Ishara 12 Za Kuonyesha Kuwa Umefall Na Mwanamke Bila Kujua


Wakati mwingine huwa tunapenda kusema kuwa tunajua kila kitu, lakini pia kuna wakati unaweza kupitwa na jambo flani bila wewe kujua.


Katika mahusiano, unaweza ukawa na rafiki yako wa karibu ambaye umezoeana kiasi cha kuwa unamwona kama ndugu yako. Lakini pia kwa upande mwingine mwili wako unajaribu kukupa ishara za kuonyesha kuwa kando na kuwa ni rafiki yako wa dhati, kuna swala la mapenzi ambalo linajitokeza.

Well, leo tumekuja na ishara 12 ambazo zitakuonyesha kuwa umefall na mwanamke bila wewe hata kujua. Ishara zenyewe ni kama zifuatazo.

#1 Yeye ndiye wa kwanza kumpa habari nzuri.
Kabla hujafall na yeye, ulikuwa unawasiliana na rafiki yako, ndugu yako ama wazazi wako kuwapatia habari nzuri. Labda umepewa cheo kazini, ama umeshinda kamari nk.

Lakini sahizi ghafla umebadilisha mtindo. Yule ambaye unataka kuwasiliana naye wa kwanza ni huyu mwanamke. Habari yeyote ile nzuri unataka yeye awe wa kwanza kujua.

#2 Unataka akutane na familia yako.
Kama uko karibu na familia yako, ungetaka ufanye bidii umtambulishe kwenu. Hii ni ishara nyingine muhimu ambayo inaashiria kuwa umeanza kufall na huyu mwanamke. Pia kama haitawezekana umtambulishe kwa familia yako, ungetamani akutambulishe kwenu. [Soma: Hatua za kumuaproach mwanamke wakati wowote]

#3 Unakuwa na hisia za ulevi.
Mapenzi yanakuwa na hisia ambazo zinaweza kufananishwa na hisia ambazo hutokana na dawa za kulevya. Ndio maana wazungu husema love is like a drug. Hivyo ukiwa na huyu mwanamke kisha unajihisi raha ambayo haisemezeki utamu wake, basi hio ni ishara kuu kuonyesha kuwa umefall na huyu mwanamke.

#4 Uko muwazi zaidi.
Kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huwa kunakufanya uwe na mawazo tofauti. Mara nyingi utajipata unajaribu kumtunza mwanamke zaidi na kutaka kujua maoni yake.

Hivyo mtu akiwa amefall na mwanamke huwa anakuwa na uwazi fulani, unaweza kuanza kuangalia filamu ambazo amezipendekeza, kuonja chakula chake ambacho hujakizoea, kukubaliana na yeye katika maswala ya kisiasa ama kidini. Ukiona umeanza kukubaliana na mambo kama haya, basi ujue upendo upo kati yenu.

#5 Watu wengine wanakuona uking’aa.
Jambo jingine ambalo ni ishara ya kuwa umefall na mwanamke ni pale ambapo rafiki zako na familia yako wameanza kuona utofauti ndani yako. Mtu akiwa anapenda anakuwa tofauti. Kwanza ni kuwa anakuwa anatabasamu, anakuwa mchangamfu, anapoteza atenshen kwa uharaka na mambo yote ambayo ni chanya katika maisha. [Soma: Ishara za kumtambua mwanamke mwenye uchu]

#6 Unajali kile ambacho anahisi.
Kama unampenda mwanamke, kwa kawaida utakuwa na hisia za kujali kwa kila kitu ambacho atapitia. Ukiona amekasirika utajaribu kumfurahisha, ukiona anatatizika utamsaidia nk. Hii  piahuja moja kwa moja pindi ambapo umeanza kufall na mwanamke.

#7 Unapunguza uchoyo.
Wakati unadeti na mwanamke ama kumtoa out, huwa kwa kawaida unaenda na programu zako. Kwa mfano ukiwa na shughli wikendi basi unaweza kukatiza deti hio. Lakini pindi ukiwa umefall na yeye, kando na kuwa utakuwa unakuwa wa kwanza kuwasili kwa deti, utakuwa pia unamletea zawadi kama maua ukikutana naye.

#8 Unamfikiria kama hayuko na wewe.
Binadamu kwa mara nyingi akiwa na shughli zake za kila siku, akili yake inamakinika kushughulikia maswala yake. Mfano akiwa kazini atakuwa anafikiria jinsi ya kutimiza kazi yake vizuri ama akiwa shuleni atakuwa anafikiria kazi zake za ziada. Lakini pindi ukiona kuwa mara kwa mara akili yako inamfikiria mwanamke huyu basi jua umeanza kufall na yeye.

#9 Kila kitu kinakukumbusha yeye.
Ishara nyingine kuonyesha kuwa umefall na yeye ni kuona kila kitu kinakukumbusha yeye. Ukienda katika supermarket unamkumbukaa, ukishika simu unamkumbuka, ukiangalia chochote unauona uwepo wake. Hapo ni ishara kuwa umefall na yeye. [Soma: Maswali 33 ya kumuuliza mwanamke unapokutana naye mara ya kwanza]

#10 Unataka kuongea kumhusu.
Ukiwa unakuwa na haja ya kuingiza jina la mwanamke huyu katika mazungumzo yako basi hii ni ishara moja wapo ambayo inaashiria kuwa umefall. Inaweza kuwa unaongea na mtu katika mkahawa kisha ukaona haja ya kumtaja mwanamke huyu katika mazungumzo yenu.

#11 Unaingia na mawazo ya kuwa unataka kuwa na yeye maisha ya usoni.
Ishara nyingine ya kuonyesha kuwa umefall na mwanamke ni pale ambapo unaingiwa na matamanio ya kuwa na yeye katika maisha yako ya usoni. Hii ni ishara ambayo iko wazi kuwa uko tayari kuchumbiana na mwanamke huyu na unataka awe na wewe maishani mwako.

#12 Unaogopa.
Hii ndio humaliza mchezo. Wanaume wengi ambao wanatufuata inbox huwa mara nyingi wanatuambia kuwa wanakuwa na uoga wa kuaproach mwanamke flani ili amweleze yaliyo moyoni mwao. Na sisi huwa tunawajibu wajizoeshe kutangamana na kuwasiliana na wanawake waliowazoea. Na kweli wakiwa wanaongea na wanawake hawa huwa hawana uoga wowote. Uoga unakuja pindi tu pale ambapo anataka kuwasiliana na mwanamke ambaye amefall na yeye. [Soma: Mambo ya kimsingi ya kuzingatia unapotongoza mwanamke katika kikundi]


Upo! Hizi ndizo ishara kuu kuonyesha kuwa umefall na mwanamke. So ukiona una ishara kama hizi, usiwe na wasiwasi, funguka umwambie mwanamke huyu kuwa unampenda.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.