Video Ya 'Nasema Nawe', Tumejifudisha Nini?


Ok katika pitapita zangu kwa mtandao nilijipata nikiangalia hii video ya Diamond ya 'Nasema Nawe'. Hii video imekuwa hit na gumzo la mjini kwa kuwa ndani yake kuna wadada wakinengua viuno. Well bigs up kwa director aliyevanikisha hio video.

Nimeamua kuandika hii post maksudi kwa kuwa nimeona hii video imekuwa maarufu sana na bila shaka zaidi ya 2 million views youtube inaashiria ya kuwa asilimia 60 ya watu kanda hii watakuwa wameiona video hii. So tumejifunza nini?

Kama Nesi Mapenzi najua hautarajii niandike kuhusu mitindo tofauti tofauti ya densi ya mduara katika hii video ama kwa nini Diamond aliamua kuvalia mavazi ya kanjibai bali kuhusu mhusika mkuu katika video na swala zima ninalozunguka na mahusiano.

Tukiongea kuhusu mhusika mkuu hapa ambaye tumempa jina 'Mamito' (jina lake halisi katika hii video hatulijui) anaonekana amewaudhi wanawake wengi katika mtaa anaoishi kwa kuwa anatabia za kuwaiba mabwana wa wenyewe. Tabia hii yake ya kuwapokonya na kuwaiba mabwana za watu inaonyesha iliwakera kiasi cha kuwa wakampangia njama la fumanizi na kumuabisha na kumkomesha hadhani. Hongera kwa hatua hii kwa kumkomesha 'Mamito'. Lakini swali tujiulize ni ilikuwaje hadi huyu 'Mamito' akaweza kuwashawishi mabwana za watu na kuwapokonya kweupe mbele za mabibi zao? Inakuwaje 'Mamito' anaweza kuzuzua kikao kizima cha wanaume kuanza vijana hadi wazee? Kwani huyu 'Mamito' ana nini cha zaidi kuwaliko wanawake wengine? Anatumia mizizi?

Mamito akiwazuzua wazee mpaka vijana

Well. Maswali ni mengi ya kuuliza kumhusu huyu 'Mamito'. Majibu niko nayo. Kabla sijayajibu maswali haya nataka nieleweke ya kuwa simsapoti yeyote ambaye anachukua hatua ya kumpokonya mpenzi wa mwenzake, kuharibu mahusiano ya wapenzi wawili nk.

Kile ninachosistiza kuangazia hapa ni kuonyesha umuhimu wa mwanamke kwa mwanaume na mambo gani ambayo yanaweza kumfanya mwanaume kuvutiwa kiurahisi na mwanamke, jambo ambalo wanawake wengi wanapuuza halafu mwishowe inakuja kama hili tatizo la 'Mamito' na wanawake wa kijijini mwake. Awali niliandika chapisho likieleza aina ya tabia ambazo kila mwanaume anatamani mpenzi wake awe nazo, na bila shaka huyu 'Mamito' angepata kumi juu ya kumi kama tungemhisabia.

Kwa nini 'Mamito' katika video ya Nasema Nawe aliwapagawisha wanaume wote

1. Mwonekano wake
Katika hii video utaona utofauti wa Mamito na wanawake wale wengine, nao utofauti huu ni kuwa Mamito alikuwa anavalia mavazi, mitindo ya nywele ambayo ni tofauti na wengine. Wale wanawake wengine katika hii video inaonyesha kuwa wana tabia ya kuvalia nguo za madera. Sikatai ya kuwa madera ni nguo za kuvalia lakini nasistiza ya kuwa kuvaa madera mara kwa mara, mchana kutwa, madera yanayofanana hujui hili ulilolivaa leo na lile la juzi ni lipi au gani hakupendezi kamwe. Mambo ya kuvaa nguo aina ama mtindo mmoja inafikia wakati flani mwanaume anachoshwa kwa kuwa unatabirika kiurahisi.
Kwa upande mwingine, Mamito anaonyesha ustadi wa kubadilisha badilisha nguo. Leo anavalia hivi kesho anavalia vile, kwa sababu mwili ni wake.

2. Anapenda kutangamana na wenzake
Kuna mambo mengine ambayo wanaume na wanawake wanagawa ikija maswala ya kupenda. Kama vile mwanamke anavyopenda mwanaume ambaye anapenda kutangamana na wenzake, hivyo hivyo mwanaume anapenda mwanamke mwenye tabia kama hio.
Katika video hii 'Mamito' anasemwa ya kuwa anapenda kukaa vikao na kusema ya watu ama kusengenya. Kwa mwanaume, kumwona mpenzi wake katika vikao kama hivyo vina manufaa kwake. Kwa mwanaume hajui ni maongezi gani yanayoongewa hapo, labda kile ambacho kitamjia akilini mwake ni wanaongea ama kufundishana mitindo mipya ya kumpendeza mwanaume ama labda kujuzana jinsi ya kufanya mtindo wa sita kwa sita bora zaidi. Mambo ya kusengenya hayamjii kwa akili. Hivyo mwanaume bila shaka anavutiwa na mwanamke ambaye anatangamana na wanawake wenzake kuliko yule ambaye anamuandama mpenzi kivuli.

Bibiake mshonaji akionyesha wivu kweupe
3. Wivu
Kosa jingine ambalo wanawake wanafanya ni kuonyesha wivu wakati ambapo wapenzi wao wanapoongea na wanawake wengine. Katika hii video inadhihirika pale ambapo Mamito anapoonekana na bibiake mshonaji. Hapa kosa ambalo bibi ya huyu mshonaji analofanya ni kuonyesha wivu mbele ya Mamito. Well, najua wivu kwa binadamu ni kawaida lakini kuonyesha kweupe kuwa una wivu mbele ya mwenzako ni hatari kwa kuwa unaashiria ya kuwa huna uwezo wa kummiliki mpenzi wako. Hapa Mamito aliuchukua huu mwanya na kuhakikisha amemfunga fundo yule mshonaji kwa njia ya rahisi.

4. Miondoko yake
Ushawahi kuskia msemo wa 'wanawake wana maringo kama ya tausi'? Huu msemo bila shaka utakuwa ulianziswa na mwanaume. 
Mwanamke amezaliwa kuwa na maringo. Maringo kwa mwanamke ndio kunamvutia mwanaume. Usimsikilize yeyote yule atakayekwambia uache maringo. Mwanzo ukiwa na maringo unamvutia zaidi mwanaume. Katika video hii ya Nasema Nawe, Mamito ameuonyesha uwezo wake wa kutumia kipawa chake cha maringo. Miondoko yake ya kuongea akiwa na wenzake hadi anapokuwa akitembea barabarani. Anaonyesha 'uanawake' wake, jambo ambalo mwanaume yeyote anatamani.

Miondoko ya maringo aliyoyasheheni Mamito

5. Ushawishi
Katika hii video inaosha ya kuwa Mamito haoni haya ya kuonyesha hisia zake kwa mwanaume anayempenda. Hii imedhihirika kweupe pale ambapo anapopimwa kiuno chake na mshonaji. Kumwelekezea makalio yake kwa mshonaji ni ishara ya kuonyesha ya kuwa alikuwa na azma ya kumshawishi huyu mwanaume.
Ok. Hapa sikubaliani na hii tabia ya Mamito lakini je ulikuwa ukifahamu ya kuwa hii ni moja ya tabia ambayo wanaume wanapenda? (Hii tabia tuliifafanua hapa) Tabia hii inaonyesha ya kuwa mwanamke aina hii si mwoga wa kuonyesha hisia zake kwa anayempenda. Wanaume hupenda tabia hii iwe na wapenzi wao wakiamini ya kuwa tabia hii kwa mwanamke hatoona aibu ya kujaribu mitindo na style mpya za mapenzi.

6. Kutojutia alichofanya
Baada ya kumnasa katika fumanizi gesti ya Mbelikwe na kumwekea kikao cha kumsuta, Mamito hakuonyesha kushtushwa wala kubabaika. Kile alichofanya hajutii wala kuomba msamaha. Anaamini ya kuwa kosa si la kwake bali ni la hao wanawake. Kama huwezi kulizingiti zizi lako utamlaumuje simba kwa kula mbuzi wako na yeye yuko mawindoni?

Ushawishi wa Mamito ulikuwa zana yake kuu


Haya ndio baadhi ya maoni yetu kutoka Nesi Mapenzi kuhusiana na swala zima la video ya Nasema Naye. Kuna mambo mengine ambayo tungeweza kuyaongezea kuhusu kwa nini wanaume waliweza kunaswa na mtego wa Mamito lakini tumeamua kukomea hapa. Ni hayo tu!
No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.