Kupata Ujauzito, Ishara 7 Za Kuonyesha Una Mimba


Kupata ujauzito ni hali ambayo wanawake wengi hutarajia siku moja katika maisha yao. Ujauzito unatambulika kuwa ni ishara moja ambayo mwanamke anajeuka na kuitwa mama. So utajuaje kama wewe ni mjamzito?

Kawaida kuna ishara ambazo huchochea kiasi cha kumfanya mtu aanze kujishuku na kujiuliza maswali ya iwapo amepata mimba au la. Kuna mambo ambayo huchangia hadi mtu apate ujauzito, nayo ni:

  1. Umefanya mapenzi bila ya kutumia kinga
  2. Kondomu uliyokuwa ukiitumia imepasuka
  3. Unatumia dawa za kujikinga kushika mimba lakini ulisahau kumeza
  4. Umemeza dawa ya kuzuia mimba lakini pia unatumia antibiotics
  5. Umemeza dawa ya kuzuia mimba lakini ulitapika ama kuharisha ndani ya masaa manne.
Kama upo katika mojawapo ya hali ambazo tumeziweka hapo juu, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwa umepata ujauzito.

Kutambua kama una ujauzito, tumeweka ishara zifuatazo ili uangalie kwa kina ili uweze kujipanga kabisa jinsi ambavyo utaendelea kuishi katika nyakati ambazo utakuwa unabeba mimba yako. Zama nasi.

#1 Kukosa hedhi

Kukosa kuingia kwa siku zako ni ishara kuu ya kuonyesha kuwa una uwezekano wa kuwa umepata ujauzito. Hii ni sababu wakati mtu anapobeba mimba, kawaida hedhi zake husimama hadi ule wakati ambapo atajifungua. Hivyo kama umepitisha zaidi ya mwezi bila ya kuona siku zako basi uwezekano wa ujauzito uko juu sana.

#2 Kichefuchefu na kutapika

Hii mara nyingi huonekana nyakati za asubuhi. Pia huonekana siku za mwanzo wa ujauzito. Wanawake wengi wakiingia katika ujauzito huwa na dalili za kutapika mara kwa mara pasi na kuwa wagonjwa. Hali hii inatambulika na wanawake wengi wakati wanapotaka kutambua iwapo ni wajawazito au la.

#3 Matiti ama chuchu kuwa kubwa

Ishara nyingine muhimu ya kutambua iwapo mwanamke ni mjamzito ni kuangalia matiti yake. Kawaida, mwanamke anayebeba mimba matiti yake huwa makubwa ili kuyaandaa kutengeneza maziwa ya mtoto mtarajiwa. Hivyo hii ni moja wapo ya ishara ya kuangalia kwa makini.

#4 Uchovu

Mwanamke pia huwa na uchovu ambao si wa kawaida wakati ambao ni mjamzito. Uchovu huu huletwa pasipo na kufanya shughuli zozote za maana. Hivyo ukiona ya kwamba kila wakati unahisi uchovu ama kuchoka basi unafaa ujichunguze kwa kina.

#5 Kuumwa na kichwa

Wanawake wengine ambao hupata ujauzito pia huweza kujikuta katika hali ya kuumwa na kichwa mara kwa mara. 

#6 Hamu ya kula sana

Ishara nyingine ambayo inaweza kudhihirisha kuwa umekuwa mjamzito ni hamu ya kula. Wanawake wajawazito wanaweza kuwa na hamu ya kupenda vyakula aina aina na pia kupenda kula sana. Hii ni kwa sababu mwili wako umebadilika na unakuwa kwa kasi hivyo inahitaji virutubisho kwa wingi.

#7 Kukojoa mara kwa mara

Ishara nyingine ambayo inaweza kuonyesha ya kuwa umekuwa mjamzito ni wakati ambapo mtu anakuwa na mikojo mingi kwa kibofu chake. Hii husababisha kwa mwanamke kukojoa mara kwa mara ili kupunguza mkazo ambao anakuwa nao.

Ok. Hizi ni baadhi tu ya ishara ambazo zinaweza kudhihirisha kuwa una ujauzito, lakini pia baadhi ya ishara hizi kuweza kuhusishwa na mzunguko wa hedhi. Cha muhimu ni kuhakikisha ya kuwa unatembelea kituo cha afya ili uweze kujua hali yako kamili



1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.