Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupatie Namba Yake Yeye Mwenyewe

Tatizo kwa wanaume wengi sikuhizi ni kushindwa kuchukua namba kutoka kwa mwanamke na huishia kuomba namba hizo kwa marafiki zake, jambo ambalo mara nyingi huishia pabaya ama kuchukua muda mrefu kwa mwanamke kukuamini. Kama unataka kufahamu jinsi ya kuchukua namba kwa mwanamke unayemzimia kwa uharaka, kwanza unafaa kujua kujenga msingi kati yenu. Kama hauwezi, basi si muhali kwako kufanikiwa kuuteka moyo wa mwanamke na kutimiza malengo yako.


TEKA HISIA ZAKE KWA KUTUMIA MAUJANJA RAHISI TULIYOYAKUANDIA
1. Mpe muda wote aongee
Hakikisha unamwangalia machoni mwake wakati wote anapokuwa akiongea na umakinike kwa kumsikiliza kila atakachoongea. Yachukue maneno yake yote na uweke hisia zako vile inavyotakikana. Jambo muhimu linalotakikana hapa ni kuhakikisha kuwa unampa nafasi aongee kila kitu anachotaka yeye bila hivyo ataona kuwa msingi wako na yeye haufai ama kutokuwa na maana. Kama ni mwanamke asiyependa kuongea sana basi makinika na ishara zake anazozifanya na pia miondoko ya macho yake.[Soma: Jinsi ya kuongea na mwanamke mpaka umvutie]

2. Msikilize kwa umakini
Hakikisha umemakinika wakati wote mnapokuwa mnaongea, na kuchukua baadhi ya maneno anayoongea ili uweze kuyapanua baadae katika maongezi yenu. Ukimakinika zaidi kunasaidia kwa sababu kutatoa fursa ya kuleta maongezi ambayo yanahusiana na yakuvutia ambayo yatampendeza huyo mwanamke. Fahamu ya kuwa wakati mwanamke anapoongea ama kutoa stori yake, ni dhahiri kuwa wakati mmoja au mwingine mnaweza kuwa na mfanano wa matukio yanayohusiana so ni vyema kumakinika ili kuweza kujenga stori za pamoja. Hii itakusaidia wewe kuweza kumfanya mwanamke kukupenda na kukuamini. Atakupenda kwa urahisi bila hata wewe kutokwa na kijasho. [Soma: Makosa unayoyafanya kwa SMS ambayo yanamfanya mwanamke akucheke]

3. Muulizie namba yake
Unless hutaki kuchukua hatua zaidi yapo, then unahitajika kumwomba namba yake finally. Hii itakuja automatically yenyewe wakati umemaliza na kutimiza hatua ya kwanza na ya pili bila wasiwasi. Hii haiwezi kuwa tatizo kwani tayari ushajenga msingi ambao unamfanya mwanamke akupende. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanamke ambaye humjui]

Kama unashindwa utatumia ujuzi gani wa urahisi kuomba namba yake basi fanya hivi. Katika hatua ya kwanza na ya pili ya maujanja haya, itakuwa tayari ushafahamu mengi kumhusu huyu mwanamke so unaweza kuleta issue moja ambayo ashawahi kuitaja wakati flani. Mfano kama ashawahi kutaja anapenda kutembea then mwambie "Naona tunafaa siku moja tutembee pamoja". Wakati mwingine mwanamke anaweza kuanzisha swala kama hili wa kwanza, so akikubali unamwomba namba yake fasta. Hawezi kukunyima. [Soma: Hatua mbadala za kumwomba mwanamke simu]

So kama kweli wataka kujua kuchukua namba kutoka kwa mwanamke, achana na porojo na mbinu wasiwasi za marafiki zako wanazozitumia ambazo mara nyingi hazifaulu. Pia sahau zile mbinu zote unaziona katika sinema. Kando na kuwa mwanamke anaweza kukupenda, lazima ujenge msingi ambao utamfanya mwanamke yeyote kujiskia huru na wewe -jambo ambalo wanaume wengi hukosea kufanya.[Soma: Makosa wanaume huwafanyia wanawake hadi wakatemwa]
Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupatie Namba Yake Yeye Mwenyewe Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupatie Namba Yake Yeye Mwenyewe Reviewed by Admin on 8:05 PM Rating: 5

1 comment:

  1. Wewe kweli mtaalamu Makala nzuri, unakaribishwa kuandika makala nzuri kama hizi ulipwe bonyeza jina langu hapo kushoto kuanza kuandika ili ulipwe. Tunataka waandishi kama nyie katika jamii

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.