Wakati Upi Mzuri Wa Kumwambia Mwanamke Awe Mpenzi wako?


Kuchukua hatua ya mbele katika mahusiano ni jambo la kutia wasiwasi na woga lakini wasiwasi huo utakutoka pindi ambapo utafahamu wakati mwafaka wa kumwambia mwanamke kuwa mpenzi wako.

Ni jambo zuri la kuchukua kumwambia mwanamke awe mpenzi wako. Hongera kwako kwa kuwa hii ni hatua muhimu katika kukuza mahusiano yako katika maisha.


Kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla kumwambia mwanamke awe mpenzi wako nayo ni kama yafuatayo.

#1 Umuhimu wa kuwa na mpenzi
Kabla ya kuchukua hatua ya kumwambia mwanamke awe mpenzi wako lazima kwanza ujue maana ya kuwa na mpenzi. Lazima ufahamu umuhimu wa kuwa na mpenzi. Usirukie kutafuta mpenzi kwa sababu ya presha kutoka kwa marafiki zako ama kutaka kupokea sifa kutoka kwa watu. Kuwa katika mahusiano kuna majukumu. Halikadhalika kuwa na mpenzi kunahitaji majukumu kadha wa kadha. [Soma: Hatua muhimu za kupata mwanamke]

#2 Lengo la kuwa na mpenzi
Jambo jingine muhimu la kuzingatia kabla ya kumwambia mwanamke awe mpenzi wako ni kujua lengo lake. Je mwanamke huyu utakuwa naye kwa nia gani? Je, unataka awe mpenzi wa kupoteza wakati tu ama atakuwa mpenzi wa muda ama ni mpenzi ambaye atakuwa wa ndoa.
Jambo hili lazima liwe kwa akili yako. Pindi utakapojua lengo lako basi unaruhusa ya kumwambia awe mpenzi wako. Usifanye kosa la kuingia katika mahusiano na mwanamke bila ya kujua lengo lako.

#3 Je, uko tayari kumwambia awe mpenzi wako?
Kumwambia mwanamke awe mpenzi wako ni rahisi. Lakini kumfanya akukubali ndilo tatizo. Hivyo kila kitu kinakuwa na muda wake maalum. Hauwezi kukutana na mwanamke siku ya kwanza kisha umwambie kuwa unataka awe mpenzi wako. Pia hauwezi kukaa miaka mitano na mwanamke kisha umwambie unataka awe mpenzi wako. Kila kitu kina kuwa na timing yake mahususi. [Soma: Jinsi ya kuishi maisha marefu katika mahusiano]


#4 Wakati wa kumwambia awe mpenzi wako.
Kama nilivyotangulia kusema awali, hakuna wakati mahususi wa kumwambia mwanamke awe mpenzi wako, lakini kile ambacho unapaswa kujua ni vizuri kama utamwambia mwanamke awe mpenzi wako wakati ambapo ameanza kuonyesha ishara za kuwa anakupenda.

Wakati huu utautambua pale ambapo mumetoka deti mara kadhaa, anapenda kuspend wakati mwingi na wewe na labda mshajuana kwa undani.

#5 Jinsi ya kumwambia awe mpenzi wako.
Kwa kuwa mshazoeana na mnajuana vizuri, huu ndio wakati mzuri wa kumwambia kuwa unataka awe mpenzi wako. Unaweza kumpeleka sehemu ambayo anapenda kutembelea kisha ukamfungukia kuwa unampenda. Ama unaweza kuenda faraghani mkiwa nyinyi wawili pekeenu kisha ukamwelezea kuwa unataka awe mpenzi wako. [Soma: Jinsi ya kupata mpenzi chini ya siku 30]

Hizi ndizo hatua za kufuata ili uweze kumwambia mwanamke awe mpenzi wako. Lakini jambo muhimu ambalo unafaa kuzingatia ni wakati maalum. Ukipitisha muda mwanamke anaweza kukujeuza rafiki yake na atakuweka katika himaya ya urafiki (friend zone) na itakuwa vigumu kwako kujinasua.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.