Sababu 14 Za Kwa Nini Unafaa Kumwagiza Mwanaume Mtoke Out Naye


Watu wamelelewa katika mazingira na jamii tofauti tofauti ambazo zinatarajia wanawake kuwa wapole na wanyenyevu, ni tamaduni ambayo inatarajiwa kuweko kwa kila mwanamke. Lakini kadri siku zinaposongea maisha nayo yanabadilika. Wanawake kwa sasa kupitia ufeministiki wamebadilika kuwa wanawake wapole na wanyenyekevu hadi kuingia wazima wazima kupambana na maisha ya ulimwengu wa karne ya 21.


Ijapokuwa wanawake wametoka mbali, bado jamii inawatarajia kuwa na tabia ambazo zilikuwa zikifuatwa na kizazi cha mababu zetu ambapo mwanamke alikuwa akifanywa kama mali ghafi  ya jamii, ambaye hana uwezo wa kuamua mbele ya jamii. Lakini tunavyojua ni kuwa sahizi kuna wanawake wengi ambao wamefanikiwa kimaisha haswa baada ya kuchukua hatua mikononi mwao wao wenyewe, hii ndio maana kuna sababu nyingi na nyingi ambazo wewe pia unafaa kuchukua huo mkondo.

Okay...

Kila mwanamke anahitaji mwanaume wa nguvu. Na kupata mwanaume wa nguvu lazima uwe mwanamke wa nguvu. So hizi ni sababu ambazo mwanamke anafaa kuchukua hatua ya kwanza ya kuapproach mwanaume na kumwambia.

Kwa nini unfaa kumwomba mwanaume utoke out na yeye

Hizi ni baadhi ya sababu ambazo unafaa kuchukua usukani wa mchezo wa kudeti, na uache kungojea mwanaume achukue hatua wa kwanza.

1. Una nguvu zote juu ya mahusiano yenu
Si itakuwa vizuri kama una uwezo wa kudibiti mahusiano yenu angalau hata mara moja? Mbona usichukue nafasi hii ya kuchukua na kudhibiti maamuzi katika mahusiano kwa kuangalia vile yataenda? Hii itaondoa ile hatua ambayo unakaa umgojee mwanaume aamue kama mahusiano yenu yatakuwa ya uhakika au la.

2. Wanaume wataona kufurahishwa kubembezwa kwa mabadiliko
Wanaume wengi ambao wanawapenda wanawake wao wataitikia vizuri kama wanawake wao ni wale wa kutaka-watakacho. Hivyo kadri unapoongeza ujasiri wako hadi kumwagiza mtoke out, mwanaume aliyedhabiti atazidi kuvutiwa kwako.

Iwapo mwanaume anajibu kihasi, basi atakuwa anatafuta mwanamke ambaye ni mpole na mnyenyekevu, na hio inakubalika. Kama ulijaribu kumwambia mtoke out halafu majibu yake hayakuridhisha, ni dalili ya kuwa mwanaume huyo hamuwezi kuwiana katika maisha yenu ya mbeleni hivyo unafaa uachane naye uangalie mwingine.

3. Unashika usukani wa machaguo ya deti yako
Hatuko karne za akina Merilyn Monroe, karne ambazo wanawake walikuwa wakingojea matakwa ya wanaume. Tuko katika karne ya 21, ambayo wanawake wanaweza kusema chochote mbele ya uso wa mwanaume. Nyakati za kumtegemea mwanaume akupe fedha, familia na kukuamulia maisha yako yamepitwa na wakati. Kadri unapotafuta wanawake kwa udi na ambari ndipo unaongeza nafasi yako ya kupata mwanaume ambaye analingana na maslahi yako.

4. Hakuna kungojea. Kama unamtaka, nenda ukamchukue
Inaogopesha. Lakini si inakaa kuvutia, kuchangamsha na changamoto pia? Hebu fikiria hisia utakazozipata wakati ambapo umefanikiwa mpaka akakubali kusema ''Ndio''? Kuna sababu ambayo wanaume hupenda kufukuzia wanawake: ni kama uraibu vile. Mbona wanawake wasikue na hio tabia pia?

5. Unayemzimia anaweza kutojua kama unaishi
Najua ushawahi kuona hii filamu za vijana ambazo unamwona msichana mzuri ambaye anampenda mvulana flani lakini kwa kuwa ni mwoga anajificha kwa nyumba na vitabu akisoma halafu mwishowe inafika mahali anaonekaniwa na yule mvulana aliyemzimia. Well, hio hufanyika kwa filamu na sinema pekeyake na unajua hivyo!

Ni bayana ya kuwa kama unataka mwanaume uliyemzimia akutambue, hawezi kukutambua mpaka ile siku ambayo utamwambia directly. Kama bado haonyeshi dalili za kukutaka, hastahili kupata atenshen yako. Songea mbele, na utafute mwingine uliyemzimia ambaye unaweza kumvizia.

6. Kama ni mzuri, anaweza kuchukuliwa kabla hata kupata nafasi ya kukugundua
Wanaume wazuri, wenye dalili za ndoa ni vigumu kuwapata ama kuwaona haswa miaka ya 20. Iwapo utapata nafasi ya kukutana na mmoja na umependezwa naye, chukua nafasi hii adimu kwa kumwonyesha kuwa wewe ni mwanamke mzuri tayari wa kuishi naye.

Kucheza cheza na nafasi nzuri kama hii itafanya upigwe chini na mwanamke mwingine ambaye amemwona. So ya nini kungojea? Kama ataringa, bahati mbaya kwako, hakuna kosa litakuwa limefanyika.

7. Wanaume wanataka kupewa fununu wakati mwingine
Wanaume ni kama wametoka katika sayari nyingine! Kama hutajieleza kwao hawatapata fununu zozote kutoka kwako. Wanaume kawaida wakionyesha interest kwa mwanamke ni rahisi kujulikana. Mwanzo hili neno friend-zone lilizinduliwa na wanaume.

Hivyo iwapo unataka rafiki yako wa kiume atambue ya kuwa mnataka kuchukua urafiki wenu hadi level nyingine, mwanamke, unafaa kumwambia. La sivyo mtatengana na hatapata kuelewa chochote kile.

8. Hata uvalie kivipi, mwanaume hatajua kama umemvalia kwa ajili yake
Mbaya zaidi ni kuwa atakuona ya kuwa unavalia kama mdoli kila siku ili uwapendeze na kupata atenshen kwa wanaume wote. Na haitaingia kwa akili yake ya kuwa umevalia nguo hizo zote kumridhisha *mjinga fulani* ambaye ni yeye.

9. Wanawake ambao hutaka-watakacho kawaida wanapata wanaume wazuri
Wanaume ambao wanawapenda wanawake ambao wanapenda kile wanachotaka huwa ni bora zaidi kuliko aina nyingine ya wanaume. Mwanaume mwenye nguvu ndie anayeweza kuhandle mwanamke aina hii. Ni rahisi, iwapo mwanamke anataka mwanaume ambaye anaweza kumhandle jinsi alivyo na nguvu basi anapaswa kumtafuta yeye mwenyewe kujua iwapo ni mwanaume wa kutosha kumdhibiti.

10. Kumwambia mwanaume moja kwa moja huwa kunamaanisha biashara, na huogopi kiurahisi
Wanawake ambao ni jasiri  kamili kumwambia mwanaume watoke out pamoja huwa ni changamoto kuu kwa mwanaume.  Wanaume ambao wanaingiana na hili wanajua unamaanisha biashara, na si mwanamke yule wa kumwambia ''La''. Itamkumbusha mwanaume ni mwanamke gani anayedeal naye hivyo hatothubutu kukuchezea kama iko kwa akili yake.

11. Wanawake wanaojua wanataka nini hupata kile wanachotaka
Zari aka thebosslady alimtaka Diamond, mwanaume ambaye aliyepachikwa jina la sukari ya wanawake, hakumruhusu Wema Sepetu aende naye. Alionyesha uwezo wake wa uke wake na kuonyesha nguvu zake za kumtaka mwanaume ambaye anapendwa na wanawake wengi. Bila woga alijieleza na akakubaliwa. Hivyo pia wewe nenda ukamtefute Diamond wako bila woga wowote.

12. Kama unataka kuwa kivuli, utabaki hapo kwa muda -na kwa muda zaidi, ama milele
Ok simaanishi ya kuwa unafaa kuwa kuwa mwanamke wa drama kila mahali. La!, Lakini pindi utakapoamini kuwa wewe sehemu yako ni kukaa kivulini, imani hio itakushika.
Mwanamke anafaa kuwa na confidence ya kuweza kuapproach na kufanya chochote kile. Labda unaweza kufanyika hivyo wakati wa miaka yako ya sekondari lakini ikipita miaka ya 20 kwenda mbele haufai kujiweka kivulini. Chukua hatua sasa.

13. Kama amekukataa, usidhoofike, ni experience umepata. Mskitie amekosa nafasi nzuri ya kuwa na mwanamke bora kama wewe
Hautakufa kama amekukataa. Hata hatokuzuia wewe kushindwa kula. Najua ni uchungu kwako kukukataa lakini kuna tatizo? Chukulia hivi, miaka 10 baadae utakuwa ukijicheka kuhusu kuahirika kwake.

14. Wanawake wana nishati sikuhizi. Akina nani ndio wanaorun dunia?
Beyonce amesema kuwa wanawake ndio wanaoindesha dunia. So mbona kila kitu usikichukulie hatua ya kwanza? Mwanzo si jambo gumu la kufanya. Kwani wanawake wengine wanafaulu vipi kuchukua hatua hii na wewe usiweze?


Kumalizia ni kuwa wanawake wanafaa kuchukua hatua ya kwanza kama umemzimia mwanaume. Haina haja kukaa mahali pamoja ukingojea uletewe chakula kwa meza hadi kwa mdomo. Maisha ni nako!
1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.