Jinsi Ya Kumpata Mwanamke Na Mbinu Kumi Za Uhakika


Kujua jinsi ya kumuwin mwanamke si jambo gumu – haswa kama unazijua mbinu za nguvu za kisaikolojia ambazo unaweza kuzitumia kwa mwanamke.


Wanaume wengi wanataka kujua jinsi ya kuwin mioyo ya wanawake na kutaka kujua jinsi ya kuweza kutoka deti na wao. Well, ijapokuwa inaweza kuonekana kuwa jambo gumu, mbinu hizi si ngumu hata kidogo. Mwanzo kama unataka kujua jinsi ya kuwin moyo wa mwanamke kirahisi, basi unapaswa kusoma mbinu kumi ambazo tumeziorodhesha na ambazo hufanya kazi kila wakati.

#1 Approach vile inavyotakikana
Kama unataka kujua jinsi ya kuwin moyo wa mwanamke, kile unachohitajika kufanya ni ufanye mambo ya kibusara tangu mwanzoni. Kufanya mambo yawe rahisi na haraka kwako: weka kwa akili yako kuwa siri ya jinsi ya kumvutia mwanamke yeyote huwa iko kwa dhana anaiyoiweka kuhusu thamana yako kwa akili yake. Kwa urahisi ni kuwa unapaswa kumuonyesha mwanamke kuwa una thamana ya yeye kuweza kuspend muda wake na wewe, na ni yeye ndiye anafaa akuwin na wala si kivingine. Yaani mwanamke anapaswa kukuona kuwa yeye anapaswa kuwa na wewe.

#2 Kuwa tuzo kwa macho yake
Kama tulivyoeleza hapo juu ni kuwa njia rahisi ya kumuwin mwanamke ni kwa kumuonyesha kuwa wewe ni kama tuzo ambalo anapaswa kulishinda na kuwa wewe ni mwanaume ambaye anapaswa kupiganiwa. Kama huelewi hii inamaanisha nini hebu uchukulie huu mfano: kila mtu anajuwa kuwa wanawake wanajichukulia kuwa wao ndio kila kitu ikija kwa maswala ya kutongoza, yaani wao ndio wanaobabaikiwa. Wanajua kuwa pia wanaume kimsingi huwa wanawafukuzia wanawake, ukweli? Well, kama wewe ni mjanja basi unapaswa kufanya kinyume cha haya yote.

Kwa njia nyingine, namaanisha kuwa unapaswa kujeuza akili ya mwanamke unayempenda na kumfanya kuona kuwa ni yeye ndiye anayepaswa kukufukuzia. [Soma: Mfanye mwanamke akufukuzie]

Pia unapaswa kumfanya aamini ya kuwa kukupoteza wewe itakuwa ni jambo baya zaidi ambalo atakuwa amefanya katika maisha yake. Hii itahakikisha kuwa hataweza kupoteza interest kwako na atafanya kila kitu kuhakikisha kuwa anakuweka kando yake katika maisha yake.

#3 Ipandishe hadhi yako
Kama unataka kujua jinsi ya kuwashawishi wanawake, unapaswa pia kuipandisha hadhi yako kiujumla mbele za wanawake. Na kwa kuanzia, mwonyeshe kuwa wewe si mwanaume wa tamaa wala mhitaji na hujali iwapo atakukubali au atakukataa. Hii mbinu kiuhakika itamshika kwa mataa kwa kuwa wanaume wengi huwa wanawaangukia wanawake ili kupata atenshen kutoka kwao (wanawake wengi  huwa wanakuwa na mkono wa mbele ikija kwa maswala kama haya.) So, kwa kuchukua hatua ya nyuma, utakuwa unamwonyesha ya kuwa wewe huna tabia kama hio na hii inamfanya kutaka kujua kwa nini wewe ni tofauti na wengine. [Soma: Jinsi ya kuipandisha hadhi yako mbele ya wanawake]

#4 Jenga nguzo na yeye
Njia nyingine ya uhakiki ambayo itaweza kumuwin mwanamke ni kwa kujenga nguzo na yeye. Kimsingi, hapa unaanza kwa kumfanya ajihisi huru na uwepo wako kwa kutumia sanaa za maongezi ya kutongoza. Kwa kufanya hivi, chagua mada ambazo zinamvutia wakati unaongea na yeye na pia hakikisha ya kuwa unampa atenshen zote wakati anapoongea.

Pindi atakapojiskia huru na wewe, unaweza kuanza kujenga mavutio kwa kuanza kumtesa na kumtania mara kwa mara. Lakini, hakikisha kuwa haumuonyeshi kuwa unataka kuwin woyo wake. Mwanzo, itakuwa vizuri zaidi kama utajivuta kwake halafu mwishoni unajitoa mbali na yeye ili uweze kuleta attraction zaidi kati yenu.

#5 Mwonyeshe kuwa unamheshimu
Kama lengo lako kutaka kujua jinsi ya kumuwin mwanamke ni uweze tu kulala na yeye, basi atajua kile ambacho unataka kutimiza kwake na utamfanya akutenge kama jinamizi. Kwa sababu ya hili, unapaswa kumuonyesha kuwa unamheshimu, kivyovyote vile. Kwa lengo lolote lile ambalo unataka kutoka kwa huyo mwanamke, kumheshimu mwanamke kutakufanya uongeze nafasi yako ya kuwin moyo wake mwishoni.

Hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kuonekana kama mtu anayeitikia kila kitu kutoka kwake. La. Unapaswa kujua mbinu ya kumtawala pia – kuwa kiongozi na mwenye kudhibiti.

#6 Mwonyeshe kuwa unajali
Kando na kuwa unamheshimu, wanawake wote huwa wanataka kujaliwa. So kabla ya kutarajia mwanamke akuangukie, unapaswa kumuonyesha kuwa unahisia kwake kwa kuonyesha kuwa wewe ni kiongozi na kuwa wewe ndie unayetawala mahusiano yenu. Kama hutafanya hivi, mwanamke wa ndoto yako hataona umuhimu wa kutoka deti na wewe na hatoona shida ya kuwa na mwingine.

ONYO: Tahadhari usivuke mipaka ya kumuonyesha mwanamke kuwa unamjali sana kwa kuwa anaweza kukuingiza katika ile himaya ya kuwa rafiki yake.

#7 Jiamini
Wanaume wengi wanapata ugumu wa kuelewa jinsi ya kumuwin mwanamke na kumwambia kuwa wanampenda. Well, unapaswa kuhakikisha ya kuwa hautamwambia ya moyoni mwako mpaka ule wakati ambao utakuwa confident ndani yako. Huwa kawaida ni hivi, wanawake wanaweza kujua iwapo uko confident au la, na unaweza kupoteza nafasi ya kumuwin mwanammke kama huyu iwapo utaharibu kila kitu kwa kumuonyesha kuwa unashindwa kujiamini ndani yako. [Soma: Jinsi ya kujiamini mbele za wanawake]

#8 Simama kati ya wote
Njia nzuri zaidi ya kuchagua wanawake ni kwa kusimama kati ya wote, Mwanzo, kusimama kati ya wote kunaweza kukufanya umuwin mwanamke haraka sana kwa sababu ndoto za wanawake ni kuwa na mwanaume ambaye ni tofauti na wale wengine. So, kama utamwonyesha talanta yako ambayo hakuna mwingine ambae anayo na akaipenda, unaweza kumfanya akuone kuwa wewe ni spesho na kukupenda mara moja.

Labda inaweza kuwa talanta ya kuimba ama labda talanta ya michezo, chochote kile kitasaidia kukutofautisha na wanaume wengine. Unajua kupiga gita ama uko sawa kucheza pepeta? Mwonyeshe!

#9 Kuwa tofauti
Kwa kuendeleza hapo juu, unaweza kutumia hulka yako kuweza kumuwin mwanamke. Kwa kueleza kiurahisi, kuwa na hulka ambayo ni tofauti na mwingine yeyote yule – kuwa na maoni tofauti na ya wale wengine kutakufanya uonekane mtofauti. Njia hii kutamfanya mwanamke kuangalia na kuchagua tabia ambazo ni tofauti na zile za wanaume wa kikawaida. Mara nyingi wanawake waliokomaa kiakili huwa wanawapenda wanaume ambao wako tofauti na wengine.

#10 Badilisha mtizamo wako
Kama unataka kujua jinsi wa kuwin moyo wa mwanamke, basi unahitajika kubadilisha akili yako kabisa – hii ni kuanzia tabia yako, dhana na fikra zako. Pindi utakapofanya hivi, utakuwa na uhakika wa kuwa utawin moyo wa mwanamke wa ndoto yako haraka sana. Njia rahisi ya kubadilisha akili yako ni kujua kuwa kuna myanya mingi unayoweza kuitumia kumuwin mwanamke.

2 comments:

 1. Hey I am so thrilled I found your website, I really found you by
  mistake, while I was researching on Bing for something else, Anyways I am here now and would just like to say
  kudos for a incredible post and a all round exciting
  blog (I also love the theme/design), I don't have time to look over
  it all at the minute but I have book-marked it and also added your RSS feeds, so when I have time I will be back to read a lot more, Please
  do keep up the great work.

  ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.