Vitu Vya Kufanya Na Kuepuka Ikija Maswala Ya Kumtext Mwanamke


Katika ulimwengu wa sasa mawasiliano kupitia jumbe fupi unazidi kutumika kiasi cha kuwa mazungumzo baina ya watu yamejeuzwa kuwa meseji fupifupi. Kupewa namba kutoka kwa mwanamke ni nusu ya muelekeo wako wa kuuteka moyo wake. Lakini je wakati wa kumtext mwanamke je unatumia mbinu ipasayo?

1. Usichelewe kutext wakati amekupatia namba yake ya simu
Kuna baadhi waliobobea katika maswala ya kutumia text kumshawishi mwanamke watakwambia kuwa usichelewe kabisa kumtext mwanamke kwani ukizubaa na kumtext baada ya masiku atakupuuza, na wengine pia wanadai kuwa ni vizuri zaidi kuchukua muda wako kama siku hivi ili mwanamke asikuone kama unambabaikia kupindukia. Kimaoni yangu ni kuwa haufai kupitisha wala kupunguza masaa 24 toka wakati amekupatia namba yake ya simu. Masaa 24 si muda mrefu wala mfupi kwani utakuwa na muda wa kutosha na kujiandaa ili kuweza kujipanga. Hivyo basi haufai kumtext papo hapo ama kuchukua masiku kabla hujamtumia jumbe. [soma: Jinsi ya kumshawishi mwanamke mtandaoni]

2. Tumia mistari ya ucheshi
Kulingana na utafiti uliofanywa ni kuwa asilimia 25 ya wanawake watakataa kujibu texts zako kama hazina chembechembe ya ucheshi ndani yake. Owk huu ni uchoyo wa hali ya juu lakini utafanyaje? Hii ndio dunia ya sasa kama huna mshiko utabakia hivyo hivyo. Hivyo ni lazima kama huna uzoefu wa kuwa mcheshi gurudumu ni lako la kuhakikisha kuwa haujatengwa na mwanamke unayemzimia.
Pia unafaa kukumbuka kuwa wanawake warembo wanatumiwa text na majamaa wengine wengi wote wakipigania nafasi io hio ambayo unaitaka hivyo wakati unapomtumia text hakikisha ya kuwa unakuwa mbunifu tofauti kabisa na mwanamume yeyote yule. Acha kutumia maneno ambayo yamerudiliwarudiliwa.

KUMBUKA: Wakati unapomtext mwanamke unayemtongoza hakikisha hautumii maneno ambayo yatakuwa mtego kwako yenye yatakufanya uwekwe katika friend zone. Kama unataka utoke naye date, jaribu kutumia maneno ya mzunguko ambayo mwishowe yataingiliana kwa nyote mkutane. Mfano unaweza kumuuliza kama ashawahi kwenda katika hoteli ama kilabu flani, akijibu bado hajawahi chukua hio nafasi ya kumuuliza kama angependa kuenda sehemu kama hio. Hii ni baadhi ya njia rahizi ya kutumia kumshawishi.


1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.