Jinsi Ya Kumwambia Mwanamke Kuwa Ni Mrembo Bila Yakuonekana Fala


Kumtamkia mwanamke kuwa ni mrembo si jambo rahisi kama vile wengi hutarajia. Lengo kuu la kumwambia mwanamke kuwa ni mrembo huwa ni kutaka kumsisimua kihisia na pia kutaka kumfanya apendezwe na wewe. Lakini tatizo ni kuwa kutamka “wewe ni mrembo” inakuwa na changamoto zake na leo tutakujuza jinsi ya kumwambia mwanamke kuwa ni mrembo kwa njia rahisi ili uweze kumfurahisha.


Wanawake wengi washazoea kuambiwa ya kuwa wao ni warembo, hivyo wakati utakapoamua kumwambia kuwa ni mrembo lazima uhakikishe ya kuwa unaamini kile ambacho unamwambia na pia unafaa aone kuwa ni jambo spesheli kwake. So haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati unapomwambia kuwa ni mrembo.


#1 Tafuta jambo la kutumia kumwambia kuwa ni mrembo.

Wakati unapoamua kumwambia kuwa mwanamke ni mrembo kuna mambo ambayo unafaa kutumia kutimiza urembo wake. Kwa mfano hupaswi kumwambia mwanamke ni mrembo tu bali unafaa uongezee kitu ambacho unaona kinamfanya apendeze. Labda inaweza kuwa ni hairstyle mpya, nguo, macho, tabasamu na kadhalika. Hapa lazima utumie ubunifu wako. Mfano mimi naweza kusema hivi, “Leo Martha umependeza, hairstyle yako imekurembesha.


#2 Tafuta hulka yake.

Kando na kuwa urembo hutumika mara nyingi kusifia umbo ama vitu vinavyoonekana, urembo pia huweza kutumika kusifia hulka ama tabia ya mtu. So usibaki ukimsifia mwanamke kuwa ana macho mazuri ya kupendeza pekee bali pia unaweza kuchukua hatua ya kumsifia tabia zake. [Soma: Ishara ya kuonyesha mwanamke amevitiwa na wewe]


Mfano ni mwanamke anayependa kutia bidii maishani, mchangamfu, ama ni mtu anayependa kujituma unaweza kuchukua nafasi hii kumsifia. Hii itakupa nafasi ya juu zaidi kumfurahisha mwanamke kwa kuwa si wanaume wengi husifia wanawake kwa kutumia hulka zao.


#3 Chagua wakati unaofaa.

Ungependa kumwambia mwanamke kuwa ni mrembo kila wakati unapokutana na yeye. Lakini hio haifai kwa kuwa ukiwa unaambiwa kitu kimoja kila mara utaanza kutia shaka jambo hilo. Hivyo hupaswi kuwambia mwanamke ni mrembo kila wakati. Lazima uwe na wakati maalum wa kuchagua kutumia kumwambia mwanamke kuwa ni mrembo. [Soma: Jinsi ya kumdhaifisha mwanamke ili akupende]


#4 Msifie faraghani.

Hufai kumwambia mwanamke kuwa ni mrembo kwa mitandao ya kijamii ama mbele ya kila mtu. Wakati mwingine wanawake hupenda vitu viwe siri. Hivyo tafuta wakati mzuri ambao utatumia kumwambia kuwa ni mrembo. Wakati mzuri ni ule ambao utakuwa mko wawili pekee. Hapa utaifanya ikuwe spesho kwake na atapenda.


#5 Tumia miondoko ya mwili kujieleza.

Wakati unapomwambia mwanamke kuwa ni mrembo unafaa kuhakikisha ya kuwa unatumia miondoko ya mwili ifaayo. Mfano huwezi kumwambia mwanamke anapendeza wakati unacheka ama unakuwa unafanya mambo mengine.  Lazima uwe umemakinika na kuwa na nishati inayofaa ili uweze kumwambia ya kuwa anapendeza. Upo? [Soma: Jinsi ya kusexchat na mwanamke]


So haya ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyatumia kumwambia mwanamke kuwa anapendeza na aweze kukuelewa kwa urahisi zaidi. Natumai utatumia vigezo hivi vizuri ili uweze kumfurahisha mwanamke ambaye umependezwa naye.
1 comment:

  1. Kweli kabisa somo nimelielewa na mara nyingi nami nimekuwa kwenye makosa baadhi

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.