Mfanye Mwanamke Ajisalimishe Kwako Na Mbinu Ya 'Sheria ya Utwekaji'


Je ushawahi kupatikana katika hali ambayo unampenda mwanamke flani lakini yeye hakupendi? Umejaribu uwezo wako wote wa kumpendeza lakini huoni ukivuna matunda yeyote?

Mbaya zaidi ni kuwa umechoshwa kwa kuwa umepoteza muda wako kumtoa deti na kutumia pesa zako, halafu mwanamke anatoa VISABABU vya kuwa hajiskii kutoka deti nyingine na wewe.

(Psss...usiendelee kusoma zaidi kama hujasoma makala ya kwanza ya chapisho hili.


Unajihisi kana kwamba wanawake hawathamini kile ambacho unawafanyia.

Ok hii ni kawaida kwa sababu wanaume karibu wote KILA MARA hufanya jambo moja au jingine kwa mwanamke na huwa mwishowe HAWAPATI kitu.

Nakumbuka hii stori ya rafiki yangu flani ambaye aliingizwa katika 'friend zone' na mwanamke kiasi cha kuwa alishindwa kujinasua.
Siku moja alialikwa na huyu 'dem aliyemkufia' siku ya Jumapili kwenda kumsaidia kuhamisha vyombo vyake hadi kwa nyumba mpya aliyokuwa akihamia hapo.

Ili kuonyesha upendo wake kwake aliamua kumsaidia na ilimchukua zaidi ya masaa 8 akiwa katika hio shughli ya kuhamisha vyombo.

Katika hali ya kuchoka na kutokwa jasho huku akitengeneza runinga na dvd, huyo mwanamke aliyekuwa 'akimzimia' alipigiwa simu na MWANAUME MWINGINE...ambaye alitaka kukutana naye (nawezasema ilikuwa kama kutoka out vile)

Na hivi ndivyo alivyomwambia rafiki yangu, "Je itakuwa sawa kama nitatoka kwa muda?"

Na (kama mjinga) alimjibu "Ok. hakuna tatizo, wewe nenda... Nitamaliza kukutengenezea kila kitu chako..."

(Huyo mwanamke hakurudi huo usiku...alianza kutoka deti na huyo 'mwanaume mwingine' na beste yangu akasahaulika...)

Well, hii ni hali ambayo wanaume hufanyika wakati ambapo wanaitishwa usaidizi ama hisani(favours) kutoka kwa wanawake.

Mwanaume atasema "Sawa, hakuna shida! Unataka nini? Nitakufanyia!"

Ok. Najua unaelewa namaanisha nini...

Unampenda mwanamke kiasi cha kuwa uko kando yake wakati ambapo anakuhitaji, lakini anakuona wewe kama rafiki, na hakuna cha ziada...

Unatoka deti na wanawake na unatumia pesa zako ambazo ulizitolea jasho jingi, lakini unaonekana kana kwamba wanakufanyia hisani kwa kuwa na wewe wakati huo wote...

Kama unajihisi ya kuwa unajitahidi kuhakikisha ya kuwa unawafanyia mazuri wanawake lakini hawathamini kitu...

Basi ni wakati wa kutumia Mbinu ya Mpatanishi inayoitwa "I.O.U.s."

Mbinu hii kwa jina jingine inaitwa "Sheria ya Utwekaji" (ambayo inaweza kuwa na nguvu NZITO iwapo utaitumia kwa wanawake...)

Inajikita na sheria halisia za binadamu: wakati mtu anakupatia kitu chenye thamani, ama kukufanyia hisani, kikawaida tunajihisi kana kwamba tuna majukumu ya kurudisha asante kwa jambo tulilofanyiwa.

Inatufanya tusijiskie huru iwapo tunafikiria ya kuwa kuna mtu anatudai jambo ama kitu flani. Huwa tunajaribu kulipa.

Kuna mfano mzuri wa kuelezea mbinu hii...

Kuna jamaa alimteka nyara mpenzi wake wa zamani na watoto wake na alikuwa amebanwa ndani ya nyumba huku ameshikilia AK-47...

Nyumba imezungukwa na jeshi la polisi...

Helikopter ya polisi ilikuwa inazungukazunguka nyumba hio...

Na katika hali hii ya mkazo, kazi ya mpatanishi ilikuwa ni KUMSHAWISHI mpaka ateke amana yake kwake na kumfanya kujihisi kama yuko UPANDE WAKE.

Mapema katika upatanishi wake, alimwambia mtekaji nyara maneno haya kupitia kwa simu, "Nataka ujue, Papito, Nitahakikisha ya kuwa hakuna mtu atakata umeme ndani ya nyumba, ama kujaribu kukuchokoza."

Baadae kidogo, yule mpatanishi akamwambia, "Papito, kama unahisi njaa ama kiu, nijulishe na nitajua hatua ambayo nitakuchukulia."

Hapa. jeshi la polisi halikuwa na nia ya kukata umeme katika nyumba...na huwa ni kawaida kwa polisi kupeleka chakula na maji...lakini huyu mpatanishi amefanya kana kwamba ni YEYE ndie anamfanyia Papito hisani.

Huyu mpatanishi ametumia msururu wa "I.O.U.s" ili kumfanya Papito ajihisi kana kwamba anafuata njia yake ili kumsaidia.

Halafu baadae, wakati Papito aliagiza paketi ya sigara...

Huyu mpatanishi "aliitisha" moja ya hisani ambayo alikuwa "akimdai"

Alimwambia hivi: "Naona unahitaji kutumiwa sigara, Papito, lakini pia nitakuhitaji uwatoe watoto kutoka kwa nyumba, sawa? Nimekuwa nikikutumikia, na sasa nakuhitaji unitumikie na mimi."

Bila kuchelewa Papito aliwaachilia watoto...

Na saa moja baadae...wakati wameshabadilishana 'hisani' zaidi na mpatanishi...Papito alitoka kwa nyumba huku mikono yake iko juu ya hewa akijisalimisha kwa amani. Hakuna mtu alidhuhurika.

So mbinu hii itatumika vipi kwa mwanamke?

Wakati ambapo mwanamke ataagiza kutaka kitu kutoka kwako hufai kukubaliana naye hapo hapo.

Badala yake, tengeneza "I.O.U.s" ambazo utazifaidi mbeleni.

Kuna mbinu nyingi zisizokuwa na mwisho za kufanikisha hivi...na utakuwa unatengeneza MAHITAJI ambayo yatamfanya ajitweke.

(Hii ni saikolojia ya binadamu, hufanya kazi kama hirizi)

Mfano #1 
Namchukua mwanamke kwenda deti naye. Anaanza kuichokora radio, akibadilishabadilisha stesheni...

Namwambia "Unajua, Mamito, kawaida huwa siruhusu mtu yeyote kuchagua nyimbo katika gari langu...lakini kwa sababu yako tu nimeamua kukuachia. Lakini kwa sharti moja...ukiweka nyimbo za Justin Bieber itabidi nikushukishe barabarani. Nakuenjoy...endelea. But niko serious, usiweke Justin Beiber, na ni kwa leo pekee.

Mfano #2
Tunaingia katika mkahawa. Tunatembea katika meza ambayo haina mtu, halafu anaanza kukaa kwa kiti...

Natabasamu na kumwambia, "Duh!, umekalia sehemu ambayo wakati wote huwa mimi nakalia nikija katika hii meza. Lakini hakuna tatizo, wewe endelea tu...Nimekuruhusia ukae katika sehemu hio kwa leo...kwa sababu umependeza sana na hio nguo umevalia halafu pia nimependezwa kukuona umevalia vizuri usiku wa leo."

Mfano #3
Nampigia mwanamke simu kupanga deti ya kwanza na yeye usiku wa Alhamisi. Anauliza: "Tutaenda wapi?" Namjibu: "Well, kuna sehemu moja kali ambayo haijulikani huwa naenda huko kila Alhamisi...ni kama sehemu yangu ya siri ninayoenda kwa sababu watu wengi hawaifahamu... lakini unaonekana uko poa, so nimeamua kukuchukua twende huko ---bora tu usiambie marafiki zako kuhusu hio sehemu. Umekubaliana?"

(Unagundua kiolezo hapa: unabadilisha 'maagizo ya kawaida' kuonekana kama HISANI ambazo utakuwa unamdai...)

Ok, usitumie sana mbinu hii, but wakati ambapo umekusanya 'I.O.U.s' za kutosha, itakuwa RAHISI kwako kupewa busu mwisho wa usiku...

Ama, unaweza kumfanya akakualika kwa nyumba yake upate ZAIDI...

Wakati unamrudisha kwake (haswa kama unaenda kumuacha huko), unaweza kumwambia: "Nimekuachia ukachagua musiki katika gari langu...Nikakupatia kiti changu cha kawaida ambacho nakitumia kila wakati katika ule mkahawa...NA nikakupeleka katika sehemu yangu ya siri ya Alhamisi ambayo hujificha huko...so sahizi unahitajika unialike kwako angalau unikaribishe na kinywaji."

Hapa ndipo sasa 'Sheria ya Utwekaji' inaingia kufanya kazi. Atakualika kwake...halafu utumie mbinu tulizokufundisha awali kumaliza mchezo mzima.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.