Sababu Zinazomfanya Girlfriend Wako Atongoze Wanaume Wengine


Wanawake wengine washawahi kufumaniwa na wanaume wengine. Hili ni jambo ambalo hutokea mara kwa mara katika maisha yetu. Utakuta mwanamke amefumaniwa na mwanaume mwingine. Mbaya zaidi unagundua kuwa huyu mwanamke aliyefumaniwa amekuwa katika mahusiano marefu na mpenzi wake.


Maswali mengi hujitokeza kutaka kuelewa ni kwa nini mwanamke kama huyu ameingiwa na tamaa hadi akachepuka.

Well, yote haya huanza na tabia za pale ambapo mwanamke anakuwa na tabia za kutongoza wanaume wengine ilhali tayari yuko na mpenzi.

Ijapokuwa ni jambo geni, kwa mwanamke aina hii labda kwake anaona tu ni njia ya kuonyesha urafiki kwa wanaume wengine, wengine ni tabia zao ama wanataka atenshen. Zifuatazo ni orodha ya sababu ambazo hufanya hadi mwanamke huyu kutongoza wanaume wengine. [Soma: Njia ambazo wanawake  hutumia kutongoza wanaume]

#1 Hufurahisha. 

Hakuna mtu atalikataa hili. Kutongoza kuna raha yake. Yale mazungumzo na kemia ya mapenzi ambayo inazunguka hewani ni raha zaidi ya chochote. Wewe kama mwanaume ukipata nafasi ya kutongoza mwanamke hutoiwacha kirahisi. Hivyo hivyo, kwa mwanamke hakuna utofauti wowote.

#2 Hajiamini.

Mwanamke ambaye anajikuta akitongoza wanaume wengine ilhali tayari yuko katika mahusiano basi bila shaka kuna kitu ambacho kinamsumbua. Nacho ni kutojiamini. Kwa kutongoza watu wengine wanajipa matumaini kuwa wao wanavutia mbele ya hadhira kiasi cha kuwa wanaweza kuteka atenshen ya wengine.

#3 Anataka atenshen.

Wanawake wengine hupenda atenshen zaidi ya wengine. Hii pia inaenda sambamba na kutojiamini. Anaweza kuwa ni mwanamke ambaye anataka kuonekana na kuwa gumzo kwa kila mtu. So njia rahisi kwake kutumia ni kutongoza kiumbe chochote ambacho kina ndevu.

#4 Labda haumtongozi vya kutosha.

Kama hapati kile ambacho anataka kutoka kwako haswa ikija katika swala la kutongoza, basi atatafuta kwingine kujitosheleza. Hii haimaanishi kuwa hakupendi bali anataka nafasi ya kuweza kutongozwa hivyo basi atatafuta sehemu hio.

#5 Anataka kukuona ukishikwa na wivu.

Wakati mwingine wanawake aina hii hupenda kutaka kujua iwapo wanaume wao wanawajali. Na njia rahisi ya kujua hili ni kwa kuwafanya kuhisi wivu. Kwa baadhi ya wanawake wanachukulia kuwa wapenzi wao wakionyesha ishara ya wivu basi ni ishara tosha kuonyesha kuwa wanawapenda. Kufanikisha hili ndio unapata wengine wakitongoza wanaume wengine kama starehe. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke aingiwe na wivu]

#6 Anawezakuwa anataka muachane.

Sababu nyingine ambayo inaweza kumfanya mwanamke kama huyu kutongoza wanaume wengine ni kuwa anajaribu kutafuta mbinu mwafaka ya yeye kuachana nawe. Labda anahisi mahusiano yenu hayafai hivyo basi anajaribu mawimbi kwingine. Ule wakati ukingundua na mkiachana itakuwa rahisi kwake. [Soma: Kwa nini wanawake hukataa baadhi ya wanaume]

#7 Hajui kama anatongoza.

Wakati mwingine wanawake aina hii wanajaribu tu kuonyesha urafiki wao kwa wengine. Na kwa kuonyesha urafiki huu unapita kiwango cha kawaida na mwishowe inaonekana kama wanatongoza. Hapa itakuwa si makosa yake. Labda anajaribu tu kuonyesha upendo kwa watu ambao anakutana nao.

#8 Hajatosheka na mahusiano yenu.

Kama anatongoza, anaonyesha mahaba na kadhalika kwingine, basi bila shaka itakuwa hajatosheka na mahusiano ambayo yuko nayo kwa sasa. Kama amependezwa na mahusiano yenu kikweli, basi hangeweza kujaribu kufanya hivyo.

#9 Unamboa.

Itakuwa anaboeka na wewe. Kutongoza mwanamke ni muhimu. Hata kama umekuwa na yeye miaka mingi. Hivyo basi mwanamke kama huyu atajikuta ameanza kutongoza wanaume wengine kwa kuwa wewe unamboesha. La kufanya ni kuwa unapaswa kuwa mchangamfu mara kwa mara ukiwa naye haswa ikija katika maswala ya mahabateni.

Well, hizi ndizo baadhi tu za sababu kwa nini girlfriend ama mpenzi wako anaweza kutongoza mwanaume mwingine. Na tumeona kuwa sababu kuu inasababishwa na mwanaume mwenyewe. Hivyo kuepusha tabia kama hii kwa mpenzi wako hakikisha ya kuwa unamtongoza mara kwa mara. Usimpuunze. Mahusiano ni changamoto hivyo lazima upambane nayo. [Soma: Jinsi ya kudeal na mpenzi wako anayetext mwanaume mwingine]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.