Ishara 14 Kuonyesha Kuwa Girlfriend Wako Hakufai


Kuwa na girlfriend huonekana kuwa ni jambo zuri sana maishani. Unaweza kuzama katika mapenzi na girlfriend wako hadi ukasahau mambo ambayo yanakupita mbele yako.


Wakati tunapokuwa katika relationship ambayo tumependezwa huwa tunavalia miwani ya mbao. Hii inamaanisha kuwa tunasahau kuangalia mambo yale muhimu kwa lengo la kufanikisha uhusiano. Ni sawa kwa girlfriend wako kujiachilia, haswa pale atakapoanza kupunguza kujirembesha. Lakini kuna kiwango ambacho hafai kupitisha. Na akipitisha tu lazima uanze kufikiria hatua nyingine la sivyo mbeleni utapata tabu.

Leo hapa Nesi Mapenzi tumekuja na ishara za kuonyesha kuwa girlfriend wako hafai, na jinsi ya kuzitambua mara moja.

#1 Hakusikilizi.

Wakati mwingine huwa tunatia bidii kusikiliza mtu. Lakini ukiona kuwa huyu mwanamke kila wakati ukijaribu kuongea na yeye anaweka shida zake mbele basi ni ishara ya girlfriend asiyekufaa. Nasema hivi kwa kuwa mwanamke asiyetaka kukusikiliza basi hakujali. Na mwanamke asiyekujali basi mbeleni atakuletea majanga. [Soma: Siri za kuwavutia wanawake]

#2 Hayuko ule wakati unamhitaji.

Ukiwa na girlfriend, lazima awe ule wakati unamhitaji kama vile ambayo wewe unakuwa karibu yake ule wakati anakuhitaji. Lakini ukimwona kila wakati ukimwita anaweka maslahi ya familia ama kazi zake mbele basi hii ni ishara tosha ya mwanamke asiyekufaa.

#3 Anavunja mipango yenu.

Kuvunja mipango ghafla si jambo baya katika mahusiano. Lakini ukimwona huyu mwanamke kila wakati anavunja mipango yenu, haswa zile dakika za mwisho, basi hajali kuspend time na wewe. Hana commitment kwako. Pia anaonyesha kuwa kuna vitu muhimu zaidi ya vile ambavyo umepanga. So girlfriend wako kama yuko na hizi tabia basi ni wakati wa kufikiria mara ya pili.

#4 Analenga familia yako na marafiki zako.

Girlfriend mzuri ni yule ambaye anataka kuwajua zaidi familia yako na marafiki zako. Zaidi ni yule ambaye angependa kuspend muda mwingi na watu wako wa karibu. Yeah, najua hatupendi girlfriends zetu watangamane na familia yetu sana, lakini pia girlfriend mzuri ni yule ambaye anajaribu uwezo wake kujivutia karibu nao.

Dalili ya girlfriend ambaye hakufai ni yule ambaye ukimwambia muende mtangamane na familia yako anakataa kata kata. Ataanza kukuletea visababu ambavyo haviishi. Hapa kuwa chonjo.

#5 Anajaribu kukubadilisha.

Kila mwanamke angependa kumnunulia boyfriend wake nguo mpya ili abadilishe mtindo wake wa kuvalia nguo. Lakini ukiona kuwa anapitisha zaidi ya hapa basi ujue huyu wanamke hakupendi. Ni kawaida kuona wanawake wakiwajeuza maboyfriend zao. Lakini ukikataa pia hakuna shida kwa kuwa anakupenda hivyo hivyo. Hii ni ishara ya girlfriend mzuri. Lakini ukimwona mwanamke kila wakati anakujeuza kuanzia mavazi, kazi yako hadi vitu unavyopenda ama nyimbo unazozisikiliza, basi huyu anakupenda kwa masharti. [Soma: Sababu ambazo hufanya mtu kupenda]

#6 Marafiki zako hawampendi.

Wakati mwingine marafiki zetu huona mambo yetu kwa jicho la tatu. Unaweza kuwa wewe na girlfriend wako mnaishi pamoja na kuona mambo yako sawa bila tatizo. Kumbe kuna kitu ambacho mnakosea. Well, marafiki zetu huwa ndio taa yetu wakati mwingine. So ukiona kuwa hawampendi girlfriend wako basi kuna sababu. Wakalishe chini uwaulize.

#7 Anakukontrol.

Je huyu girlfriend wako anataka kujua pale ulipo na uko na nani? Je anataka kuichukua simu yako na kuchunguza kila mwanamke aliye kwa contact yako? Hii ni tabia ya girlfriend ambaye hakufai na hakuamini. [Soma: Saikolojia ya kumfanya mwanamke akupende bila masharti]

#8 Anakutumia. 

Wanawake wengine wanaweza wakajiweka kwa mahusiano na wewe kumbe ajenda yao kuu ni kukutumia kama pamba halafu wakutupe. Mwanamke aina hii utamgundua pale ambapo anakutaka ule wakati anataka yeye na wala si vile unavyotaka wewe.

#9 Anakuchukulia hivi hivi.

Ukimpeleka dinner, kumchukua kutoka kazini, ama kumsaidia na chochote hata kama ni kidogo kuna ishara anafaa kukuonyesha ama kukuambia shukrani. Iwapo unamfanyia haya yote na hakuna hata siku moja amekushukuru basi huyu hakufai. Ni girlfriend mbaya.

#10 Anakuchukulia kama mfanyakazi.

Masikitiko mengi ni kuwa wanaume wengi wanafanyishwa kazi kama punda na girlfriends zao. Ok, sikatai unafaa kumsaidia girlfriend yako mara moja au nyingine. Lakini ukimwona mwanamke anakuamuru umbebee maji, anakulazimisha uende dukani ukanunue kitu flani ama anakupa masharti ya kumfanyia kitu then hapo unachemsha. Unadili na girlfriend ambaye hafai. Usoni mwake anakuona kama mfanyakazi na wala si boyfriend wako.

#11 Anatarajia mengi kutoka kwako.

Kama vile mara ya kwanza ulipowa mnadeti, huyu mwanamke anatarajia makubwa kama vile umtoe deti katika hoteli za kifahari, umnunulie maua kila siku, basi huyu haonyeshi dalili za girlfriend anayefaa. Girlfriend mzuri ni yule ambaye anashukuru yale ulimfanyia awali na sahizi anamakinika zaidi na kupanga maisha ya mbele.

#12 Hakusaidii.

Kusaidiana huwa ni muhimu katika relationship yeyote. Unatoa kidogo na unapokea kidogo. Huu ndio mtindo wa kukuza mahusiano yawe ya nguvu. Lakini ukiona kuwa huyu girlfriend wako hatoi chochote, kazi yake ni kupokea tu bila hata kukupa saprize basi usitarajie zaidi sababu hakufai. [Soma: Mbinu ya utabiri kumfanya mwanamke avutiwe nawe]

#13 Anaisimamia akili yako.

Hii ni ngumu kuigundua haswa kama ashakuteka kisaikolojia. Mwanamke aina hii anaweza kutumia mbinu za kisaikolojia kuiteka akili yako. Mfano ukimwona kuwa girlfriend wako anatumia kigezo cha kufanya mapenzi ili kutaka kile ambacho anataka, ama hata kulia ili kufanikisha ajenda yake chafu basi hapo unachezwa.

Mbaya zaidi anatishia kukatiza uhusiano wenu, kutoboa siri zako, ama kukuharibia maisha iwapo hutamfanyia jambo flani basi huyu ni girlfriend unafaa uachane naye mara moja.

#14 Anakucheat.

Hii ndio dalili kuu ya girlfriend asiyekufaa. Ukimwona girlfriend wako anakucheat haina haja ya kuendeleza mahusiano yenu. Huyu hatakufaa kamwe.

Ok. Hizi ni orodha tu ambazo tumeweza kuziweka hapa lakini najua kuna ishara nyingi zaidi za kuonyesha kuwa girlfriend uliye naye hakufai. Ujanja wako ndio utakuwezesha kuzijua. Hivyo basi makinika na dalili yeyote ambayo itajitokeza.

Amani Kwako!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.