Je, Niachane Na Mpenzi Wangu? Ishara 9 Za Kutambua Kama Wakati Wako Umefika Kuachana Naye


Kuwa katika mahusiano si rahisi. Kawaida inahitaji uwe na moyo wa kuvumilia. Lakini kuvumilia huku kuna kipimo chache ambacho hupaswi kukipita.

Ukiingia katika mahusiano kuna mambo mawili makuu ambayo mtu anapaswa kuzingatia. Kwanza lazima ajue mahusiano hayo lengo lake ni gani. Pili ni lazima utambue na ujue jinsi ya kujipanga katika mahusiano hayo.


Lakini mara nyingi utapata mtu ameingia katika mahusiano bila mpangilio wowote wa maana. Yeye kwa kuwa amependa basi anaona ni sawa kuingia katika mahusiano.

Hivyo inafikia mahali anapata mahusiano aliyoyaingia hayafanyi kazi kama alivyotarajia, mwisho anajikuta kwa njia panda.

Well, hapa Nesi Mapenzi hatungependa kuona mambo yafikie hapo, hivyo leo tumeleta ishara kukueleza ni wakati gani bora wa kuachana ama kukatiza mahusiano yako na mpenzi wako.

Zama nasi!

#1 Mahitaji yako hayatimizwi.
Kila mtu huwa na malengo yake katika mahusiano. Wengine wanaweza kuwa wanataka mahusiano yaendelee hadi ndoa, wengine wanataka kutimiziwa kifedha ama chochote kile. Ukiona mahusiano yenu hayafikii pale yanatakikana basi fahamu mahusiano hayo yamefika ukingoni.

#2 Unaogopa kuongea na mpenzi wako
Kwa njia yeyote ile, kama unashindwa kuongea na mpenzi wako basi mahusiano yenu hayana umuhimu wa kuendelea zaidi. Nguzo kuu katika mahusiano ni mawasiliano. Iwapo hakuna mawasiliano kati yako na mpenzi wako basi uhusiano huo umefika mwisho. [Soma: Tambua kama mpenzi wako anakucheat na mwingine]

#3 Unaenda kwa wengine ili uweze kutimiziwa mahitaji yako
Kwa kuwa tayari mpenzi wako anashindwa kutimiza mahitaji yako, lile ambalo unabaki nalo ni kuenda kwa marafiki zako kupata msaada. Ukiona umefika hatua hii, basi fahamu ya kuwa mahusiano yenu yamefika mwisho.

#4 Hisia zako zinakwambia uachane na yeye
Hisia kama hizi kawaida humjia mtu. Unapata katika mawazo yako umechoka na mahusiano ambayo uliopo. Mara nyingi hisia hizi huwa ni za kweli kwa kuwa umechunguza na kuona ya kuwa mahusiano yenu yamefifia.

#5 Mpenzi wako anakunyanyasa.
Ukiona wakati wowote mpenzi wako anakutukana, anakupigia kelele na mwisho kukupiga, basi unafaa uachane naye mara moja kwa kuwa mahusiano yenu hayatafikia mbali. Mbaya zaidi anaweza kukudhuru kimawazo ama hata kimwili. [Soma: Ni wakati upi mzuri wa kumwambia awe mpenzi wako?]

#6 Marafiki zako na familia yako hawatoi sapoti katika mahusiano yenu.
Mahusiano bora ni yale ambayo yamekubalika na kila mtu. Familia yako na marafiki zako wanakubaliana na mahusiano hayo. Lakini ukiona wote, ikiwemo marafiki zako hawapendi mahusiano yenu, bila shaka itakubidi utathmini tena mahusiano yenu.

#7 Haumpendi mpenzi wako
Hali kama hii bado hutokea katika mahusiano. Unapata mmoja wa wapenzi wawili yuko katika mahusiano lakini hampendi mpenzi wake. Hatua kama hii ni ishara ya kuwa imefika wakati wa kuachana. Mahusiano na mapenzi huenda sambamba.

#8 Hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako.
Ukifikia kitengo cha kuwa unashindwa kufanya mapenzi na mpenzi wako bila sababu yeyote, basi ni wakati mzuri wa kuachana naye. Mara nyingi ukiona unashindwa kufanya mapenzi na mpenzi wako ni kuwa umechoshwa na yeye, ama tabia zake, ama maamuzi yako tu. [Sababu kuu za kumfanya rafiki yako awe mpenzi wako]

#9 Umechoshwa na kila kitu
Hii ndio ile hatua ya mwisho ambayo huwa ishara kuu ya kutambua kama wakati wako wa kuachana na mpenzi wako umewadia. Hatua hii ni pale unachukizwa hata kuuona uwepo wake.

Ok. Hizi ni baadhi  ya ishara muhimu ambazo huonyesha kama wakati wa kuachana na mpenzi wako umewadia. Usijiingize katika mahusiano ambayo hayana manufaa kwako.

Pia fahamu ya kuwa haimaanishi kuwa ukiwa una ishara moja katika hizi basi uachane na mpenzi wako, la. Kuachana na mpenzi wako ni mchakato mkubwa ambao unafaa ufuatwe na umakini. Usiharakishe kuachana na mpenzi wako kwa makosa madogo madogo. [Hatua 8 mtu hupitia baada ya kuachwa na mpenzi wake]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.