Jinsi Ya Kutumia 'Nguzo Ya Maingiliano' Kuwavutia Wanawake


Ushawahi kujiuliza kwa nini kuna baadhi ya wanaume wakiingia katika klabu hutoka na wanawake wanaopendeza zaidi? Ama ushawahi kujiuliza ni kwa nini kuna baadhi ya wanaume wakiingia katika klabu wanawake wote wanataka kuongea ama kutangamana nao. Na je mbinu hii inaweza kufanikishwa kivipi?


Hebu tuangalie hii mifano...

Hali #1: Kikundi cha wanaume watatu wameingia katika klabu. Wanaume hao wanatafuta meza ya kukaa. Wanapata sehemu ya kukaa na wanachukua masaa mengi wakinywa bia na kufuata kila mwanamke anayepita kwa macho huku wakipigana makumbo kuonyesha wanaridhika. Wanawake wanawadokezea macho ya kigeni na wanaipita sehemu walioko haraka iwezekanavyo. Baadae, wanaume hao watatu wanaapproach kikundi flani cha wanawake katika meza flani na wakatumia michongo yao mizuri kuwavutia. Hao wanawake waliangaliana, wakasimama na kuenda zao.

Hali #2: Kikundi cha wanaume watatu wanaenda katika klabu nyingine na mara moja walianza kusalimia watu walioko katika klabu hio kabla hawajaenda katika meza iliyokuwa kando. Kwa muda wa lisaa moja walikuwa wakitumia muda wao wakitangamana na (wanaume au wanawake) waliokuwa wakipita, na cha kushangaza ni kuwa wanawake walionekana wakijitokeza kutoka sehemu yeyote kuja kuwasalimia wanaume hao. Baadaye, waliapproach kikundi cha wanawake ambao walikuwa wametulia katika meza flani. Na bila kupoteza muda wanawake hao walikubali kudensi na wanaume hao katika sakafu.

So tofauti ni ipi katika makundi haya mawili? Jibu ni kuwa kundi la pili lilitumia 'nguzo ya maingiliano' ilhali kundi la kwanza halikutumia.

Kundi la kwanza halikuwa na hadhi ya kijamii. Walijitawanya na kujitenga kwa dunia yao. Tendo walilolijenga la kujitenganisha lilijenga athari hasi kwa kila mtu katika sehemu hio. Katika lile la pili, kundi hilo lilijenga mazingira ya kuonyesha kuwa wako huru kutangamana na yeyote hivyo ni rahisi kwao kuongea nao na kuwaaproach. Mwanamke hatohisi shoto kupita karibu na meza ya kundi hilo na kukaa hapo.

Kuwa na marafiki waliokuzunguka, na kuonyesha uwezo wa kujenga urafiki na watu kutaongeza hadhi yako ya kijamii mbele ya macho ya wanawake ambao unataka kuwavutia. Utakuwa "umechagulika" na wanawake ambao tayari wamevutiwa kwako.

Jambo zuri kuhusiana na mbinu hii ya nguzo ya maingiliano ni kuwa unaweza kuitekeleza hata kama utakuwa uko pekeako. Pindi tu utakapoingia katika himaya ya kujamii, jenga urafiki na utangamane nao. Usijitenge kwa kona halafu utarajie kuwa wanawake watakuaapproach; hawatathubutu.

Hii hapa ni mbinu ya haraka ambayo itajenga nguzo ya maingiliano na uweze kutambulika na wanawake:

Hatua #1. Ingia ndani ya klabu na uweke tabasamu kwa mwanamke kando yako. Ukiona kikundi, approach halafu ufunguke. Tumia madakika kadhaa na wao mkibadilisha salamu na mawazo kabla ya kujiondoa. Kama uko na rafiki yako unaweza kumtuma katika kikundi kingine.

Hatua #2. Tangamana na ujenge urafiki na kila kikundi halafu katulie katika sehemu ambayo imetulia katika hio klabu na rafiki mpya ambaye umekutana naye kwa moja wapo ya makundi hayo. Ongea na kusalimia yoyete ambaye umekutana naye awali katika klabu hio.

Hatua #3. Usichague wala ubague. Ni lazima utangamane na uongee na kila kundi hata kama mwanamke unagemuwinda hayuko katikayo. Fikra hii ni kukufanya utangamane zaidi ili uongeze hadhi ya kijamii na ukutane na watu wengi zaidi.

Kufikia mwisho wa usiku, utakuwa ukiongea na kubadilishana mawazo na karibu kila mwanaume na mwanamke hapo. Na katika harakati hii itakusaidia wewe kupata mwanamke unayemvizia kwa urahisi sana. [Soma: Mbinu rahisi ya kupandisha hadhi yako kwa wanawake]

Kazi kwako sasa!

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.