Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupeze Ama Akumiss

Kumfanya mwanamke akumiss ni kitu muhimu kwa mwanamume kufanya kwa sababu mwanamke atakuwa akikufikiria wakati mwingi zaidi na kutaka kuwa na nafasi ya kuwa kando yako kila mara.
Kufanya hivyo ni rahisi sana na si lazima uwe na shahada ya uzamili ya kutongoza mwanamke ili uweze kumfanya akumiss.
Ukifuata hizi njia tatu kwa umakini bila shaka kila ambapo atakapoenda utakuwa ukicheza ndani ya ubongo wake.

1. Kuwa wingu lisilofahamika
Hii inamaana ya kuwa usikuwe na yeye wakati wote. Kama mmepanga kukutana na yeye ili muongee kwa saa limoja, hakikisha umekaa na yeye muda wa nusu saa halafu utoe kisababu cha kujiondoa katikati ya maongezi yenu. Hii itamfanya kuachwa kwenye mataa na kutaka kujiuliza maswali kama mungekuwa naye saa zima mngeongea nini. Hii itamfanya yeye kukufikiria kwa urahisi. Lile ambalo mmeliacha kati kati litakuwa likimzunguka akilini mwake. [Soma: SMS 47 za mapenzi za kumnyegeza mwanamke]

2. Uwe usukani
Mwanamke yeyote, uwe uko na mahusiano naye au la, hakikisha kuwa wewe ndiye unayeamua mambo yote mtakayoyafanya mkiwa pamoja. Kama ni kuchagua sehemu ya kukaa, sehemu ya kula, sehemu ya kutoka ama chochote kile ambacho mnachotaka kufanya, wewe ndiye utakuwa ukiamua bila kumwachia nafasi yeyote ile. Huu ujanja utamfanya yeye kutofanya jambo lolote bila kukufikiria wewe. Yaani atakuwa hawezi kujiamulia mwenyewe hadi wewe uwe karibu yake. Hii automatically itakuwa njia rahisi ya kwake kukufikiria wakati wote ule atakapokuwa akifanya shughli zake. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akunotice]

3. Kuwa mtu wa mwisho akilini mwake
Utafiti umegundua ya kwamba kile kitu ambacho mtu hufikiria cha mwisho ndicho kitakachomjia ndotoni mwake. Na kama usiku wake umemuendea vizuri bila tatizo, basi asubuhi yake kitu hicho kitakuwa bado kinamjia akilini. Mbinu hii inaweza kutumika vizuri kama utahakikisha ya kuwa wewe ndiye mtu wa mwisho kabisa ambaye ameongea naye...yaani unaweza kumpigia simu nyakati zake za kulala. Hii itamfanya yeye kuweza kukuota na kuchangia  kukufikiria siku ya pili. Hii ni njia nyingine rahisi ambayo itamfanya yeyote kukufikiria mara kwa mara.

Niamini, ukitumia mbinu hizi tatu vizuri, mwanamke yeyote atakuwa akikufikiria wewe mara kwa mara na inafanya kazi asilimia 100 bila shaka yeyote ile.
[Soma: Jinsi ya kurespond baada ya mwanamke kukukataa]

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupeze Ama Akumiss Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupeze Ama Akumiss Reviewed by Admin on 11:09 AM Rating: 5

1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.