia pua yako na chini. Ok, wengi wanaweza kudhania huu ni ujinga lakini sivyo.

Pozi kama hili linakupa confidence ya papo kwa hapo. Hii ni pozi ya mwanaume alpha. Damu itakuwa inachuruzika vizuri kwa mwili na ubongo wako hivyo kuweza kukupa uwezo wa kujiamini na kumakinika. Anyway, pozi kama hili limepitishwa na wanasayansi na tumekuwa tukiongea umuhimu wa kutumia pozi aina kama hii tangu kitambo.

#3 Weka kiwango cha mazungumzo.

Hii ni muhimu kwa kuwa utakuwa umejiweka katika hali iliyo salama wakati unaongea na wanawake. Woga wa mwanaume ni pale wakati anakuwa na mawazo ya kukataliwa ama kuonekana mjinga mbele ya wanawake.

So kwa kujiwekea kiwango flani cha mazungumzo na mwanamke kunasaidia kuondoa ama kupunguza ule wasiwasi ambao unaweza kujitokeza na badala yake unakuwa umerelax. [Soma: Mbinu za kuyafanya maongezi na mwanamke kuwa marefu]

Mfano unaweza kumuapproach mwanamke halafu ukamwambia, “Nilikuwa naelekea sehemu flani lakini...” ama “Nilikuwa naenda kukutana na marafiki zangu lakini...”

Kile unachofanya hapa ni kuwa unatoa sababu za kwa nini umeamua kumuapproach mwanamke. Na uzuri wake ni kuwa watakuwa na maswali wakijiuliza, “kwa nini umeamua kuongea na mimi”.

Pia utakuwa unamwambia una haraka ya kuwa mahali so ile hali ya kupanic itakuwa imejiondoa automatic.

#4 Anza maongezi. 

Hapa ndio kizungumkuti hutokea. Wanaume wengi wangependa kuenda na kitabu ambacho kitaweza kuwasaidia kuanza mazungumzo na mwanamke. Lakini ubaya ni kuwa mazungumzo ni kama mawimbi ya bahari, hayatabiriki.

Unaweza kuanza na matamshi kama, “Nimekuona kwa mbali na nikaona uko na nishati ndani yako, mimi naitwa....” Unajitambulisha jina lako na pia yeye atakwambia jina lake. Halafu baada ya hapo bila wasiwasi unaanza kwa kumuuliza swali la ucheshi.

Kama umekutana naye katika supermarket unaweza ukasema, “So naona umekuja kuifilisi (taja sehemu mlipo) ama kama umekutana naye katika klabu unaweza kumwambia, “So naona umekuja kusajili wafuasi wapya kwa kanisa lenu, kweli?”

Hapa usijifanye mjanja. Haya ni baadhi tu ya maneno unaweza kutumia lakini si lazima uyatumie. Kuna maongezi tofauti tofauti unaweza anza nayo. [Soma: Hatua 5 tofauti za kupewa namba na mwanamke]

#5 Funga jamvi na ujiondoe.

La kufanya hapa ni kuwekeza kwa jambo ambalo litamfanya aone kuwa atakosa kitu pindi ambapo utajiondoa. Na mbinu nzuri hapa ni kumsoma na kujua mambo ambayo anayoyapenda.

Mfano umekutana naye katika kibanda cha filamu na series halafu unamwona anachagua collection flani halafu wewe utamwambia, “By the way kuna collection ya huyu msanii niko nayo lakini hata sijaiskiliza, maybe tunafaa tumeet tena unipe uhondo kwa nini unapenda kuskiliza nyimbo zake”

Ukiona macho yake wamemulika then uko kwa njia iliyo sahihi na umefanya kazi nzuri. Hakikisha ya kuwa anakupatia namba yake ya simu ili uweze kumpigia wakati mwingine. [Soma: Njia za kutongoza kwa kutumia macho]

Hapo ndio unafaulu kirahisi bila wasiwasi!

2 comments:

  1. Samahani hatuna. Lakini unaweza kujiunga na page yetu ya Facebook

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.