Jinsi Ya Kuyafanya Maongezi Yako Na Mwanamke Yawe Marefu


Je kuna kitu ambacho kinafurahisha zaidi (kando na kufanya mapenzi) ambacho kinasisimua zaidi kuliko kuwa na mazungumzo ya kufurahisha na mwanamke? Ok. unajua vile mazungumzo aina hii hutokea, wakati ambapo unayaona mazungumzo yako na mwanamke yanaenda na wimbi moja, unajihisi kana kwamba mko mkondo mmoja, na cha kufurahisha zaidi ni kuona ya kuwa mnamaliziana sentensi zenu bila wasiwasi halafu...


Ghafla inatokea situation ambayo kuna kuwa na kimya. Wakati ambapo umebakia unang'ang'ana angalau upate kitu cha kufanya maongezi yenu yarudie tena , kuna ile hisia ya pole pole inayokuja ambayo unajihisi kana kwamba unapoteza nafasi yako na mwanamke huyo kuendeleza matangamano yenu. Kibaya zaidi ni kuwa, kadri kimya kinapoendelea kuzidi...ndipo unazidi kuwa na mawazo ambayo hayana msingi ambayo unayajaribu kuyasema.

"So, anga ya leo unaionaje?" ama "leo kuna jua kali!" ni maneno ambayo unabakiwa nayo kuyasema ukijaribu angalau ufanye ukimya wenu upotee...

Well, kama umekuwa ukikumbwa na changamoto kama hizi wakati ambapo unajaribu kuongea na mwanamke... acha tuongee jinsi ya kuhakikisha ya kuwa unakwepa jangamizi hili wakati ambapo unakuwa na mwanamke.

1. Usipange kuhusu maongezi yako ya mbeleni sana... lakini...
Ingawa itakuwa ni jambo mwafaka la kupanga kitu cha kusema mbeleni wakati ambapo unakumbwa na hisia za shoto (awkward), hii inaweza kufanya kutangamana kwenu kuonekana shoto zaidi. Walakin kuna njia kadhaa ambazo unaweza kusema wakati ambapo unakumbwa na kimya kirefu. Maneno haya yatasaidia sana haswa wakati imetokea situation kama hii.

Hizi ni baadhi ya sentensi unaweza kutumia wakati kimya kimewajia ghafla katika maongezi yenu:

"Ushawahi kujiuliza ni kitu gani kinachofanya kimya kirefu kuleta hisia za shoto?"

Ukifikiria vizuri kuhusu hili swali, utaliona kuwa ni swali zuri ambalo linasisimua na ambalo linaweza kujenga maongezi marefu. Swali kama hili pia linakupa wewe nafasi ya kuweza kupata kuijua haiba ya mwanamke unayeongea naye.

"Ulikuwa wajua ni njia gani rahisi ya kuonyesha kuwa unamtambua na kumfahamu mtu flani? ---mpe nafasi akujibu--- "Wakati ambapo inatokea ukimya wenu mumeuzoea kuwa ni sehemu yenu ya mazungumzo.  Je, uligundua hilo?"

Hii tena inatoa nafasi kwako kupata kumwelewa zaidi mwanamke unayeongea naye na bila shaka inaweza kumfanya mwanamke kuvutiwa kwa mazungumzo ambayo utakuwa ukiyaendeleza. Kutumia mbinu hizi pia kunasaidia kufanya ukimya wenu kuonekana kama kitu ama jambo la kawaida bila kuleta  hisia za shoto. Hii ni kwa sababu mambo ambayo huonekana kama hayajazoeleka yakiwekwa wazi na kuzungumziwa kwayo inayafanya yaonekane kama mambo ya kawaida.

Hii ni kweli kwa sababu hisia za shoto ambazo zinajitokeza katika maongezi ni sawa na jambo lolote lile ambalo huonekana kama ni geni. Lakini pindi ambapo mtaamua kuweka wazi na kuliongea swala hilo, inatoa hisia zozote ambazo zinaweza kuharibu maongezi yenu.

NB: Anza mazoezi ya kutumia mbinu hii kwa kuwauliza marafiki zako na watu unaotangamana nao kabla ile siku ya kuanza kuongea na deti wako. [Soma: Mada ambazo zitaua upendo kwa mwanamke]

2. Mtie ufunguo yeye ndie awe anayeongea
Wanaume wamebarikiwa sana kwa kuwa wanawake ndio wamepewa talanta ya kuongea. So kwa mwanaume akicheza karata zake vizuri, hahitaji kufanya mengi ikija kwa maswala ya maongezi. Kile kinachohitajika ni kujua wakati na maswali ambayo unafaa kumuuliza mwanamke na kuwa msikilizi mzuri.

Ukiwa mbora zaidi wa kusikiliza anachosema ndipo unapomfanya azidi kuwa interested na kuongea na wewe. Pia utakuwa ukimfanya ajiskie huru kwako. Mwanzo iwapo utamfanya ajihisi yuko huru kwako utafanya maongezi yenu yawe marefu zaidi kuzidi yale ambayo ulikuwa ukiyatarajia.

Ufunguo hapa ni kujua jinsi ya kuyaandaa maswali yako kulingana na kitu ambacho anaongea. Kama anakuambia kuhusu kitu anachopenda, muulize kwa nini anakipenda. Kama ni kitu asichokipenda, muulize kwa nini hakipendi.

Kuuliza swali la 'kwa nini' huwa inasaidia sana kuingia katika mzizi wa haiba  yake na kutakufanya umuelewe kiundani zaidi kumhusu. Kadri unapozidi kufanya hivi, ndipo unazidi kumfanya afunguke na kuongea vitu zaidi ambavyo utakuwa na nafasi ya kuuliza maswali zaidi kwayo.

Kando na hio usijisahau ukaingia katika wingu la wanaume wengine wengi feki ambao hupenda kujibu maswali na neno moja. Ni muhimu kuhakikisha ya kuwa wakati ambapo yeye pia atakuuliza swali uhakikishe ya kuwa unafunguka na kuelezea kila kitu ambacho unaona kinafaa kwa yeye kujua.

Kawaida ni kuwa kadri unapofunguka kujieleza kwa mwingine, ndipo pia yeye anafunguka kukuelezea yake...na hii huchangia mazungumzo yenu kuwa wazi na marefu. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanamke umvutie]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.