Ujuzi 10 Wa Kutongoza Mwanamke Ambao Unapaswa Kujua Kabla Valentine Kufika


Kuna ujuzi ambao kila mwanaume anapaswa kujua ikija katika maswala ya kutongoza mwanamke. Na huu ujuzi ndio ambao unahitajika kila wakati ambapo utaanza approach kwa mwanamke. Ujuzi huu wa kutongoza huanzia kwa kujua kumwangalia kwa macho, kutabasamu, kuapproach, kuongea, kuomba namba hadi kutoka deti. Mbinu hizi ni lazima mwanaume awe na uwezo wa kuzikamilisha bila tashwishi wowote.


Somo la leo tutawafundisha ujuzi huu wa kutongoza ambao unapaswa kuujua kabla siku ya Valentine kufika. So tuanze na wapi?

Zama nasi.

#1 Hauwezi muwini mwanamke kama hautaucheza mchezo.

Wanaume wengi wanakuwa na uoga wa kuaproach mwanamke. Wanaogopa ya kuwa wakiaproach mwanamke watakataliwa ama mbaya zaidi waingiwe na kigugumizi kisichokuwa na mwisho pindi watakapomtokea mwanamke. Uoga huu ndio unawafanya wengi wasichukue hatua ya kuaproach mwanamke.

Kile wanachokisahau ni kuwa uko na asilimia hamsini ya kukubaliwa kama utamuaproach mwanamke, lakini utakuwa na asilimia mia ya kumkosa mwanamke iwapo hutachukua hatua ya kumuaproach mwanamke. So kuaproach mwanamke ni lazima kama unataka kufanikiwa. Usitarajie mwanamke akuaproach wewe.

#2 Mtizamo wa macho.

Njia rahisi ya kuteka atenshen ya mwanamke na kutaka kujua kama yuko interested na wewe ni kwa kupitia njia ya macho. Tumia sanaa za kutongoza kwa kutumia macho. Usimwangalie sana asije akakuona kama fala. Kuna mbinu mwafaka ambazo unafaa kufuata wakati ambapo unatumia macho kuiteka atenshen ya mwanamke. [Soma: Mbinu za kutumia macho kuteka atenshen ya mwanamke]

#3 Ustadi wa kutabasamu.

Jambo jingine ambalo lazima ujue ni kutabasamu. Wanaume wengine wanakuwa na tabasamu bora natural kama vile Vin Diesel ama Christiano Ronaldo. So ukiona tabasamu lako unaliona halivutii, unaweza kufanya mazoezi kwa kioo ujifunze kutabasamu. Yaani itakubidi uige hadi ikuige. Hakuna cha kubahatisha. Kusmile kunaweza kuwa tofauti tofauti. Kuna kule kutabasamu kiaibu, kujiamini, kutoeleweka nk. Mwisho wa siku tafuta tabasamu ambalo linawiana na hulka yako.

#4 Approach yako.

Baada ya kutumia macho yako na kujua kama yuko interested, unachohitajika kufanya ni kuanza approach kwake. Usipanic, ni kitu cha dakika moja. Unaenda hadi pale alipo. Usiingiwe na uoga kama atakukataa ama atakupigia kelele. Kwa akili yako unapaswa kufahamu ya kuwa una asilimia hamsini ya kuweza kumuwini huyu mwanamke bila wasiwasi wowote. [Soma: Jinsi ya kuapproach mwanamke]

#5 Jifunze kuskiliza.

Swala jingine ambalo unahitajika kujifunza ni kuwa wakati unaongea na mwanamke, lazima ujue kusikiliza. Hii ni muhimu kwa kuwa wanawake hupenda kusikilizwa. Wao hupenda kuona watu wakiwasikiliza. Hii inasaidia kwa kuwa hujenga mazungumzo kuwa marefu. Kutokana na kumsikiliza, utapata maswali kadha wa kadha ambayo utaweza kumuuliza kwayo.

#6 Songea na umshike.

Kivyovyote vile lazima umshike huyu mwanamke. Mbinu hii lazima uilete kwa njia ambayo hataigundua kirahisi na pia usionekane fala. Unaweza kumuuliza kuhusiana na bangili aliyoivaa mkononi aliinunua wapi, halafu kwa kumuuliza hivyo unaushika mkono wake huku ukiangalia na kuilisha mikono yako kwake. Mbinu ni nyingi. Tafuta moja nzuri ambayo unaweza ukaitumia. [Soma: Jinsi ya kumgusa mwanamke na asione tatizo]

#7 Mwonyeshe kuwa una interest naye.

Hapa ndipo wanaume wengi wanakosea. Wanasahau kuonyesha interest kwa mwanamke wanapokuwa wanaongea. Hapa unachohitajika kufanya ni kumsikiliza, kumuangalia machoni, na wala usimkatize wakati anapokuwa anaongea. Usiangalie simu, tv ama watu wengine wakati mnaongea. Hakikisha unamakinika na yeye

#8 Usisahau mizaha.

Kuingisha ucheshi ndani ya mazungumzo ni muhimu kwa kuwa mazungumzo yenu yatakuwa na nakshi ya mvuto. Mizaha yako iwe ile ya kawaida. Usianze ile ya sijui mama yako nk, wewe jaribu ile mizaha ya kawaida tu. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke acheke]

#9 Chukua namba.

Mazungumzo yenu hayapaswi kuisha na hapo, lazima yaelendee baadae. Hivyo lazima uchukue namba kutoka kwa mwanamke huyu. Ushapu na ujanja wako ndio utakuwezesha wewe kutoka na namba yake ya simu. [Soma: Mbinu tofauti za kumuomba mwanamke namba ya simu]

#10 Mtoe deti.

Hii ndio siku ambayo utakuwa unaitarajia. Wanawake wengi wanatamani kutoka deti siku ya Valentine, hivyo ni rahisi kwake kuitikia mwito wako. Muulize iwapo siku hio atakuwa na mipango gani. Kwa kuwa tayari ushamvutia na maneno yako, atakwambia ataispendi nyumbani pekeake. So wewe hapo ndio unaingilia kati na kumwambia mtoke deti pamoja. [Soma: Jinsi ya kumuuliza mwanamke atoke deti na wewe]

Well. Huu ndio ujuzi ambao unapaswa kuwa nao iwapo unataka kufanikiwa kila wakati unapoaproach mwanamke. Mafanikio kwako!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.