Jinsi Ya Kumuathiri Mwanamke Na Mbinu Ya 'Wazo Mkato'


Imagine unaaproach mwanamke wa ndoto yako, halafu sahizi unaongea naye. Kwa kuwa unataka kumfanya akuwe interest na wewe muda wote unatumia mbinu zifuatazo kuhakikisha anapendezwa nawe...

Je, uli...

- mwambia stori ya kupendeza kuonyesha kuwa una 'hadhi ya juu'

- fanya maujanja ya kiini macho ili umfurahishe...

- buni maslahi ya uongo (interest) halafu ukamwambia ajieleze kwa undani huku ukihakikisha kwa kujifanya ya kuwa unamsikiliza kwa umakini...

...na orodha ni ndefu haiishi na hapo...


Kwa mshangao kwako unamwona akiangalia juu ya bega lako mara kwa mara, na anaonekana kuwa amevutiwa na mambo ambayo yanafanyika kando yake (isipokuwa wewe). Unaanza kujishuku na uwezo wako wa michongo ya kuhifadhi, na kutojiamini kunaanza kugonga katika akili yako.

Unajaribu kumaintain hadhi yake ya maslahi, lakini unagongwa na jibu, "Nimefurahi kukutana na wewe, lakini nataka kuondoka sahizi".

Ok relax. Usibabaike. Sote tumeshawahi kuwa huko wakati flani. Pia mimi nishawahi kupatikana.


Wakati ambapo imekutokea, najua ulikuwa na mawazo ambayo yalikuwa yakikugonga kichwa. -"Kama tu ningekuwa na uwezo wa kumwambia stori za kuvutia zaidi, najua angevutiwa na mimi zaidi na zaidi."

Ndio nakubali hii ingekuwa ni ukweli (kwa kiasi flani), lakini kuna vitu unafaa kujua kwanza-


Kile UTAKACHOSEMA si muhimu na vile ambavyo UTAKAVYOSEMA.

Kwa sababu hii, chapisho hili kutoka kwangu sitakufundisha jinsi ya kujifunza kutumia mistari ya papo kwa hapo, michongo, mbinu murwa za kumfurahisha wala mbinu za kumchekesha mwanamke.


Badala yake, utavumbua SIRI MOJA ya kumnasa mwanamke ambayo hujawahi kuiskia wala kuisoma mahala popote pale. Kwa kutumia mbinu hii ambayo nimeamua kugawa nawe, utakuwa na uwezo wa kumfanya mwanamke yeyote kuendelea kuwa interested na wewe -bila kutilia maanani kile ambacho utasema.

Shuleni, ulifundishwa ya kuwa unapaswa kumaliza hoja fulani kabla ya kuenda kwa hoja ama mada nyingine. Kwa ukweli, huu ulikuwa ni ushauri mzuri, lakini tu kama unataka kumfanya mwanamke alale.


Iwapo unataka kuwa kama Don Juan na kuwafanya wanawake wakuwaze ndotoni mwao, basi unafaa uache hii tabia na uanze kutumia mbinu ambayo nataka kukuonyesha sasa hivi.

Mbinu Ya 'Wazo Mkato' - Ni nini, Na Kwa Nini Inafanya Kazi

Mbinu ya 'wazo mkato' ni rahisi kuieleza, kama tu vile jina lenyewe linavyomaanisha - ni mawazo au stori ambayo haijakamilika. Unaanzisha stori ya kuvutia, halafu badala ya kuimaliza, unaanzisha stori mpya.


Wakati ambapo tunakumbana na wazo ambalo halijakamilika, akili zetu zinalazimishwa kutafuta jinsi ya kutatua jambo hilo. Kwa mazingira ya kuwavutia wanawake, mbinu ya 'wazo mkato' inamlazimisha mwanamke kumakinika na kila ambacho utakuwa unasema - hii ni kwa sababu akili yake haitomruhusu kufanya jambo jingine.

Hebu fikiria unamwendea mwanamke na kumwambia, "Hi. Naitwa Papito, na mimi ni mweka hazina katika Benki ya Barclays. Unataka kujua nimefanya kazi gani siku ya leo?"

Nafasi hapa ni kuwa hatakuwa na interest zozote kutaka kujua kutoka kwako -hii ni kwa sababu umejitokeza kama mtu ambaye hana thamana ya kuongea naye kamwe.


Badala yake mbona usimwambie "Kuna kitu ambacho nakijua kukuhusu, lakini siwezi kukuambia." Hii itajenga tenshen katika akili yake -ambayo inaweza kutatuliwa na wewe pekee.

Hapa gundua ya kuwa nishati zote zimelenga KWAKO. Wewe sasa ndiwe utakayethibiti maongezi na kutangamana kwenu, na utagundua ya kuwa CHOCHOTE utakachomwambia (kuanzia mwanzo hadi mwisho) atakumbuka.

Nishati ya nguvu! Ama waonaje?

Jinsi ya kutumia mbinu hii wakati mwingine ambapo utakutana na mwanamke usiyemjua

Wakati ambapo unakutana na mwanamke, je huwa unamwambia jina lako ghafla wakati ambapo unamsalimia kwa kumpa mkono? Kama ni kweli, basi kuna nafasi kuu kuwa atasahau jina lako (ama kitu chochote kukuhusu) wakati ambapo atamaliza maongezi na kuenda zake.


Hivi ndivyo ambavyo ninavyosema wakati ambapo mwanamke ananiuliza jina langu - kwa kutumia mbinu hii ya 'wazo mkato'.

"Babangu alikuwa anapenda kuniambia ya kuwa mwanzoni alitaka kuniita jina la Abujahal - baada ya amiri jeshi mkuu wa Rashidun enzi za zamani. Halafu nilimuuliza, "baba, hilo ni jina zuri kabisa. Mbona hukuliweka?"
Na aliniambia hivi, "Ok. Sababu kuu ni kuwa kulikuwa na samaki ambaye tulikuwa tukimfuga alikuwa pia anaitwa Abujahal, na ile siku ambayo ulizaliwa aliweza kuliwa na paka ambaye tulikuwa tukimfuga ambaye aliitwa Muadh. So hatukutaka kukumbushwa kuhusu huyo samaki aliyekufa so tukaamua kukuita Ibrahim""

Badala ya kumwambia jina langu hapo hapo, huwa nimezunguka katika mada kuhusu jina langu, na hivyo kuibua maswala ambayo yanakuwa kama tenshen katika akili yake.

Bila kujielewa atajaribu kuvumbua tenshen hio, hivyo kumfanya aathirike zaidi na kila neno ambalo litatoka kutoka kwa kinywa changu.

Kama ningemwambia direct kuwa naitwa 'Ibrahim Morowa' kuanzia mwanzo, angekuwa ashanihukumu kama wanaume wale wengine ambao amekutana nao katika party flani, na hangenitambua.

Kwa kutumia mbinu hii ya 'wazo mkato' nimeonyesha mambo matatu makuu wakati mmoja: kwanza ni kuwa nina hadhi ya juu, pili ni kuwa nina hisia ya juu ya ucheshi, na tatu kuwa mtu mzuri wa kuibua stori. Kwa kifupi, nimejitokeza kama mwanaume wa kuvutia.

Upo!? [Soma: Sanaa za Kutongoza za Nesi Mapenzi]

Psss! Nakushauri uingie katika group letu changa la Facebook kwa jina Nesi Mapenzi ambapo utanipata huko nikijibu maswali ambayo uko nayo, plus utapata nafasi ya kutangamana na wote ambao husoma maujanja ya blog hii ya mapenzi.

1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.